Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu: Wagonjwa 37 wamethibitishwa kupona virusi vya Corona na wameruhusiwa kwenda nyumbani

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu: Wagonjwa 37 wamethibitishwa kupona virusi vya Corona na wameruhusiwa kwenda nyumbani

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hadi sasa jumla ya Wagonjwa waliopona ni 48 ambao ni kati ya Wagonjwa 108 waliothibitika kuwa na Ugonjwa huo, ila kwa sasa hawana dalili

Amesma, "Tuna vifo 10, na hivyo tukabakiwa na wagonjwa 274 na kati ya 11 tumeshawatolea taarifa kuwa wamepona. Ni kweli kama alivyosema Rais Magufuli katika watu 263 waliobaki, 108 hawana ugonjwa wowote"

Ameongeza, "Watua hao 108, hawana homa, kifua, kikohozi wala chochote, ila tuliwazuia katika vitua ili kusubiri vipimo vya mwisho na kuthibitisha kama hawana maambukizi kabla ya kuwaruhusu kwenda nyumbani."

Amesema leo wameruhusu watu 37, na kuwa vipimo vyao vimeonesha hawana maambukizi ya #COVID19. Ametoa wito kwa jamii kuwa isiwanyanyapae na kuongeza kuwa wengine 71 vipimo vyao vinasubiri siku 2-3 wataruhusiwa kurudi nyumbani

 
Tunahitaji maendeleo ya matokeo ya utafiti wa dawa za asili hizo takwimu hata BBC tutazipata.
 
Back
Top Bottom