Waziri wa Elimu anasimamia asichokiamini? Mwanae anasoma English Medium

Waziri wa Elimu anasimamia asichokiamini? Mwanae anasoma English Medium

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Heshima sana wanajamvi,

Tanzania pengine ni nchi pekee duniani yenye maajabu yasiyoweza kulinganisha au kufananishwa na nchi nyingine.

Ni jambo la ajabu waziri wa elimu msimamizi wa elimu yenu na mustakabali wetu wa siku zijazo.Waziri wetu huyu watoto wake hawasomi katika shule za umma,wapo katika zile shule zetu "english medium" binafsi. Ikiwa Waziri hana imani na shule zetu za Kata au ukipenda St Kayumba na wakati huo huo yeye ni msimamizi na mwangalizi au ukipenda mlezi mkuu hapeleki watoto wake huko maana yake nini ?.

Mwl Nyerere watoto wake walisoma Tabora,Bunge,Tambaza. Waziri wake wa Elimu aliyajua matatizo yote ya elimu kwakuwa hata watoto wao walisoma shule hizo hizo.Watoto wake walikwenda JKT,walipigana vita vya Uganda hapakuwepo ubaguzi wa aina yoyote kama tunavyoona leo.

Ifike mahali uzalendo usisitizwe katika nyanja kama hizi,ukibahatika kupata nafasi ya kuongoza wizara ya Viwanda basi wewe kama Waziri lazima uonyeshe mfano wa kununua bidhaa za Tanzania mfano thamani za maofisini,nguo. Ukibahatika kuongoza Wizara ya Elimu lazima watoto wako wasome shule za kata wakutane na changamoto za ukosefu wa waalimu,vitabu madarasa,matundu ya choo na nk.Hii itasaidia Wizara kupanga mipango ambayo italenga kuondoa kero zote zinazozikumba shule za umma.

Ni aibu kwa jamii iliyostaharabika kuhubiri jambo ambalo kwa hakika wewe mwenyewe huliamini unalitilia shaka,unalionea aibu,hulipendi hauko tayari jamii yako ya karibu kwa maana ya watoto wako wasilishiriki.

Mama Ndalichako, Ummy ikiwa watoto wenu hawasomi shule za serekali wakati nyinyi ni wasimamizi wakuu wa elimu Tanzania basi hakuna nafasi nyingine zaidi ya kujiuzulu.
 
Wajukuu wa Nyerere niliobahatika kuwafahamu tulisoma nao shule zetu za umma...
Watoto wa Mwinyi walikuwa wanakula bakora za ndossi pale Muhimbili shule ya msingi....
Mwendazake mtt wake kazungusha Form four, wangu kazungusha form two wote wakisomaa shule za kata...

Mimi Bado nakubaliana na sehemu kubwa ya falsafa za mwendazake alikuwa anarejesha Uzalendo.... Hawa wengine siwaelewi wanachoongea nawasikiliza kwa sikio moja....
 
... alivyokubali kuandika "historia mpya" ya Tanzania anayoijua yeye na aliyemtuma nilimdharau mazima. Ingekuwa ni issue ya maana asingeruhusu mchakato ufutwe baadaye. Hii inaonesha ni mtu asiye na msimamo na asiyesimamia taaluma badala yake ni fuata upepo mradi madaraka yapo! Halafu utasikia wakipayuka majukwaani "vijana mkajiajiri" wakati wao wanalilia 70+.
 
Hiki ndicho alichokimaanisha mkuu wa mkoa wa dodoma.

Huyu ni mtoto wa waziri wa tamisemi anayesimamia elimu ngazi ya msingi na sekondari na hapa akiwa amevalia uniform ya international school. Inshort hata waziri hana imani na shule za serikali unafikiri ndio atakuwa na uchungu na mwanao anayesoma shule ya kata?

Screenshot_20210714-121107.png

I stand with Antony mtaka!
 
Heshima sana wanajamvi,

Tanzania pengine ni nchi pekee duniani yenye maajabu yasiyoweza kulinganisha au kufananishwa na nchi nyingine.

Ni jambo la ajabu waziri wa elimu msimamizi wa elimu yenu na mustakabali wetu wa siku zijazo.Waziri wetu huyu watoto wake hawasomi katika shule za umma,wapo katika zile shule zetu "english media" binafsi.Ikiwa Waziri hana imani na shule zetu za Kata au ukipenda St Kayumba na wakati huo huo yeye ni msimamizi na mwangalizi au ukipenda mlezi mkuu hapeleki watoto wake huko maana yake nini ?.

Mwl Nyerere watoto wake walisoma Tabora,Bunge,Tambaza. Waziri wake wa Elimu aliyajua matatizo yote ya elimu kwakuwa hata watoto wao walisoma shule hizo hizo.Watoto wake walikwenda JKT,walipigana vita vya Uganda hapakuwepo ubaguzi wa aina yoyote kama tunavyoona leo.

Ifike mahali uzalendo usisitizwe katika nyanja kama hizi,ukibahatika kupata nafasi ya kuongoza wizara ya Viwanda basi wewe kama Waziri lazima uonyeshe mfano wa kununua bidhaa za Tanzania mfano thamani za maofisini,nguo. Ukibahatika kuongoza Wizara ya Elimu lazima watoto wako wasome shule za kata wakutane na changamoto za ukosefu wa waalimu,vitabu madarasa,matundu ya choo na nk.Hii itasaidia Wizara kupanga mipango ambayo italenga kuondoa kero zote zinazozikumba shule za umma.

Ni aibu kwa jamii iliyostaharabika kuhubiri jambo ambalo kwa hakika wewe mwenyewe huliamini unalitilia shaka,unalionea aibu,hulipendi hauko tayari jamii yako ya karibu kwa maana ya watoto wako wasilishiriki.

Mama Ndalichako,Ummy ikiwa watoto wenu hawasomi shule za serekali wakati nyinyi ni wasimamizi wakuu wa elimu Tanzania basi hakuna nafasi nyingine zaidi ya kujiuzulu.
Sifa pekee ya kiongozi ni kuonyesha njia,Kama waziri hana imani na shule ambazo yeye ni msimamizi hivi ofisini anafanya nini,lazima awajibike.
 
Hiki ndicho alichokimaanisha mkuu wa mkoa wa dodoma.

Huyu ni mtoto wa waziri wa tamisemi anayesimamia elimu ngazi ya msingi na sekondari na hapa akiwa amevalia uniform ya international school. Inshort hata waziri hana imani na shule za serikali unafikiri ndio atakuwa na uchungu na mwanao anayesoma shule ya kata?

View attachment 1852747

I stand with Antony mtaka!
wanachotaka wadogo zetu wawe ma-barmade, security guard, walimu, mgambo, bodaboda, konda, madereva, police, watendaji wa mitaa. Kifupi hawa jamaa hawana nia njema na masikini.
 
Back
Top Bottom