Hapana B
Jamani wa Tanzania tumemkosea nini Mungu?? hivi wewe unaandika kabisa na kujiamini kuwa tunachofanya ni sawa?? Huu ugonjwa sio issue ya Tanzania ni duniani kote chanjo utapiga unataka hutaki ni lazima jeuri yako italeta majanga kwa watu wengine hii sio optional tena, adhabu ya kwanza zitapigwa ban ndege zote kutua hakuna nchi itakayochukuwa risk kuwapelekea ugonjwa mbaya zaidi kuruhusu virus kubaki katika mzunguko ni kuvipa njia ya kujiegeuza na kuunza upya hili halitakubalika. Israel wameshasema jana 71% wamepata chanjo na drop ya wagonjwa 94% na UK number zinashuka USA number zinashuka unataka prove gani, piga marufuku basi na chanjo zote za watoto maana huko ndio wangetupa kama wanatutaka waje kutufunga uzazi leo watu wenyewe hata kwa vumbi la congo huna faida. Dunia nzima wako serious ila sisi tu wenye nyimbo ya uchumi wa kati(fake) ndio tuko smart sana? Nailaumu CCM wanaipeleka hii nchi kubaya na tutafika huko kama ZANUPF. tutafika tu ila kurudi ndio kimbembe.