Waziri wa Elimu anasimamia asichokiamini? Mwanae anasoma English Medium

Waziri wa Elimu anasimamia asichokiamini? Mwanae anasoma English Medium

Hiki ndicho alichokimaanisha mkuu wa mkoa wa dodoma.

Huyu ni mtoto wa waziri wa tamisemi anayesimamia elimu ngazi ya msingi na sekondari na hapa akiwa amevalia uniform ya international school. Inshort hata waziri hana imani na shule za serikali unafikiri ndio atakuwa na uchungu na mwanao anayesoma shule ya kata?


View attachment 1852747

I stand with Antony mtaka!
Duuuuuuuuuuuu,watoto wa aina hiyo wapo wengi.mtaka yupo sahihi Sana.
 
CCc
Hiki ndicho alichokimaanisha mkuu wa mkoa wa dodoma.

Huyu ni mtoto wa waziri wa tamisemi anayesimamia elimu ngazi ya msingi na sekondari na hapa akiwa amevalia uniform ya international school. Inshort hata waziri hana imani na shule za serikali unafikiri ndio atakuwa na uchungu na mwanao anayesoma shule ya kata?


View attachment 1852747

I stand with Antony mtaka!
CCM oyeee, wanatupa mfumo mbovu wa elimu, watoto wao wanasoma nje ili waje kututawala
 
Heshima sana wanajamvi,

Tanzania pengine ni nchi pekee duniani yenye maajabu yasiyoweza kulinganisha au kufananishwa na nchi nyingine.

Ni jambo la ajabu waziri wa elimu msimamizi wa elimu yenu na mustakabali wetu wa siku zijazo.Waziri wetu huyu watoto wake hawasomi katika shule za umma,wapo katika zile shule zetu "english medium" binafsi. Ikiwa Waziri hana imani na shule zetu za Kata au ukipenda St Kayumba na wakati huo huo yeye ni msimamizi na mwangalizi au ukipenda mlezi mkuu hapeleki watoto wake huko maana yake nini ?.

Mwl Nyerere watoto wake walisoma Tabora,Bunge,Tambaza. Waziri wake wa Elimu aliyajua matatizo yote ya elimu kwakuwa hata watoto wao walisoma shule hizo hizo.Watoto wake walikwenda JKT,walipigana vita vya Uganda hapakuwepo ubaguzi wa aina yoyote kama tunavyoona leo.

Ifike mahali uzalendo usisitizwe katika nyanja kama hizi,ukibahatika kupata nafasi ya kuongoza wizara ya Viwanda basi wewe kama Waziri lazima uonyeshe mfano wa kununua bidhaa za Tanzania mfano thamani za maofisini,nguo. Ukibahatika kuongoza Wizara ya Elimu lazima watoto wako wasome shule za kata wakutane na changamoto za ukosefu wa waalimu,vitabu madarasa,matundu ya choo na nk.Hii itasaidia Wizara kupanga mipango ambayo italenga kuondoa kero zote zinazozikumba shule za umma.

Ni aibu kwa jamii iliyostaharabika kuhubiri jambo ambalo kwa hakika wewe mwenyewe huliamini unalitilia shaka,unalionea aibu,hulipendi hauko tayari jamii yako ya karibu kwa maana ya watoto wako wasilishiriki.

Mama Ndalichako, Ummy ikiwa watoto wenu hawasomi shule za serekali wakati nyinyi ni wasimamizi wakuu wa elimu Tanzania basi hakuna nafasi nyingine zaidi ya kujiuzulu.
Mbuzi anakula kwa urefu wa kwamba yake.
 
Kwani Antony yeye anasemaje? Yeye watoto wake wako wapi? Je wako shule zetu? Au naye mchana anamchana waziri then usiku anaishi maisha ya Waziri? Pamoja na kwamba Mtaka anaweza akawa hana legitimacy kwneye hili lakini hoja yake ina mashiko. Tumechoka na viongozi wanaoimba wasichoamini wala kutenda.
Nadhani iwe kikatiba viongozi watoto wao wasome shule za umma pamoja na kutibiwa nchini.
 
Back
Top Bottom