Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, aagiza kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na Meneja udhibiti na ubora

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, aagiza kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na Meneja udhibiti na ubora

Hongera zake ingawa hii kamati haipo sawa/huru kwa sababu imesheheni wataalamu wetu wa afya ambao wanaweza kulindana kwa namna moja au nyingine. Ingekuwa vyema kama wataalamu wa kada zingine wangewekwa katika kamati hiyo ili kuweka mizani katika hali ya usawa.
Soma vizuri bro.
SUA,Mandela,Tmda,ni wataalam wa afya hao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mgonjwa mathalani wa moyo amezidiwa, kakimbizwa hospitali, madaktali hawamtibu hadi wajiridhishe na hali yake kuhusu corona, machine inachunguzwa, watu wa maabara wapo chini ya uchunguzi....

Nini hatma ya wagonjwa, hasa waliozidiwa?

Hatima yao sote tunaijua, tuwaongoze sala ya toba tu.
 
Ivi ni kweli papai limepimwa likakutwa na corona,,? Haini ingii akilini.
Majimaji yake yalipelekwa kama sampuli ya kupimwa na yakapimwa!!
Baba mwenye nyumba kashasema sasa wewe ikuingie akilini au ikatae ndo keshasema......tutulie tu tunyolewe mwanawane…………… Nifanyieni booking Chatto nikapumzishe akili mie.
 
Tatizo lako naliona, ni kuwa mpo tofauti na mawazo ya Magufuli. Wewe unataka kuona kama machine yetu hapa TZ zinatoa majibu halisi, wakati yeye anaamini machine zipo Sawa ila majibu yanahujumiwa ili tuonekane hapa Tanzania kuna wagonjwa wengi. Kwa hitaji lake alikuwa na option mbili ya kwanza kama unayofikiria na ya pili ni kukonfuse hiyo machine ili aone ni nini! Kwa Magufuli sample ya mbuzi kukutwa na coronavirus anadhani aidha wapimaji wamehongwa wanajitolea data tu (usisahau vijijini ulipokuwa enzi zile unapima malaria wengi waliandikiwa ipo), au vifaa vinavyotumika vimewekewa corona kimakusudi na waliotuuzia. Hivyo kwake papai kukutwa positive ni kuonesha si machine ila ni hila
Alishauri nchi zingine pia zipime papai! 🤣🤣
 
MA
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwasimamisha kazi Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Jacob Lusekelo na Meneja uthibiti na ubora ili kupisha uchunguzi.

Sasa wameanza kushughulika na wataalam badala ya kudeal na Corona

View attachment 1439553
mabeberu sio watu wazuri wanamtumia kila mtu kutoa matokeo hasi na wanatuonea wivu sana hadi wanawatumia watu wa Maabara.
 
Mambo mengine nivizuri kutumia busara kuya kabili hapa tumesha watoa imani watu watu hawajui sasa klpi ni sahihi haya mambo ni technical sana tena world Wise tuna haribu
 
Nlifikir kamati ya kuingia chimbo kutafta dawa. Kama majibu anayo anko kuna haja gani ya kuharibu pesa?

Hapo hakuna atakayekuja na majibu tofauti na yaliyotolewa jana na anko.
 
Ivi ni kweli papai limepimwa likakutwa na corona,,? Haini ingii akilini.
Inaweza isiingie Akili yako lakini kwa alibukua vizuri sayansi inaingia fresh tu. Inaitwa false positive FP ama false negative FN pale unapotumia sampuli isiofaa
 
ushauri kwa wanaoanzisha mada wanatakiwa kuwa neutral kuacha wasomaji watafsiri kwa muono wao na si kuanzisha mada na kuwaelekeza wapi wapite. mfano

"Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwasimamisha kazi Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Jacob Lusekelo na Meneja uthibiti na ubora ili kupisha uchunguzi.

Sasa wameanza kushughulika na wataalam badala ya kudeal na Corona".
HAPA KUNA SHIDA HISIA ZIMEMZIDI AKILI
 
Hongera zake ingawa hii kamati haipo sawa/huru kwa sababu imesheheni wataalamu wetu wa afya ambao wanaweza kulindana kwa namna moja au nyingine. Ingekuwa vyema kama wataalamu wa kada zingine wangewekwa katika kamati hiyo ili kuweka mizani katika hali ya usawa.
Hilo nalo ni neno!
Pia wangeshirikisha wataalamu toka WHO au Namibia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwasimamisha kazi Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Jacob Lusekelo na Meneja uthibiti na ubora ili kupisha uchunguzi.

Sasa wameanza kushughulika na wataalam badala ya kudeal na Corona

View attachment 1439553
Safi sana Umy Mwalimu kuna Watu wanatumika kuidhalilisha taaluma yetu, tunasoma miaka 4 harafu jitu moja linasababisha tuonekane si wazalendo.
 
Safi sana Umy Mwalimu kuna Watu wanatumika kuidhalilisha taaluma yetu, tunasoma miaka 4 harafu jitu moja linasababisha tuonekane si wazalendo.
Kwa hiyo wamehongwa na mabeberu siyo ?Mabeberu hawa hawa wanaowapa ARV za bure ?
 
ushauri kwa wanaoanzisha mada wanatakiwa kuwa neutral kuacha wasomaji watafsiri kwa muono wao na si kuanzisha mada na kuwaelekeza wapi wapite. mfano

"Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwasimamisha kazi Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Jacob Lusekelo na Meneja uthibiti na ubora ili kupisha uchunguzi.

Sasa wameanza kushughulika na wataalam badala ya kudeal na Corona".
HAPA KUNA SHIDA HISIA ZIMEMZIDI AKILI
Exactly👊👊👊...Nimeshangaa kuna watu walitaka serikali ikae kimya kwa hili...Mtoa mada yeye anaona wakifanya hivi basi hawadeal na #covid19.
 
Back
Top Bottom