Waziri wa Elimu anasimamia asichokiamini? Mwanae anasoma English Medium

Arusha School ilikuwa ikitumia lugha ya kiingereza tangu miaka ya 1970s nashindwa kuelewa Serekali ilishindwa nini kuongeza idadi ya shule wakati waalimu wapo.

Nafikiri kuwepo mkakati maalumu wa kuongeza idadi ya shule za Serekali zinazotumia lugha ya kiingereza.

Mfano Serekali inaweza kuja na mkakati wa kuzibadili shule tano kila mwaka katika majiji yote Tanganyika.Niomeona kuanza na majiji ni rahisi kwasababu idadi ya waalimu wenye sifa ni rahisi kupatikana na nafasi ya kushirikisha wazazi kwa maana ya kuchangia gharama ni rahisi pia.
 
Kwa sababu ww ni public servant lazima watoto wako wasome shule za kata?this is such a dumb take....haya mawazo ni ya kidikteta.

Unaweza kutoa maoni yako bila matusi wala kejeli.

Waziri wa Elimu na Tamiseni ni wasimamizi Wakuu wa sera ya Elimu.Ikiwa suala la lugha ambayo inatumika katika Elimu ya msingi Wakati huo huo hawataki kuonyesha mfano wanakimbiza watoto wao shule binafsi !.
 
Bado hamjashtuka tu kuwa wanasiasa wanatamani sana wananchi waendelee kuwa maskini ili wawatawale na watoto wao wakimaliza Hizo international school watawale watoto wenu waliosoma st. Kayumba na kufeli.
 
sina tatizo kuwapeleka watoto wao hizo shule kwa pesa zao maana watanzania wengi wanaweza hiyo ada bila wizi, tatizo ni wale wanaokwenda London kutibiwa huku tukijua 100% huo uwezo hawana
 
Shida ni kwamba watanzania wengi hatujiamini maana hata walimu japo anafundisha ila hawezi kumfundisha mtoto kwenye shule hiyo ya kata anayofundisha,hivyo hivyo kwa mawaziri unakuta waziri wa afya anaenda tibiwa nje na yeye anasimamia hospital hapa bongo,hakuna uzalendo haya madaraja yatatugawa watu tunafanyia kazi mshahara na hakuna uzalendo
 
rudisheni kiingereza mashuleni kama the medium of instruction. kila mttanzania anpenda kuongea kiingereza sasa kama serikali hairudishi kiingereza mashuleni basi kila ajiwezaye atapeleka mwanae english medium. msiwalaumu waheshimiwa Joyce ndalichako na Ummy mwalimu kwa kupeleka watoto endlish medium.
 
Naona una hallucination kijana. Unamtafutia visa tu waziri. Kwani amefanya kosa gani kupeleka watoto wake katika shule anayotaka kama uwezo upo. Achana na haya mawazo ya kijima dogo.
hayo sio ya kijima, nchi zilizostaarabika hufanya hivyo
 
Is she doing her job accordingly ?
 
Watoto wao wangesoma kata na kupanda daladala elimu Ingekuwa bora nchini.Maana Katu huwezi endesha gari ukiwa nje.
wakati ule tunasoma na kina makongoro kwenda shule za private ilikuwa ni aibu na ndio maana hata chakula cha ukweli kilipatikana shuleni,
 
WATOTO WA MKUU WA MKOA WA DODOMA NDUGU ANTONY MTAKA WANASOMA SHULE GANI? NAOMBA JIBU TAFADHALI KAMA WAPO KWENYE HAYO MAKAMBI YA KUPEANA UJAUZITO
 
Si mmeona hata mtoto wa PM mstaafu Pinda kashaingia 18 za utawala.....muwe wapole tu.
 
Hapa una maana ya English Medium School au International School? Sina hakika kama International Schools wanavaa uniforms, wanaovaa uniforms ni English Medium Schools. Watu wengi wamekua hawaelewi tofauti ya International Schools na English Medium Schools.

International School ni kama, International School of Tanganyika, International School of Moshi etc.
 
Watch mwigulu wall tegeta Feza
55 ft
 
Siku zote huwa najiuliza hivi kiswahili ni lugha ya taifa? Na kama ni lugha ya taifa kwa nini shule za maskini wanasoma masomo kwa kiswahili na shule za matajiri wasome kwa kiingereza? Ina maana watoto wa matajiri ndiyo wanaoandaliwa kwenda secondary? Maana masomo yote huko ni kwa kiingereza! Hapa lengo ni nini hasa?
Hapa inabidi tuseme ukweli kwamba kiswahili ni lugha ya taifa la maskini wa Tanzania na kiingereza ni lugha ya matajiri wa Tanzania.
Kuhusu uzalendo ilifaa tunapochagua viongozi tuchague watu tunaofanana nao. Tuangalie kama watoto wao wanasoma shule hizi hizi tunazopeleka watoto zetu. Anaposema tumeboresha huduma za afya je wanatibiwa kwenye hospitali zetu? Wake zao wanaenda kwenye klinik zetu? Inaumiza sana.
 
Hapana jamani, huwezi kumpeleka mtoto hizo shule za Kata na Serikali; yaani kama kweli una uwezo na unampenda mwanao. Hapana! Elimu bure ni elimu hovyo, hakuna cha thamani kisicho na gharama.

Mawaziri na Wabunge wangeboresha hizo shule, kama zilivyo hospitali na zahanati, ungeona wakipeleka watoto wao huko. Tusiwaadhibu watoto wote kisiasa. Na hata kumpeleka mtoto wako Shule hizo pia sio kipimo wala kigezo cha uzalendo - I cant's see how.

In fact, Mh Ndalichako alikosea kutoa tamko, na Mh Mtaka naye alikosea kuongea alivyoongea - ukweli usemwe.
Na kama Wakuu wa mikoa na Wilaya kadhaa wakiendeleza hiyo tabia ya Mtaka then soon we will find our redemption, indirectly.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…