#COVID19 Waziri wa Afya: Watu 408 wamebainika kuwa na Corona , 284 wakiwa katika mashine za oksijeni

#COVID19 Waziri wa Afya: Watu 408 wamebainika kuwa na Corona , 284 wakiwa katika mashine za oksijeni

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amesema hadi kufikia Julai 8, 2021 jumla watu 408 walibainika kuwa na ugonjwa wa corona huku 284 wakitumia mitungi ya oksijeni.

Dk Gwajima ametoa taarifa hiyo leo Jumamosi Julai 10, 2021 wakati akitoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kwenye mnada wa Msalato jijini Dodoma.

Kwa upande wa Mkoa wa Dodoma, Waziri huyo amesema hadi kufikia Julai 8, 2012, jumla ya watu 26 waligundulika kuwa na ugonjwa huo huku 22 wakiwa katika mitungi ya oksijeni.

Wakati huo huo, Dk Gwajima na kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka wametembea umbali wa kilometa nne lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kuvaa barakoa ili kujikinga na maambukizi.
=====

Ni wakati sasa wa Wananchi na asasi na taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali kushirikiana na serikali katika kutekeleza na kuhamasisha maelekezo ya wataalamu wa afya juu ya hatua za kukabiliana na ugonjwa huu.

215513749_10159494182949339_7610896480387748996_n.jpg
214148503_4266395070085545_417713494375459152_n.jpg
 
Waziri wa Afya, Dk Dorothy Gwajima amesema watu 408 wamebainika kuwa na ugonjwa wa corona nchini huku 284 wakiwa katika mashine za oksijeni
Sijui Mh. Rais alikubalije kuendelea na huyu waziri comedian!!! Huyu mama hajitambui, na wananchi hatumsikilizi maana alikuwa kituko kipindi cha Jiwe.
 
Sijui Mh. Rais alikubalije kuendelea na huyu waziri comedian!!! Huyu mama hajitambui, na wananchi hatumsikilizi maana alikuwa kituko kipindi cha Jiwe.
.
Kuendelea kuwepo kwake kuongoza mapambano haya kunakwamisha mapambano yenyewe. Kuna kazi kubwa mno ya kurekebisha uharibifu, kufuta imani potofu zilizojengwa kuhusu covid. Akili ya kawaida ingetegemea hii kazi si ya kuongozwa na yoyote ambaye akizungumza haaminiki. Anaweza kuwa waziri mzuri tu lakini kwa hili ni liability.
 
Serikali ya Samia soon inakwenda kuwaweka ndani wanyonge ...hakuna beberu anayekubali kujenga banda then mifugo ikaendelea kuzulula tu
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Dk Dorothy Gwajima amesema watu 408 wamebainika kuwa na ugonjwa wa Corona (Covid-19) nchini huku 284 wakiwa katika mashine za oksijeni.

Ni wakati sasa wa Wananchi na asasi na taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali kushirikiana na serikali katika kutekeleza na kuhamasisha maelekezo ya wataalamu wa afya juu ya hatua za kukabiliana na ugonjwa huu.

View attachment 1848604 View attachment 1848605
Baada ya kubanwa mbavu na mabeberu sasa wameanza kuzungumza ukweli
 
Back
Top Bottom