Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu: Wagonjwa 37 wamethibitishwa kupona virusi vya Corona na wameruhusiwa kwenda nyumbani

Naona unaumia sana, kwanini uteseke?

Nawahurumia mno watanzania ukiwemo na wewe usieteseka....Aise hapa ni kumtegemea Mungu tu na si chochote....mijitu yenyewe haifuati agizo la wataalamu wetu, stand za mabus, makanisa, mabar, minada haifungwi unategemea nini!!


Mungu atulinde
 
Amina. Ila kibaya sasa, kuna watu wanaumia na kuteseka na kusononeka sana wanaposikia habari njema juu ya hilo gonjwa, wanaumia sana, tena watz wenzetu, sijui wanashida gani...
Hao watu niwakina nani. mbona mnapenda sana kusemea watu au kulisha watu maneno kwa hisia zenu binafsi zakijinga.Wenye akili wanafikiria namna yakupambana na huu ugonjwa wewe bado unawaza watu.
 
Hao watu niwakina nani. mbona mnapenda sana kusemea watu au kulisha watu maneno kwa hisia zenu binafsi zakijinga.Wenye akili wanafikiria namna yakupambana na huu ugonjwa wewe bado unawaza watu.
Angalia comments za wadau kama wewe huko juu, kwanini mnateseka lakini, mnaumia nini hasa?
 
Hakuna chochote hpo kunawengine turikua fresh tu nimafua ya kawaida tu afu tunawekwa karantini yanii hotuba ya Jana ya mweshimiwa rais ndio imetuacha huru Leo
Mungu awaweke huru kwelikweli.
 
Wale waliotoroka pale Amana baada ya kutelekezwa na mamlaka husika huku wenzao wakiwafia mikononi, wameingizwa katika hii listi ya walioruhusiwa?
Nitoe ushauri tu, wale mnaojihisi roho zenu kuwasuta kwa kuwasaliti watanzania wenzenu kutokana kulazimishwa kufata amri kutoka juu ni bora muachie ngazi. Mkifanya hivyo mtakuwa mmezitendea haki nafsi zenu na Watanzania wezenu.
 
Boss Return Of Undertaker Ni jambo jema na la kufurahia, Ndugu zetu kupona na tunawaombea wote wanaoumwa wapate kupona, maana ni hazina ya Taifa.

Ila kuna kitu kinanikwazwa sana, Kwanini kila kitu kinafanyika mpaka Rais aseme??? !!! Ni kuwa Watendaji wetu hawajui majukumu na wajibu wao???? !!! Yaani Mh. Rais asiposema, Mambo hayawezi kwenda ??? !!!

Binafsi, nampongeza sana Mh. Rais kwa Udhubutu wake aisee, Ila namwomba kitu, Asione Chadema na Upinzani kama ndio wakwamisha Maendeleo, Asione Mitandao ya Kijamii kama ndio wakwamisha Maendeleo, Yaani atumie Chadema na Mitandao ya Kijamii kama Source zake za Information kama Back Up Information.

 
amina
 
Huu ugonjwa unaathiri watu, unaathiri uchumi wa watu. Tukiujadili ni ili kulinda watu.Unataka tuseme vipepeo wamepona?..Ukiwa mkosoaji mzuri jifunze kufikiri vizuri.
 
Hahahahaha we mjamaa hujipendi, hujui kwamba tumekatazwa kutoa takwimu za uongo..?
Wanapopatikanna watatangazwa kama kawaida Rais alisema wasitangazwe tu walioonngezeka,watangaze na wanaopona ili kuwaonndoa hofu kubwa wananchi,tutakuwa na Imani kuwa kumbe wanapona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…