Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa aingilia kati mgogoro wa ardhi wa Wananchi na Kampuni ya Tanzania Road Haulage

Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa aingilia kati mgogoro wa ardhi wa Wananchi na Kampuni ya Tanzania Road Haulage

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa ameingilia kati mgogoro wa ardhi wa muda mrefu kati ya Wananchi wapatao 246 na muwekezaji wa Kampuni ya Tanzania Road Haulage katika eneo la Kurasini wilayani Temeke jijini Dar Es Salaam ambapo wananchi hao wanadai kutolipwa malipo stahiki kulingana na uthamini wa maeneo yao wa mwaka 2008.

Waziri Silaa baada kupitia nyaraka hizo na kusikiliza pande zote zenye mgogoro amewataka wananchi hao wafike ofisi za ardhi za mkoa wa Dar es Salaam na kuhakiki uhalali wa malipo yao ili Serikali iweze kulitafutia ufumbuzi suala hilo.
 
Back
Top Bottom