Ngoja nikujibu taratibu, ada za watoto unalipa wewe kwa sababu una afya sasa waliopoteza wazazi wao au walezi?. Sisi tuna uchumi gani wa watu kutuonea wivu?? budget zetu tu 40% nyingi. Uonewe wivu kwa lipi? turudi kwenye uchumi je USA, EU au China watuogope sisi? South Africa yenye uchumi mkubwa Africa na Nigeria wamechukuwa hatua kulinda watu wao na chanjo wamenunua. SA huyu mdudu mpya walitangazia dunia kuwa kuna issue mpya hapa kwetu, unadhani hawaogopi uchumi wao? lakini wanajuwa jirani yako akiwa mgonjwa na wewe utakuwa mgonjwa. Tofauti ni ndogo tu, hizi nchi zina akiba ya pesa na uchumi unaweza kuhimili, sisi hatuna kitu hatuna pesa huo ndio ukweli na alisema yeye corona ya kwanza siwezi kufunga Dar huko tunakusanya pesa, sawa hakuna mtu amesema hapa lockdown ila zuia mambo yasiyo na lazima sio kila siku nyimbo hawataki tuzae unadhani hao wazungu wangekuwa wanataka kutudhuru wangetudhuru watoto bado kwenye chanjo sio jitu umezaa mpaka basi ndio waje kukudhuru kwa lipi? ok wazungu wabaya na hawa viongozi wengine wa Africa walioona kuna shida hapa nao vichaa na wabaya. Rwanda kinchi kidogo uchumi mdogo lakini wameona hatari mbele yao. na kule kujitapa hata tukikaa miezi 5 bila kufanya kazi tutakula tu pesa tunayo, yako wapi sasa???