Waziri wa Elimu na TAMISEMI, ni sawa Wanafunzi Shule za Serikali kuambiwa waende na dissecting kit na vitabu vya tahasusi?

Ni kawaida tu hilo, unanunua vitabu na makorokoro yote, hujasema mashuka na magodoro, tranka, track suit, soksi, mashati, suruali, madaftarii quire 3 ama 4, kalamu, sabunj za kuogea na kufulia, pocket money, remedial, ada, na mengineyo.
Hakuna bure hapo.
 
Hawa ni wazazi ambao hata kuwapelekea watoto chakula shuleni hilikuwa ni shida sasa anafikiri na A level ni hivyo hivyo. Badilika mzazi timiza mahitaji yote uliyoambiwa.
 
Michango 113,000/= !!!!!!!

Bado mifagio[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Kayumba raha sana!!!
 
If you think education is expensive then try ignorance.
Naomba tumtafsirie mdau huu msemo
 
Pole ndugu. Kwa waliozoea kusomesha watoto hawatashangaa hayo unayoyalalamikia ila watakushangaa wewe mwenyewe.
Nafahamu ni kutokana na wewe ama kutokuwa na elimu ya kutosha yaani wewe ni mbumbumbu ama huna exposure.

Ukiona huko shoda mpeleke private ila najua ni mbwembwe tu maana huna hela wewe ndio maana unapiga mihayo humu.

Elimu ni pesa usipende mtelemko we mpiga kura
1. Mwanangu amechaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita (F. V & VI) mwaka huu 2021 Shule ya Sekondari Nyantakara katika tahususi (Combination) ya Chemistry, Biology & Geography (CBG) iliyoko wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera. Hii ni shule ya serikali ya Tanzania.

2. Licha ya orodha ya mahitaji mengi anayotakiwa aende nayo mfano; fagio wa kufagilia ndani, sabuni ya maji ya chooni, fagio wa kufagilia nje, ream ya kataratasi nk nk, lipo hili ambalo mimi limeniacha hoi hata kujiuliuza kulikoni hizi shule za serikali? Nimeambiwa nimnunulie mwanangu

[A.] Vitabu yote vya tahasusi (subject combinations) anayokwenda kusoma yaani CBG & Basic Applied Maths

[B.] Dissecting Kit ya somo la Bailojia

3. Nikajiuliza ina maana shule hii anayokwenda kusoma mwanangu haina vitabu? Imekuwaje inaanza kidato cha tano huku ikiwa haina vitabu? Kipi kilipaswa kuanza, majengo au vitabu na walimu kwanza? Hivi mzazi kama nanunua vitabu vyangu kwa ajili ya mwanangu, si bora asomee nyumbani sasa na siku ya mtihani aende kufanya tu?

4. Nimelileta humu tujadiliane ili tujue majigambo ya serikali kuwa imeboresha elimu Tanzania, yana maana gani kama hali iko hivi ktk shule zake?

4. Naambatanisha na Joining instructions ya shule kwa ajili ya ushahidi na reference zaidi kwa atakayetaka kuthibitisha maelezo yangu.

5. Honestly, baada ya kuipata hii fomu ya maelekezo, nimeanza kusaka fedha tu na kufikiri kumpeleka shule ya binafsi.
View attachment 1829765View attachment 1829766View attachment 1829769
 
Hata uniform kwa nini kila mtu asivae la kwake.

Umeshawahi jiuliza kwa nn majeshini hata mashuka , neti zina fanana?

Msiwe wapinzani wa kila kitu. Mbona watoto wakienda jkt vifaa mnanunua wenyewe tena mnapangiwanmpaka rangi?

Kama hujawahi pitia maisha ya shule ni ngumu kusomesha maana unaona pesa ni nyingi
Kuna vitu ukiambiwa kununua vinaleta mantiki na vingine havileti. Tatizo la shule za Tanzania wanajaribu ku-complicate mambo bila sababu. Kwa mfano hili la shuka. Kwani ni lazima yawe na rangi moja? Vitu kama vitabu inaweza kueleweka lakini vitu kama dawa ya chooni, mafyekeo etc ni vitu vinatakiwa kutolewa na shule.
 
Jeshi siyo shule. BTW mimi nimpinga complication zisizo na lazima. Sipingi kununua vifaa. Karne ya leo unawaambia watoto wabebe majembe na makorokoro kibao yaliyopitwa na wakati kwenye dunia ya leo!
 
1. Mwanangu amechaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita (F. V & VI) mwaka huu 2021 Shule ya Sekondari Nyantakara katika tahususi (Combination) ya Chemistry, Biology & Geography (CBG) iliyoko wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera. Hii ni shule ya serikali ya Tanzania.

2. Licha ya orodha ya mahitaji mengi anayotakiwa aende nayo mfano; fagio wa kufagilia ndani, sabuni ya maji ya chooni, fagio wa kufagilia nje, ream ya kataratasi nk nk, lipo hili ambalo mimi limeniacha hoi hata kujiuliuza kulikoni hizi shule za serikali? Nimeambiwa nimnunulie mwanangu

[A.] Vitabu yote vya tahasusi (subject combinations) anayokwenda kusoma yaani CBG & Basic Applied Maths

[B.] Dissecting Kit ya somo la Bailojia

3. Nikajiuliza ina maana shule hii anayokwenda kusoma mwanangu haina vitabu? Imekuwaje inaanza kidato cha tano huku ikiwa haina vitabu? Kipi kilipaswa kuanza, majengo au vitabu na walimu kwanza? Hivi mzazi kama nanunua vitabu vyangu kwa ajili ya mwanangu, si bora asomee nyumbani sasa na siku ya mtihani aende kufanya tu?

4. Nimelileta humu tujadiliane ili tujue majigambo ya serikali kuwa imeboresha elimu Tanzania, yana maana gani kama hali iko hivi ktk shule zake?

4. Naambatanisha na Joining instructions ya shule kwa ajili ya ushahidi na reference zaidi kwa atakayetaka kuthibitisha maelezo yangu.

5. Honestly, baada ya kuipata hii fomu ya maelekezo, nimeanza kusaka fedha tu na kufikiri kumpeleka shule ya binafsi.
View attachment 1829765View attachment 1829766View attachment 1829769
Hizi high school za kata zimeanzishwa kisiasa.Nina wasiwasi hata mitihani ya kumaliza form six inasahihishwa kisiasa vile vile.
 
hiyo kit unayoizungumzia ni kawaida kwa wanafunzi wa biology kujinunulia, labda huko burundi ulikosoma ww wanafunzi wanavikuta shuleni
 
Kuna vitu ukiambiwa kununua vinaleta mantiki na vingine havileti. Tatizo la shule za Tanzania wanajaribu ku-complicate mambo bila sababu. Kwa mfano hili la shuka. Kwani ni lazima yawe na rangi moja? Vitu kama vitabu inaweza kueleweka lakini vitu kama dawa ya chooni, mafyekeo etc ni vitu vinatakiwa kutolewa na shule.
Ashira Girls wanafunzi wa EGM wameambiwa wapeleke MUNDU au kwa jina lingine Shami
 
Vitabu lazima anunue hata Sisi tuliosoma zamani tulikuepo tunanunua tuu. Dissecting kit ni vizuri Kwa maana hiyo itakuepo ni Mali yake. Understanding biology, understanding chemistry
Ulisoma "zamani" ya lini ndugu ambayo ulikuwa unaagizwa uende na sabuni ya chooni lita 5, ufagio wa kufagilia ofisini kwa Headmaster/mistress nk nk?

Kama mtanzania analipa mpaka kodi ya simkadi ya simu, tozo ya kutuma na kupokea mobile money, kodi ya LUKU na zingine nk nk...

Hii fedha inakuwa inakwenda wapi kama serikali inashindwa kupeleka fedha za kuhudumia shule zake...?

Mbona mnajisemea tu bila hata kufikiria kabla ya kusema...?

Nimeleta mada hii ili kutoa changamoto ya kufikiri juu ya wajibu wa serikali ktk kutoa huduma bora za kijamii kama vile elimu, afya, usafiri na usafirishaji nk nk kwa wananchi wake...

Si serikali inakusanya kodi kwa kila mtu..??? How comes ishindwe kutoa fedha za uendeshaji kwa shule zake...??

Let's think about. Hoja si nani alisoma wapi, lini na kwa namna gani...!!
 
Kuwa na vitabu ni basic needs za mwanafunzi. Hata kama unalipa Kodi lakini sio kila kitu service itatolewa bure na serikali. Kitabu, madaftari , pencil , pen hizo ni basics needs .
 
3. Nikajiuliza ina maana shule hii anayokwenda kusoma mwanangu haina vitabu? Imekuwaje inaanza kidato cha tano huku ikiwa haina vitabu? Kipi kilipaswa kuanza, majengo au vitabu na walimu kwanza?

Hivi mzazi kama nanunua vitabu vyangu kwa ajili ya mwanangu, si bora asomee nyumbani sasa na siku ya mtihani aende kufanya tu?

Hili wazo lako zuri pia, asomee nyumbani ataenda tu kufanya mitihani, na hao panya chura atawapasua hapo hapo nyumbani na wembe wa topaz.

Ndo umemaliza kusema na kushauri tayari?

Umeelewa mantiki (logic) ya hoja yangu kweli wewe?

Wewe shule uliyosoma wakati ule uliagizwa uende na karibu pickup nzima ya vifaa mfano fagio, mundu, kwanja, sabuni ya maji lita 5 au 10, maboksi ya vitabu nk nk ?

Kwani kuna sababu na ugumu gani kwa serikali kusema moja kwa moja tu kwa wananchi kuwa ada ni 1,000,000 ili tujue kuwa tunagharamia wenyewe elimu kuliko kudanganya watu na sera za kijinga na kipumbavu kuwa Tanzania tuna sera ya "elimu bure/bila malipo" huku mambo yakiwa tofauti..?

Tuache kudanganyana. Serikali ikokotoe tu gharama ya kusomesha mtoto mmoja kwa mwaka, iweke wazi na kumtaka kila mwenye mtoto alipie hiyo ili wanaoweza wapeleke watoto shule na wanaoshindwa washindwe...!!
 
1. Mwanangu amechaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita (F. V & VI) mwaka huu 2021 Shule ya Sekondari Nyantakara katika tahususi (Combination) ya Chemistry, Biology & Geography (CBG) iliyoko wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera. Hii ni shule ya serikali ya Tanzania.

2. Licha ya orodha ya mahitaji mengi anayotakiwa aende nayo mfano; fagio wa kufagilia ndani, sabuni ya maji ya chooni, fagio wa kufagilia nje, ream ya kataratasi nk nk, lipo hili ambalo mimi limeniacha hoi hata kujiuliuza kulikoni hizi shule za serikali? Nimeambiwa nimnunulie mwanangu

[A.] Vitabu yote vya tahasusi (subject combinations) anayokwenda kusoma yaani CBG & Basic Applied Maths

[B.] Dissecting Kit ya somo la Bailojia

3. Nikajiuliza ina maana shule hii anayokwenda kusoma mwanangu haina vitabu? Imekuwaje inaanza kidato cha tano huku ikiwa haina vitabu? Kipi kilipaswa kuanza, majengo au vitabu na walimu kwanza? Hivi mzazi kama nanunua vitabu vyangu kwa ajili ya mwanangu, si bora asomee nyumbani sasa na siku ya mtihani aende kufanya tu?

4. Nimelileta humu tujadiliane ili tujue majigambo ya serikali kuwa imeboresha elimu Tanzania, yana maana gani kama hali iko hivi ktk shule zake?

4. Naambatanisha na Joining instructions ya shule kwa ajili ya ushahidi na reference zaidi kwa atakayetaka kuthibitisha maelezo yangu.

5. Honestly, baada ya kuipata hii fomu ya maelekezo, nimeanza kusaka fedha tu na kufikiri kumpeleka shule ya binafsi.
View attachment 1829765View attachment 1829766View attachment 1829769
Na hapo wamekukumbusha tuu, lakini Mimi nilinunua kabla hata ya fomu sijapata na fomu ilipofika hapakuwa na sehemu ya kitabu
Advance wanafunzi ni wengi science, so sometimes kunakuwa na upungufu hasa biology na chemistry kwenye practical That's why, sometime wanaagiza vitu kama dissecting kit ili imuwie rahisi mtoto wako mwenyewe, Kuna Muda mtu mwenyewe unahitaji kuinunua ukiwa shuleni Kwa sababu ya upungufu.
So ni matumizi na faida Kwa mtoto wako na akimaliza atavirudisha sio kwamba shule itamnyang' anya.
 
Kuwa na vitabu ni basic needs za mwanafunzi. Hata kama unalipa Kodi lakini sio kila kitu service itatolewa bure na serikali. Kitabu, madaftari , pencil , pen hizo ni basics needs .
Kama unajadili kitu unachokielewa, hebu jibu maswali yafuatayo kwa ufasaha;

1. Je, unaelewa kuwa ili shule ianze au ipate kibali cha kuanza inapaswa ku - meet terms & conditions gani ambazo serikali yenyewe imeweka..?

2. Je, unaelewa kuwa moja ya sifa kuu kwa shule yoyote kuanzishwa iwe ya serikali au binafsi ni lazima iwe na vifaa vya kujifunzia na kufundishia vya kutosha ikiwemo vitabu...?

Kwa taarifa yako kama hujui kuna mpaka ratio kwa kila kifaa per mwanafunzi iwe ni kitabu, dawati etc

3. Katika shule za serikali ni nani mwenye jukumu la kuhakikisha shule hizi za zina vifaa vya kufundishia na kujifunzia vya kutosha...?

4. Watoto wa masikini wasio na uwezo wa kununua kitabu chochote achilia mbali kupiga photocopy wafanyeje iwapo shule ya serikali inaanzishwa huku ikiwa haina vifaa vya kufundishia na kujifunzia vikiwemo vitabu?

Je, inawezekana hujui hili simply tu kwa sababu wewe unakula na kusaza na kujamba jamba hovyo kwa sababu ya shibe yako, unadhani watu wote wana uwezo huo...?

Kununua vitabu vya ziada (reference books) is an option kwa atakayeona inafaa kuliingana uwezo wake wa kiuchumi kuongezea kwenye vilivyopo. Uwepo wa vitabu vya kiada (text books) mashuleni NI LAZIMA na ni jukumu la mwenye shule...

Please don't be too insensitive & selfish to that extent...

Fikiri kuhusu wengine pia. Ndiyo maana kukawepo na serikali...!!

5. Ni wazi kuwa wewe unajadili jambo hili kwa kutumia uzoefu wa kukariri na uliojaa mazoea mabaya ya kutotambua jukumu lako kama mwananchi na hutambui jukumu la serikali la ktk hili...!!!

NOTE:
å Nakuelimisha hili ili ujue. Kuwa, kila shule hususani za serikali ni lazima ziwe na vifaa vyote vya kujifunzia na kufundishia walimu na wanafunzi...

å Kuna vitabu vinaitwa kwa jina la TEXT BOOKS. Hivi ni lazima viwepo mashuleni. Mwanafunzi akitaka "ziada", anaweza yeye mwenyewe kwa kushirikiana na mzazi wake akanunua vitabu vya ziada (REFERENCE BOOKS) for more topical reference kwa manufaa yake.

Lakini hii kamwe haiwezi kuwa kama ni sharti la lazima ili mtoto apokelewe shule...!

Kwa heri na usiku mwema..
 
Kama shule kuna shamba kwa nini asibebe na jembe la kulimia? Umeambiwa shule ina trekta?

Kama hutaki hayo mpeleke private basi.
Jeshi siyo shule. BTW mimi nimpinga complication zisizo na lazima. Sipingi kununua vifaa. Karne ya leo unawaambia watoto wabebe majembe na makorokoro kibao yaliyopitwa na wakati kwenye dunia ya leo!
 
Na hapo wamekukumbusha tuu, lakini Mimi nilinunua kabla hata ya fomu sijapata na fomu ilipofika hapakuwa na sehemu ya kitabu
Advance wanafunzi ni wengi science, so sometimes kunakuwa na upungufu hasa biology na chemistry kwenye practical That's why, sometime wanaagiza vitu kama dissecting kit ili imuwie rahisi mtoto wako mwenyewe, Kuna Muda mtu mwenyewe unahitaji kuinunua ukiwa shuleni Kwa sababu ya upungufu.
So ni matumizi na faida Kwa mtoto wako na akimaliza atavirudisha sio kwamba shule itamnyang' anya.
This is not my point. Hiki ulichokiandika mimi nakielewa zaidi pengine kuliko wewe unavyoelewa...

I advice you to read my topic again and again and again until you realize what I want you to see and understand about the situation of almost all government schools today...

Hiyo joining instructions kwa wanafunzi inakupa picha ya jinsi government schools zilivyo na jinsi ambavyo serikali hii imeshindwa kuzi - finance shule zake ili ziweze kutoa huduma bora ya elimu...

This is contrary na political gimmicks zinazofanyika kuaminisha baadhi ya wananchi wajinga kuwa serikali inatenda wajibu wake...

Swali kwako;

Je, hivi ndivyo mambo yanavyopaswa kuwa...???
 
Kama unampeleka mwanao kusoma basi mnunulie hayo mahiyltaji But ka anaenda kukua bas Achana navyo
 
Back
Top Bottom