Waziri wa elimu lingalie hili la walimu hasa wa Primary kutoza pesa kila siku eti ni mitihani

Waziri wa elimu lingalie hili la walimu hasa wa Primary kutoza pesa kila siku eti ni mitihani

Hivi hiyo pesa unayolalamika ya mtoto wako ya mtihani ata kama anafanya kila siku unajua adha ya kufundisha wewe?
 
Uko sahihi. Kuna shule inaitwa Sinon Primary ma Secondary inamichango ya kutosha. Mtihani kila wiki sh 2000 kwa nini? Nilipiga hesabu kidogo tu ya wanafunzi 800 mara 2000 mara 4 kwa maana ya mwezi mmoja. Wanakula hela balaa
Hata kuandaa hiyo mitihani na kusahihisha ni gharama pia.

Kuhusu kula pesa hakuna kosa hapo hakuna cha bure kwenye maisha, kuinua taaluma ya mwanao kunahitaji kuingia gharama.
 
Fika shuleni uulize naamini utapewa ufafanuzi mzuri utaelewa vizuri kwanini michango kwa wanafunzi ya kila siku.
 
Upo nchi Gani wewe?
Mbona nchi ya Tanzania elimu ni buree kabisa
 
Kwa swala hili acha niwe upande wa walimu kiukweli. Ukifatilia kwa ukaribu utakuta awa wanaotoza hizi pesa ni wale walimu wa kujitolea wasiokuwa na posho wala mshahara ule wa serikali, swali wataishi vipi bila mitihani hii?

Hata hivyo hii mitihani kiukweli inasaidia kumfanya mtoto kuwa active na kukutana na maswali mengi tofauti ambayo yatamsaidia katika mitihani yake ya mwisho.

NB: Unamsomesha mwanao kayumba na bado unakuwa mvivu wa kutoa hela ndogo ndogo za kufanya mwanao asaidike huko kayumba.....akifeli unalalamikia elimu mbovu.
 
Education is expensive, no free lunch in a capitalist world.
We are not a capitalist country, take note of this....... let CCM not deceive people that primary education is free, tell the truth so that people can fight for their education survival
 
We are not a capitalist country, take note of this....... let CCM not deceive people that primary education is free, tell the truth so that people can fight for their education survival
Free is expensive too......
 
Mnalipishwa shilingi ngapi Kwa ajili ya hiyo mitihani?
 
Shule za binafsi watu wanalipa ada mamilioni na bado Kuna michango ya maelfu na malaki kwa ajili ya shughuli za kitaaluma na extracurriculars.
 
Ada imetolewa ili wazazi wasifuatilie maendeleo ya watoto wao na hata wakifutilia wasilalamike serikali inaposhindwa kuajiri walimu, kujenga madarasa, kununua vitabu n.k watoto wa viongozi wakiwa shule binafsi wakipewa elimu bora washike nafasi za wazazi wao wewe wa kwako umfundishe kubeti au umuozeshe
 
Serikali ingerudisha tu ada .Kwa sababu huko shuleni kumekuwa na michango mingi ambayo si rahisi hata kutrace mapato na matumizi yake.Wazazi wamekua wakiitwa shuleni kila wakati na kuambiwa wachangie hiki au kile na kwenye vikao hivyo hakuna mzazi ambaye anaweza kupinga kwa sababu ukipinga mtoto wako anayesoma hapo ataandamwa sana na walimu.
Usilolijua ni sawa na usiku wa kiza.
 
Acha upuuzi. Magufuli hajawahi kuwa killer na wala hatokuwa.
1. Mpuuzi ni aliyekuzaa
2.
 
Back
Top Bottom