Waziri wa Afya Oman: Asilimia 18% ya wasafiri wanaotokea Tanzania wamekutwa na maambukizi ya virusi vya corona, tunafikiria kusitisha safari za ndege

Watakuwa wanatumiwa tu na mabeberu waarabu koko hao.

Hizi ni chuki tu za mabeberu kwa kipenzi cha Mungu Dkt JPM.

Watakuwa wanatuonea wivu tu kwa kuwa tuko uchumi wa kati.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Ndio unasema uongo.
 
Dunia nzima tujifunze kuishi na hivi vijimafua visivyo na madhara yoyote kwa binadamu, kuzuia watu kusafiri au lockdown haiwezi kuwa suluhisho make hivi vijimafua bado vipo vipo saaana tu!
Wewe kama nani unaiambia dunia?
 
Watu wanalalamika humu, kwanin wasitengeneze chanjo zao wenyew ?wamekalia kulalamika mara ooh Wazungu wanataka watuue, Sasa najiulz mnaopinga chanjo si mtengeneze yenu?
 
Dunia nzima tujifunze kuishi na hivi vijimafua visivyo na madhara yoyote kwa binadamu, kuzuia watu kusafiri au lockdown haiwezi kuwa suluhisho make hivi vijimafua bado vipo vipo saaana tu!
Una maanisha kama huyu mhandisi?
Kwani ukiwahi kusikia kuwa tuna vipimo vya corona?
Vyetu huwa vya mbuzi na mapapai. Siyo vya watu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Mbona hawafi wala kuumwa sasa hao wasafiri?
 
Kumbe waTanzania wenye angalau akili kichwani bado mpo, safi sana..
 
18% tu alafu unasitisha safari?? Yeye nchini kwake maambukizi ni % ngapi??

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Watu wanalalamika humu, kwanin wasitengeneze chanjo zao wenyew ?wamekalia kulalamika mara ooh Wazungu wanataka watuue, Sasa najiulz mnaopinga chanjo si mtengeneze yenu?

Tuuliwe tuna nini? ARV tu ni kwa hisani ya watu wa huko huko? Achilia mbali vyandarua?

Kujikinga mwambafy kwingine, khaaa! Mbona hata kichefu chefu?

Au nasema uongo ndugu zangu?
 

Sasa huo ni mlinganisho wa kimahesab zaid. Maisha hayako hivyo. Kwan huwez kuwa na rafiki unaweza kufanya nae biashara lakin hamwez kukopeshana? Chanjo hii ina maswali meng kuliko majibu. Iwe kwetu. Iwe kwao. Iwe kwa jiran zao. Afya haijaribiwi. Nijibu kwanini South Africa wameisitisha chanjo? Kweli hili jiongeze maarifa zaidi ya milengo ya kisiasa. Muhim tushirikiane kumwomba Mungu ashughulike na kidudu na aliyetengeneza.
 

Chanjo ya South Africa imesitishwa kwa sababu ufanisi wake kwa virus vipya vya South Africa ni mdogo. Zipo chanjo katika zilizopo zenye ufanisi pia na kwa virus hivi. Iliyositoshwa itaelekezwa kusiko virus vya South Africa. Tatizo like wapi?

Si nchi zote zina virus daraja hili la Africa Kusini ambavyo ni vikali zaidi.

Kwani sisi vya Africa Kusini vipo hapa nchini kwetu pia? Au navyo ni nyara za serikali?

Chanjo haina maswali yoyote zaidi ya kuwa wasio wataalamu wameteka nyara mambo ya ugonjwa huu kwa maslahi binafsi.

Enyi msiokuwa katika makundi yaliyoko hatarini tafadhali fungeni midomo yenu inanuka uvundo! Mna nini cha kufanya nyie au mnawacheza shere tu hawa wanaokufa?
 
Watakuwa wanatumiwa tu na mabeberu waarabu koko hao.

Hizi ni chuki tu za mabeberu kwa kipenzi cha Mungu Dkt JPM.

Watakuwa wanatuonea wivu tu kwa kuwa tuko uchumi wa kati.

Au nasema uongo ndugu zangu?unasema ujinga wa kiwango cha juuu
 
Ndio unasema uongo.

Basi kama ninasema uongo, ukweli ni kuwa:

Hayupo beberu wala mtumiwa na beberu. Tuna gonjwa ndani ya nchi. Gonjwa hili na tulikabili vinginevyo tunachofanya ni kujidanganya tu.

Better late than never!

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Hakuna anayependa mtanzania afe. Nchi hii haijawai kuzalisha shetan. Naamin kupitia chanjo hata wewe huna uhakika kuwa watu hawatakufa. Kuwa umepata suluhisho. Sio tiba ile. Haijathibitishwa ipasavyo. MRNA sio kama chanjo nyingine ulizotolea mfano. Ni bora nusu shari kuliko shari kamili. Katika vita kuna askar hupotea pia. Mashujaa. Tumetupiwa tatzo. Tulikabili kwa namna hatutazalisha tatzo kubwa zaid. Tena la kudumu.
 

Huu ugonjwa unauwa zaidi wazee na wenye magonjwa mengine. Kundi jingine la walioko hatarini ni wafanyakazi wa afya.

Ujasiri wa kuwaongelea kwa sauti wahanga hawa wanao endelea kufa kama makafara tu hali nyie haliwahusu mnaupata wapi?

Unasema kuepuka mikusanyiko, ila ya uzalishaji hamna shida. Nani alikwambia ya uzalishaji haina maambukizi?

Hivi:



Kwa nini wewe unadhani uko kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuonyesha uelekeo ufaao kuliko wataalamu wetu wa afya?

Ni Tanzania tu ambako vita hivi vimepokwa tokea kwa wataalamu wa afya. Hilo pia halikufikirishi?

Mna maslahi gani kwenye kuhozi vita hivi huku watu wakiendelea kupukutika hivi?

Serikali inajua kuwa kuna janga na ndiyo inaongeza kodi zaidi na kuzipandisha zaidi zilizokuwapo? Ili iweje?

Wapandisha kodi wenyewe ndiyo hawa hawa wasio lipa kodi stahiki au hawakupoteza kodi kabisa?

Mkuu ulichoandika mbona ni bonge la utopolo mtupu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…