Waziri wa Elimu na TAMISEMI, ni sawa Wanafunzi Shule za Serikali kuambiwa waende na dissecting kit na vitabu vya tahasusi?

Waziri wa Elimu na TAMISEMI, ni sawa Wanafunzi Shule za Serikali kuambiwa waende na dissecting kit na vitabu vya tahasusi?

• Zamani za kale, miaka ya arobaini na kitu, na miaka ya tisini na kitu
Serikali iliweza kuwapa huduma zote za kijamii wananchi wanazotaka bure, watu walikuuwa wachache na serikali zilimudu.
View attachment 1829880

'Serikali itahakikisha itatoa huduma za hakika na bure' kwa zama hizi kauli hii haitekelezeki. Abiria chunga mzigo wako. Isitoshe vifaa husika ni vya mwanafunzi mwenyewe.
Kuna baadhi ya shule zimeelemewa, wanafunzi ni wengi kuliko rasilimali zilizopo. Nimesoma shule za kata; huenda Tabora boys na Kibaha hilo tatizo hakuna, ila mnunnulie kam huwezi mwache akapambane. Fikiria shule labda ina , ina Biology takers 180 alafu BS ziko 50 au 25! Acheni utani nyie, wenye pesa hawapelekagi watoto wao shule hizi zetu; wakiwapeleka hutimiza kisemwacho kwenye 'join instruction'

Anything cheap is expensive
What do you mean saying "..anything cheap is expensive...?" Who wants cheap things, cheap education...? You or me..?

Ukipenda, unaweza kurudia kusoma tena andiko langu kuu hapo juu na utaelewa nini mantiki ya hoja yangu...

Sijaogopa kununua kitabu kwa ajili ya mtoto wangu. Lakini pia unadhani kila mzazi anaweza kununua vitabu..? When we are discussing this topic we have to think about other poor people who can't even afford a lunch and dinner and they have children who must go to school...

Hoja yangu ya kujadili ni;

Hivi ni kwanini shule ya serikali isiwe na vitabu? Sababu ni mini hasa...?
 
Huenda kwa upande wako uko sawa, ila kwa upande wangu vitabu mimi nitamnunulia mtoto wangu bila hata kuuliza, utanisamehe tu kwa kweli mkuu.
Sawa kabisa. Mimi nitafanya hivyo pia...

Lakini ninachotaka tujadili hapa ni "SHULE ZA SERIKALI NA MAPUNGUFU YAKE". Je, ni sawa na ni kwanini..?

Hii ndiyo mantiki ya hoja yangu lakini hawaelewi wanadhani Mimi naogopa kununua kitabu kwa ajili ya mtoto wangu...

Ishu ni kuwa,serikali yetu haina uwezo kui - equip shule zake na vifaa vya kujifunzia na kufundishia vitabu vikiwemo? Na kwani, ni nini hasa maana " formal" ya "shule"..?
 
Tena shukuru sasa Hiv mnaandikiwa sis ilikuwa unaripot ndo Unajua kumbe kuna dissection kit, kumbe kuna chandi, kumbe kuna scientific calculator, kumbe kuna vitin pamflect
Explain pls...

Una maana gani kusema hivi? Umeelewa hoja yangu kweli...?
 
Kwa hiyo hata darasani inakuwa hivyo sio? Kwa hiyo ndiyo Tanzanianayotujemgea. Tammbua Tanzania sio ya mtu mmoja. Mimi Kama mzazi nipe ufafanuzi.
Ufafanuzi gani unataka? Be specific pls. Niko kwa ajili yako...
 
Sawa kabisa. Mimi nitafanya hivyo...

Lakini ninachotaka tujadili hapa ni "SHULE ZA SERIKALI NA MAPUNGUFU YAKE". Je, ni sawa na ni kwanini..?

Hii ndiyo mantiki ya hoja yangu lakini hawaelewi wanadhani Mimi naogopa kununua kitabu kwa ajili ya mtoto wangu...

Ishu ni kuwa,serikali yetu haina uwezo kui - equip shule zake na vifaa vya kujifunzia na kufundishia vitabu vikiwemo? Na kwani, ni nini hasa maana " formal" ya "shule"..?
Wewe pamoja na wazazi wanaojitambua hamna shida mtanunua mabox ya vitabu hata mkitaka kujenga darasani kwa ajili ya watoto wenu. Tatizo ni wazazi ambao wameshasikia elimu bure, hataki kusikia ufagio au kitabu Cha elfu 80 mfano maxmillia kinauzwa Bei g and?

Sikulaumu Ila machozi ya Hawa watoto wanaotaka kutimiza ndoto zao na hazitimii ndizo zitakutesa. Kwa ajili ya ulafi.
 
Serikali ya CCM ni wanafiki na wazandiki wanasema elimu bure ni uwongo huku wazazi wakiamini,huko mashuleni hakuna vitabu kuanzia shule za msingi hadi sekondari unashangaa wazazi yaani maccm yanaamini sijui hawa watanzania wamelogwa au vipi!
Lini walikwambia form six bure?
 
No! No! No kauli mbiu elimu bure!!!!. Tukubaliane ni kauli ya kitapeli. Rudini kwa wazazi muwaelishe. Mzazi mshari hapa mtoto atashindwa kutimiza ndoto zake. Ndiyo maana watoto wanajiingiza kwenye Mambo ya kishetani kwa ajili ya kauli hizi.

Hujui watoto wa wenzako wanapata ushawishi wa ajabu kwa ajili hiyo. We tuliza ushetani.

Mpaka ufagio ? Kumbe safari ya utumwa bado ipo.
Elimu bure Advance nani alisema?
Kuna cost sharing hata hiyo 70 unayolipa haitoshi ndio maana unaambiwa upeleke mpaka mafagio
 
1. Mwanangu amechaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita (F. V & VI) mwaka huu 2021 Shule ya Sekondari Nyantakara katika tahususi (Combination) ya Chemistry, Biology & Geography (CBG) iliyoko wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera. Hii ni shule ya serikali ya Tanzania....

2. Licha ya orodha ya mahitaji mengi anayotakiwa aende nayo mfano; fagio wa kufagilia ndani, sabuni ya maji ya chooni, fagio wa kufagilia nje, ream ya kataratasi nk nk, lipo hili ambalo mimi limeniacha hoi hata kujiuliuza kulikoni hizi shule za serikali? Nimeambiwa nimnunulie mwanangu

[A.] Vitabu yote vya tahasusi (subject combinations) anayokwenda kusoma yaani CBG & Basic Applied Maths

[B.] Dissecting Kit ya somo la Bailojia

3. Nikajiuliza ina maana shule hii anayokwenda kusoma mwanangu haina vitabu? Imekuwaje inaanza kidato cha tano huku ikiwa haina vitabu? Kipi kilipaswa kuanza, majengo au vitabu na walimu kwanza? Hivi mzazi kama nanunua vitabu vyangu kwa ajili ya mwanangu, si bora asomee nyumbani sasa na siku ya mtihani aende kufanya tu...?

4. Nimelileta humu tujadiliane ili tujue majigambo ya serikali kuwa imeboresha elimu Tanzania, yana maana gani kama hali iko hivi ktk shule zake...?

4. Naambatanisha na Joining instructions ya shule kwa ajili ya ushahidi na reference zaidi kwa atakayetaka kuthibitisha maelezo yangu....

5. Honestly, baada ya kuipata hii fomu ya maelekezo, nimeanza kusaka fedha tu na kufikiri kumpeleka shule ya binafsi...
View attachment 1829765View attachment 1829766View attachment 1829769
Mzazii shule nyingi hazina vitabu narudia tena hazina vitabu na vikiwepo nivile vya TIE(Tanzania Institute of Education) ambavyo viko shallow mnoo
 
Labda cha kukushauri, vitabu muhimu sana hata kama havijaandikwa kwenye joining instructions isipokuwa kama huna hela angalia kwanza mahitaji ya umuhimu kisha vitu vingine vitafuata kidogokidogo

#A level inabidi uache ubahiri, hapo bado kuna tuition likizo zina gharama, pamphlets zinahitajika na ikiwezekana pesa ya matumizi ya kutosha maana Kula maharage -ugali siku zote za wiki haijakaa vizur

Shule hazina hela, kuna shule inabidi ziingiziwe mil 38 kwa mwez ila inaingia mil chini ya 25 so zina madeni hatar
 
Hujui uandikacho wewe. Ni wazi umezaliwa juzi, umekuta matatizo haya na unadhani ndivyo ilivyo....

Mimi nimesoma O' Level, Shule ya Sekondari Kibaha [boarding]....

Nikasoma A'Level Tabora Boys' Sec. School [boarding]....

Hizi zote ni shule za serikali. Kote huko sikuwahi kuagizwa kwenda na kitabu chochote. Kila kitu tulikikuta hapo hapo shuleni...

Na zipo shule za kata [A'Level Sec. Schools] haziagizi mpaka vitabu kwa sbb shule haiwezi kuitwa shule isipokuwa ina mambo matatu muhimu na ya msingi...

[A.] Majengo (madarasa)

[B.] Walimu

[C.]. Vifaa vya kufundishia na kujifunzia

Sasa jibu swali hili; Kwanini hii shule ya serikali iitwe shule wakati haina vifaa vya kujifunzia na kufundishia i.e vitabu, vifaa vya maabara, chaki nk nk...???
[emoji23][emoji23]Kumbe mzazi na yeye alipita shule tena special school[emoji23] acheni kumlaumu sasa
 
Hujui uandikacho wewe. Ni wazi umezaliwa juzi, umekuta matatizo haya na unadhani ndivyo ilivyo....

Mimi nimesoma O' Level, Shule ya Sekondari Kibaha [boarding]....

Nikasoma A'Level Tabora Boys' Sec. School [boarding]....

Hizi zote ni shule za serikali. Kote huko sikuwahi kuagizwa kwenda na kitabu chochote. Kila kitu tulikikuta hapo hapo shuleni...

Na zipo shule za kata [A'Level Sec. Schools] haziagizi mpaka vitabu kwa sbb shule haiwezi kuitwa shule isipokuwa ina mambo matatu muhimu na ya msingi...

[A.] Majengo (madarasa)

[B.] Walimu

[C.]. Vifaa vya kufundishia na kujifunzia

Sasa jibu swali hili; Kwanini hii shule ya serikali iitwe shule wakati haina vifaa vya kujifunzia na kufundishia i.e vitabu, vifaa vya maabara, chaki nk nk...???

..serikali imenunua ndege kwa fedha taslim.

..subiri kwanza wamalize kununua ndege then kutakuwa na fedha za kuhudumia mashule.

..au tutakapopata mkopo toka World Bank kugharamia elimu.

..kwani wewe hutaki nchi yetu iwe na ndege?

..hivi hujisikii fahari Tz kuwa na shirika la ndege?
 
Wewe nashindwa hata kukujibu kwa sababu ni wazi hujelewa mantiki ya andiko langu lote. Na hiki unachosema "Elimu ni gharama" na kuwa kama sitaki gharama, nijaribu UJINGA, it's completely irrelevant na mantiki ya hoja yangu...

Anyway, ngoja nikupe tip kidogo kufungua ufahamu wako...

Mada yangu kimantiki inahusu "SHULE ZA SERIKALI" na mapungufu yake...

Wewe umejibu kitu kilicho "out of context" na ni kana kwamba unahalalisha upungufu huu na kuona ni sawa tu...

For your information, mwenzio nimesoma shule bora sana zenye kila kitu. Watoto wangu wanasoma shule bora za mashirika ya dini zenye kila kitu kwa sababu huo usemi "IF YOU THINK EDUCATION IS EXPENSIVE, TRY IGNORANCE" naufahamu maana yake pengine kuliko wewe unavyoelewa...

Seriously, ninaye mtoto mmoja. Amefaulu vizuri O'Level na kapata nafasi shule za serikali. Niliona nipunguze gharama kidogo asome shule hizi hizi za serikali...

Nilipotumiwa Joining Instructions, nilichokisoma kikanishangaza na nikaona napeleka mtoto Jehanamu tu. Hiki ndicho kilichonifanya nishee nanyi humu ili tujadili...

Sasa watu badala ya kujadili hoja, wengi ufahamu wao mdogo sana kumbe wa kuelewa mambo badala ya mnajadili mtu....

Nakubali kuwa serikali haiwezi kukamilisha kila kitu kwenye shule zake. Lakini mambo ya msingi kama vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa ajili ya ujifunzi wa watoto wetu ni lazima iyape priority....

Naomba tujadili hilo tukihusianisha na jukumu kuu la serikali ktk kutoa huduma kwa wananchi. Achana na hiki ulichokiandika hapa maana hakuna mwananchi ambaye halipi kodi ili kuboresha shule zetu...
Hadi nakuhurumia unavyojitahidi kuwaelewesha hawa viumbe[emoji23] tulia tu kunywa maji ulale it's too complicated! Bongo wajinga wengi mno.
 
Hujui uandikacho wewe. Ni wazi umezaliwa juzi, umekuta matatizo haya na unadhani ndivyo ilivyo....

Mimi nimesoma O' Level, Shule ya Sekondari Kibaha [boarding]....

Nikasoma A'Level Tabora Boys' Sec. School [boarding]....

Hizi zote ni shule za serikali. Kote huko sikuwahi kuagizwa kwenda na kitabu chochote. Kila kitu tulikikuta hapo hapo shuleni...

Na zipo shule za kata [A'Level Sec. Schools] haziagizi mpaka vitabu kwa sbb shule haiwezi kuitwa shule isipokuwa ina mambo matatu muhimu na ya msingi...

[A.] Majengo (madarasa)

[B.] Walimu

[C.]. Vifaa vya kufundishia na kujifunzia

Sasa jibu swali hili; Kwanini hii shule ya serikali iitwe shule wakati haina vifaa vya kujifunzia na kufundishia i.e vitabu, vifaa vya maabara, chaki nk nk...???
Mpeleke Tabora boys
 
Back
Top Bottom