Kitchener
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 13,833
- 27,753
Ni wiki sasa nimeweka kambi Dodoma kufuatilia hati za viwanja vyangu pale kwa maafisa ardhi jiji, urasimu ni mwingi, wanataka pesa, nikiwa DSM kuna mtu nilisema afuatilia baada ya mimi kufanya application mtandaoni manake siku hizi kuna e-ardhi kila kitu unaupload mtandani, lakini nikaambiwa wamemwambia mtandao haufanyi kazi. nikapanda SGR ni wiki sasa wale mabinti zenu wa ardhi pale chini wanasema mtandao unasumbua. Swali langu ni hili,
- Wewe Waziri wa ardhi, kwa nini mliamua kuanzisha e-ardhi kwa kuzuia makaratasi ya manual kama mlijua bado mfumo wenu wa computer haupo vizuri? sijui kama ni Dodoma tu au nchi nzima.
- Kwani ni shilingi ngapi mnaweza kulipia ili server zenu ziwe na uwezo kuhimili watu nchi nzima? ina maana wizara yenu haina pesa ndogo kama hiyo ili huduma kwa wananchi iwe njema?
- kwa nini tusiamini kama mnahujumu server za mtandao wenu makusudi li wananchi wakiwa foleni kubwa mpate nafasi ya kuwaomba rushwa ili mambo yao yaende haraka? kwanini mntatengeneza huo mwanya wa rushwa?
- Kuna tofauti gani sasa ya kuchelewa, kati ya mfumo wa manual na e-ardhi wa sasa?
- Pamoja na e-ardhi kuwepo, lakini bado watendaji wenu wanataka rushwa ili kukamiliza jambo ambalo umeupload, yaani utumie watu wa pale watafuta mtu ambaye jalada lako limefikia ili afanyie kazi kilichopo kwenye computer yake uendelee na hatua nyingine au la mwenzio aliyekuja nyuma yako atashughulikiwa na wewe utaambiwa mpo kwenye foleni wengi, whats the difference na rushwa za zamani?
- Kwenye mtandao wanaahidi kuwa ndani ya siku 14 hatua zote zitakuwa zimekamilika, meaning, watakuwa wamereview nyaraka ulizoupload, watapeleka kwa maboss wao kupitisha, watakuwa wamepeleka kwa kamishna wa Mkoa, na watakuwa wameshapeleka kwa msajili wa hati, hivyo ndani ya wiki 2 mtu anaweza kupata hati. mfumo huu kama sikosei alianzisha komredi Lukuvi akiamini atakuwa amepunguza urasimu na mtu atapata hati kwa haraka kuliko zamani. lakini, mbona imekuwa njia ngumu na yenye rushwa kuliko zamani?
- Tupate Waziri gani wa ardhi atakayefanikiwa kukomesha rushwa na urasimu kwenye sekta ya ardhi Jiji la Dodoma? kama Lukuvi alijitahidi, jerry slaa aliangukia pua, huyu naye ndejembi hana lolote labda kwa sababu na yeye ni mtu wa dodoma, mrudisheni Lukuvi basi kama mmeshindwa.