Hii tabia ya watendaji wa Elimu kutotii maagizo ya boss wao either ni ishara ya dharau au ni kushindwa kutii maagizo kwa makusudi. Sisi wazazi tunasubiri watoto wetu kurejea nyumbani alafu wanatokea maafisa Elimu na wakuu wa dhule wasio na nidhamu kwa maboss wao kwa makusudi wanaamua kuwakatalia watoto wetu shuleni.
Hizi shule za binafsi Wana sababu Mfu kuwa watoto wakirudi nyumbani et huwa wanazurura tu. Hii ni dhana ya hovyo kabisa maana wazaz wengine husubiri watoto warudi likizo ili wafundishwe maadili ya kifamilia na kijamii kulingana na ukuaji wao wa akili na mwili.
Wanadai kuwa wazazi huwa wanaridhia. Sio kweli bali wazazi hupewa tu taarifa ya mipango Yao na pale wazazi tunapoitwa huwa km ni kupokea tu agizo kutoka kwa uongozi wa shule. Na km wanaona wakija likizo watazurura basi wawe wanawapatia assignments ili wafanye wawapo makwao. Kinyume na hapo si tu kuwa wanawafanyia watoto ukatili wa kiakili bali wanatunyanyasa wazazi kwa kukosa fursa ya kukaa na kuongea na watoto wetu kadri ya mabadiliko ya miili yao.
Hivi Wizara wakati wanaweka mihula hawa wanaokaidi wanadhani wao walikuwa wajinga. Hakuna elimu Wala kazi isiyo na mapumziko. Hata hao Walimu wanahitaji kupumzika, siyo maroboti. Inafikia wakati watoto wengine wanaenda shule kabla ya kuvunja ungo, wanakaa huko hadi wanavunja ungo na hatimae kukosa taulo za kike.
Hii hali inakera sn, ebu Waziri wa Elimu tumia kipaza sauti ili tuone wapi panavuja.
Kwanza nadhani wew sio mzazi. Watoto wetu waache wabaki shule, tunataka walimu wawe na muda zaidi wa kuwafundisha wanetu.
Wanasiasa hamtakiwi kutuingilia kiivo, ni maamuzi yetu sisi wazazi, na tumechangia fedha zetu ili walimu waendelee kuwafundisha watoto wetu.
Nyie chawa wa kisiasa, tunawaomba tena tunawaomba sana, mmeiharibu nchi sana, na hata tumefikia hapa kielimu na hata mambo mengine kisa nyie chawa wa kisiasa.
Tafadhari Mkenda na hao chawa wako(mfano huyu aliyepost post hii) tuacheni na walimu wetu, mzazi ambaye anamtaka mwanaye akae nae nyumbani kuangalia the ottoman wakawachukue wanao, ila sisi wazazi wengine(huenda sisi ndo wajinga ila nyie msiotaka watoto waendelee na masomo mna akili) tuacheni na makubaliano yetu.
Aisee walimu wa shule x iliyopo tukuyu, kata ya kyimo. Nawashukuru Kwa kunifundishia mwanangu, mnafundisha adi jumamosi, mwanangu kabadirika sana.
Sina Cha kuwalipa walimu, ila MUNGU wa mbinguni awabariki, awape mahitaji yenu, mifuko yenu ijaye adi mkopeshe wengine.
Duuuuuhhhhh!!!! Kwa sababu yenu walimu, na hata Mimi nitawalea watoto wa wengine wakitanzania