Waziri wa Afya Oman: Asilimia 18% ya wasafiri wanaotokea Tanzania wamekutwa na maambukizi ya virusi vya corona, tunafikiria kusitisha safari za ndege

Waziri wa Afya Oman: Asilimia 18% ya wasafiri wanaotokea Tanzania wamekutwa na maambukizi ya virusi vya corona, tunafikiria kusitisha safari za ndege

View attachment 1703573
View attachment 1703577

Waziri wa Afya wa Oman amethibitisha takwimu za maambukizi ya Corona kwa wasafiri wanaotokea nchini Tanzania kuwa katika kiwango cha juu sana, ambapo asilimia 18 ya wasafiri wamekutwa na maambukizi ya virusi hivyo. Waziri huyo amesema wanafikiria kuzuia safari za ndege kutoka nchi zinazoonyesha kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi ya virusi vya corona.
Tanzania tunahujumu Juhudi za Dunia kutokomeza Corona. Tujiandae Kutengwa, maana we zeta wanna banana kwa Hali Na Mali... halafu sisi tumejiachia tu. Tutabaki kwetu kama JPM
 
Hakuna anayependa mtanzania afe. Nchi hii haijawai kuzalisha shetan. Naamin kupitia chanjo hata wewe huna uhakika kuwa watu hawatakufa. Kuwa umepata suluhisho. Sio tiba ile. Haijathibitishwa ipasavyo. MRNA sio kama chanjo nyingine ulizotolea mfano. Ni bora nusu shari kuliko shari kamili. Katika vita kuna askar hupotea pia. Mashujaa. Tumetupiwa tatzo. Tulikabili kwa namna hatutazalisha tatzo kubwa zaid. Tena la kudumu.
Kwa hiyo kati ya chanjo na malimao kipi kimepitishwa na WHO au wapi wamesema chanjo inaua?
 
Usitake kunambia kabla ya hivi vijimafua watu walikuwa hawafi, halaaafu mbona nyinyi waleta tanzia humu hamfi wanakufa mawakili tu?
Daa hivi hizi akili mnatoa wapi hizi? Ko barabarani wanavoongeza torch za matraffic police wanavokataza magari mabovu wanavoweka macctv camera ili kupunguza ajali ili watu wasipate majeraha na vifo na kweli tunaona matokeo leo hii mtu unaleta hoja ya kishamba kama hii eti tutakufa 2.

Kwanini hutembei katikati ya bara bara kama utakufa tu na kwann ukiumwa ujitibu maan si utakufa 2. Ko kwasababu zilikuwepo sababu nyingine za vifo basi tuendelee kuongeza nyingne. Sio kosa lako lakini.
 
Ambacho hujaelewa nini hapo? Wanahofia watu wao wasije wakapata maambukizi unaleta maswali ya ajabu. Kwani kila mtu akiumwa lazima afe? Ko wewe waliokufa tayari unaona sio watu mpaka wakafa? Akili za kishetani hizi
Mbona hata hawaumwi sasa hao wasafiri, wanatest positive tu 😂😂🤷🏽
 
Tanzania tunakiri corona ipo. Hata Abas kashaliweka sawa. Ila tunatofautiana namna ya kukabiliana nayo. Sisi kama nchi hatuko tayar kwa chanjo ambayo haijafanyiwa uhakiki wa kutosha. Hatuko tayar kwa lockdown. Sana sana tuongeze vifaa tiba kama oxygen na watoa huduma wa kutosha ikibid. Tuchukue taadhar za kawaida kama usafi, distancing na barakoa[barakoa si muhim sana]. Tupunguze mikusanyiko isiyo ya lazma[lakin ya kiuzalishaji iendelee]. Pia tuziamin dawa zetu za asili kama kufukiza na limao na tangawizi. na tule vyakula vya kuongeza virutubisho kinga. Tuone kama herd immunity pia itafanya kaz. Tusijiingize kwenye mbinu zinazotugharim kwa tija kidogo. Muhim zaid tupunguze hofu mana huu si ugonjwa wa kuisha leo. Tukabilane nao. Lawana na laana ziwaendee waliotengeneza hiyo virus kwa maslahi yao.
Wewe umeweka point ambazo mimi nilishindwa kuziweka kwenye moja ya thread nilizochangia

Umeongea ukweli ulio wazi na hiki ndicho inachomaanisha serikali

Sema wale wanaojijua wanauwezo wa kukaa ndani mwaka mzima bila kuhangaika na chakula ndo wanataka lockdown, hawajui kwamba kuna watu tukikaa home siku moja tu tunashinda njaa
 
Hizo tiba za asili za malimao na kujifukizia zilijaribiwa wapi na lini zikaonyesha mafanikio?Na hayo mafanikio yalikuwa ni asilimia ngapi?Halafu hizo njia ulizotaja hapo juu mbona hazisaidii chochote?Kwa sababu watu wanazidi kupukutika deile!Ni sahihi kuendelea kukumbatia njia ambazo badala ya kusaidia watu zinaua watu?
Acha tufe tu ili dunia ibaki na watu wachache

Au we unaogopa kufa mkuu?
 
Hizo tiba za asili za malimao na kujifukizia zilijaribiwa wapi na lini zikaonyesha mafanikio?Na hayo mafanikio yalikuwa ni asilimia ngapi?Halafu hizo njia ulizotaja hapo juu mbona hazisaidii chochote?Kwa sababu watu wanazidi kupukutika deile!Ni sahihi kuendelea kukumbatia njia ambazo badala ya kusaidia watu zinaua watu?

Dah....mkuu tafuta buku 20...
Mimi nitakuongezea laki2...tuagize chanjo yako [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Daa hivi hizi akili mnatoa wapi hizi? Ko barabarani wanavoongeza torch za matraffic police wanavokataza magari mabovu wanavoweka macctv camera ili kupunguza ajali ili watu wasipate majeraha na vifo na kweli tunaona matokeo leo hii mtu unaleta hoja ya kishamba kama hii eti tutakufa 2..kwanini hutembei katikati ya bara bara kama utakufa tu na kwann ukiumwa ujitibu maan si utakufa 2. Ko kwasababu zilikuwepo sababu nyingine za vifo basi tuendelee kuongeza nyingne. Sio kosa lako lakini..
Kwa hiyo babu unataka tupigwe lockdown na serikali si ndio?
 
Lazima nisiijue kwani nina shida ya kukimbilia ubeligiji mie .....we ijue eapoti hadi ya ahera ila chanjo mkapapasiwe hukohuko mnapotaka kwenda
Mhh huo mwandiko umenishtua na nimekuelewa mtu wa aina gani Naby Keita. siku njema
 
Na ndio nikauliza, wote hao mbona hawaumwi, si angeumwa hata wawili watatu basi...🤷🏽, au huo ugonjwa ukoje kwani? 😂😂
Mkuu kuna elimu ya huu ugonjwa watu hawapewi vya kutosha. Kupata corona sio lazima uumwe unaweza ukawa positive na usijue kabisa tatizo unaweza kumuambukiza mtu bila kujuwa na huyo mtu akapata shida sana hata kupoteza maisha sababu watu tunatofautiana. chukulia mtu kabeba virus bila kujuwa kapelekea wazazi wake watu wazima ua kati ya family yake ukawachukuwa vibaya wakapoteza maisha au kuteseka. hatari ya ugonjwa huu ni dalili zake kuchukuwa muda ndio maana unaambiwa ukae siku 14. Oman wamekuja na number hizi kwa sababu ukifika Oman inabidi ulipe dola 70 wanachukuwa kipimo cha PCR halafu unatakiwa uchukuwe Hotel kwa hesabu yako ukae ukisubiri majibu siku ya pili unatumiwa majibu yakiwa mazuri ndio unaenda unakoenda ukiwa positive inabidi ukae quarantine hesabu yako hotelini. ndege ikitoka Tz wanachukuliwa vipimo hata kama una certificate ya negative sasa hapo ndio majibu yanatoka katika kila abiria 100 kumi na nane yanatoka positive. Na hii wanafanyiwa abiria wote ncho zote. sampling kama hii ni kama kusema 18% ya watanzania wana corona, kuumwa au kutokuumwa sio issue wengi wanapata bila kujuwa kabisa hatari yake kumuambukiza mtu dhaifu. tujikinge sisi na family zetu na majirani zetu na hata tusiowajuwa.
 
Na sisi sasa hatuwauzii majini kama unyama unyama tu/
Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kwani wanapo ondoka hawapimwi jamani? Basi ukimjua adui tafuta mbinu anazotumia ili asikudukue mapema, viongozi fanyeni kazi yenu!
Wapimwe kwa kutumia vipimo vipi? Maana mkuu alishasema vipimo vyote ni feki kwahiyo vinaonesha majibu yasiyo sahihi hivyo kutupilia mbali zoezi la upinaji tangu April mwaka jana
 
Back
Top Bottom