Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hao waliobaki mbona haelezi wako wapi
Ataje na hospitali zinazowahudumia
Hii ni hatari tuchukue taadhari
Takwimu hazipo detailed, utafikiri primary school pupil ndo ametoa.
Wagonjwa 408 ni wachache sana ni sawa na asilimia 0.000742 ya watanzania wote. Wakifika asilimia moja mnijulishe nianze Kuvaa barakoa.Watu 400 tu!
Kuna nchi kila siku maambukizi ni zaidi ya 500 na lockdown hamna.
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Tufate maagizo ya waziri inatosha.Tuwafurahishe vizuri watoa pesa,lockdown itakosha mioyo yao.
Wagonjwa 408 ni wachache sana ni sawa na asilimia 0.000742 ya watanzania wote. Wakifika asilimia moja mnijulishe nianze Kuvaa barakoa.
Hizi data ZA kupikwa ila mwanzo mzuriWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amesema hadi kufikia Julai 8, 2021 jumla watu 408 walibainika kuwa na ugonjwa wa corona huku 284 wakitumia mitungi ya oksijeni.
Dk Gwajima ametoa taarifa hiyo leo Jumamosi Julai 10, 2021 wakati akitoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kwenye mnada wa Msalato jijini Dodoma.
Kwa upande wa Mkoa wa Dodoma, Waziri huyo amesema hadi kufikia Julai 8, 2012, jumla ya watu 26 waligundulika kuwa na ugonjwa huo huku 22 wakiwa katika mitungi ya oksijeni.
Wakati huo huo, Dk Gwajima na kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka wametembea umbali wa kilometa nne lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kuvaa barakoa ili kujikinga na maambukizi.
=====
Ni wakati sasa wa Wananchi na asasi na taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali kushirikiana na serikali katika kutekeleza na kuhamasisha maelekezo ya wataalamu wa afya juu ya hatua za kukabiliana na ugonjwa huu.
View attachment 1848604 View attachment 1848605
Duh! kwani mkuu unafikiri hata hao wanatajwa kufa kwa covid ni kwamba kweli wote vyanzo vya vifo vyao ni covid? wewe unaweza kufa na mipresha yako huko ila ukipimwa na kukutwa na virusi vya corona teyari kifo chako kinahesabika ni cha covid.Huyu mama ni muongo kuliko Prof. Muhongo. Hapa nilipo Kuna watu 9 wamefariki Leo Kwa COVID-19. Hospital zimejaa wagonjwa. Mbona hakutaja waliokufa? Hiyo idadi ni kutoka mkoa au wilaya gani Tanzania?
Hii ndio TZNdio nini sasa hiki ? hao 408 wamegundulika lini ? Na Wapi ? Katika kutambua ukubwa wa tatizo tunatakiwa tuambiwe eneo na kipindi cha muda walipogundulika vinginevyo tunaona ni janja janja tu !
Hivi kwanini lawama hapewi Rais mama samia katika hili kama ambavyo alivyokuwa anapewa lawama Magufuli? Rais mwenyewe kanyamaza kimya kwa maana haoni kinachofanywa na waziri wake ila sisi ndio tunamlaumu waziri na kumuacha Mama samia.Huyu mama ni PhD Kwa kusomea au ni Dr wa binadamu? Data alizo zitoa Leo ni maajabu ya data