Tatizo lako naliona, ni kuwa mpo tofauti na mawazo ya Magufuli. Wewe unataka kuona kama machine yetu hapa TZ zinatoa majibu halisi, wakati yeye anaamini machine zipo Sawa ila majibu yanahujumiwa ili tuonekane hapa Tanzania kuna wagonjwa wengi. Kwa hitaji lake alikuwa na option mbili ya kwanza kama unayofikiria na ya pili ni kukonfuse hiyo machine ili aone ni nini! Kwa Magufuli sample ya mbuzi kukutwa na coronavirus anadhani aidha wapimaji wamehongwa wanajitolea data tu (usisahau vijijini ulipokuwa enzi zile unapima malaria wengi waliandikiwa ipo), au vifaa vinavyotumika vimewekewa corona kimakusudi na waliotuuzia. Hivyo kwake papai kukutwa positive ni kuonesha si machine ila ni hila