Mnafiki Wa Kujitegemea
JF-Expert Member
- Dec 30, 2022
- 3,751
- 6,337
Ni kweli kwamba ushoga umeshamili sana shuleni kuzidi makanisani na misikitini? Nimesoma andiko lako hili nikiwa na dogo hapa,nikapata pia maoni yake.Ujue ni kwa vile siyo wazazi wote ni Walimu au wana wanafunzi huko. Ila ukweli hali ni tete sn, hasa shule za serikali. Yani unakuta kidato cha nne wanabakizwa ilihali shule siyo za bweni. Watoto wanarundikwa madarasani eti wanaita kambi. Humo madarasani wanarundikana km nzige huku wakilala chini kwenye mikeka wengine wenye uwezo wazazi wanawanunulia vigodoro vidogo. Hapo sasa unadhani ushoga utaisha vipi. Kuna watu humu sababu ya ukosefu wa taarifa ya yanayoendelea huko wao wanaona kubakiza watoto shule sawa tu.
Wewe fanya research tu kidogo watoto wa kidato cha nne shule za serikali zisizo za bweni utajua wanalala vipi. Kwa kweli ni hatari sn. Uhakika wa hao watoto kufirana ni 💯% ukizingatia ndiyo umri wa balee.
Ignorance ni kitu kibaya sana. Yani mtu anashaaikia eti kambi watoto wasirudi nyumbani!!!
Yeye anasema kule anako fundisha,ndio wana kijiji hawana elimu ama uelewa dhidi ya Ukimwi na VVU kiasi kwamba wanapeleka na kuwaunga binti zao na matumizi ya majira.
Lkn pia mzazi anampeleka shule mtoto ili serikali (mtendaji wa kijiji au Kata)asimsake. Kimsingi hawataki watoto wao wasome.
Kwenye suala la ushoga ananiambia kwa vijijini hasa kule aliko hawajui hizo mambo,ila vi binti vidogo kuanzia darasa la sita kubeba mimba ni kawaida kabisa na mwl akionekana kupinga watoto hasa wa kike kungonoa hata wazazi wata mshangaa huyo mwl.
Sasa nije kwenye suala la likizo.
Sidhani km hii ni njia sahihi ya kudhibiti jambo hili.
Nasema hivyo kwa sababu leo hii kuna UHASAMA MKUBWA SANA baina ya Walimu na wazazi wa wanafunzi.
Na mratibu MKUU wa UHASAMA HUO ni WANASIASA hasa MADIWANI. Hali hii hupelekea walimu kufanya na kutimiza wajibu wao mama wa kufundisha.
Kulea nje ya ulingo wake hafanyi kwakuwa matatizo yanayo paswa kutatuliwa kitaalamu siku hizi hutatuliwa kisiasa na hawa wanasiasa hapa ndipo wanapopigia kampeni hata km muda wa kampeni haujafika.
Mimi nyumbani ni karibu kabisa na st PIUS SEMINARY MAKOKO MUSOMA.
Pale siku ya kufunga shule Ina bandikwa ratiba ya mitihani inayoanza siku ya jumatatu inayofunguliwa shule.
Pamoja na ratiba hiyo,mwanafunzi haruhusiwi kuondoka na mali ya shule iwe ni kitabu cha kwenda kujisomea nyumbani wala 4 figure.
Na ktk mitihani itakayo fanyika siku ya kufungua shule,mwanafunzi atakeye shindwa kupata daraja A au B ktk somo mojawapo,barua tayari zilishachapwa,ziko kwa manager,pale jukumu lake ni kuweka mhuri,tarehe na saini.
Hivyo mwanafunzi ataekekea ofisini kwa manager ili akachukue hiyo barua na haruhusiwi kuingia bwenini,Mwl wa bweni atamkabidhi mizigo yake na yeye ataelekea stand ili akampelekee padre wa eneo anako tokea hiyo barua na huo ndo utakuwa mwisho wa huyo mwanafunzi kuonekana ndani ya st Pius seminary.
Shule ya pili ni WAJA,hizi shule ziko GEITA na hapa amewahi kufundisha huyu mdogo wangu.
Ktk shule hii kuna mikakati mbalimbali ambayo huwafanya wawe moja ya shule shindani hapa Tz.
WAJA,dogo anasema kuna wanafunzi wanao lipa nusu ada,sharti ni kuhakikisha km alienda pale akiwa na ufahulu wa DARAJA A ama DIVISION ONE POINT 7,hatakiwi kuporomoka. Kwa kutimiza sharti hilo basi mzazi ataendelea kulipa NUSU ADA.
Mbali ya hapo,hapa hukutana watoto walioenda kusoma na siyo KUCHEZA SINGELI (Mwenye kale ka video ka wale wanafunzi wanaocheza siingeli akasogeze hapa tafadhari). Sasa hawa wanafunzi mazungumzo yao ni kwenda kufanya utalii mlima Kilimanjaro na Dubai na kwingine duniani kutokana ahadi walizopewa na wazazi wao.
Wengine ni kwenda kusoma SINGAPORE, MALAYSIA na kwingineko duniani.
Kwa upande wa walimu wanalipwa, overtime wanalipwa pesa nzuri na mwl akifahulisha vizuri pesa km kawaida.
Sasa njoo ST KAYUMBA,muda wowote diwani anakuja shuleni kuwasalimia wanafunzi hata km ni muda wa vipindi,watapelekwa mstarini.
Usisahau maagizo ya UFAHULU WA 100% kutoka halmashauri na kwa hao madiwani.
Huo ufahulu wa 100% nikwa wanafunzi ambao hata hawajui kuandika majina yao achilia mbali+-*na/ ,physics, chemistry na mathematics hakuna walimu na maagizo hayaangalii hilo.
Sasa mchukue mwanafunzi wa Seminary,WAJA na mwanafunzi wa St Kayumba uniambie ni mwanafunzi yupi anaye paswa kuwa na full likizo.
Bila shaka jibu lako ni kati ya haya.
1: Seminary na WAJA
2: Wote.
Km jibu lako ni 1, una jidanganya ama una wadanganya Watanzania wanao dhani kuwa mkombozi wa maisha yao ni mwanasiasa kwani wao huwatengeneza watoto wao ili waje kuwa bosses wa taasisi nyeti na watawala wa nchi hii kwa kupokekezana wao kwa wao.
TRA,TANAPA,BOT,STAMICO,TPA na kwingineko ni wao tu na baadae hawa hawa st Kayumba wataendelea kulalamika kuwa tuna tawaliwa na koo za kina flani na blaablaa nyingi.
Mtaji wa wanasiasa na matajiri ni WAJINGA,hivyo kwa kulitambua hilo,wanasiasa wana mkakati wa kutengeneza wajinga wengi sana ili wawatawale watakavyo.
Jiulize,
Kuna kipindi ilisemekana kuna walimu kule SAME walikuwa kwenye semina ya ushoga,na ikasemekana hawali haikuwa wazi kuwa ni semina ya ushoga ila katikati ya semina ndo gia zikabadilika juu kwa juu.
1:Sasa je,unadhani hao walimu walihudhuria hiyo semina kwa bila ruhusa?
2: Ni nani aliye wapa ruhusa?
3: Ni nani aliyekuwa ana ratibu hizo semina?
4: Ni nani aliyempa kibali Mratibu wa hizo semina?
5: Je,umewahi kusikia kukamatwa kwa Mratibu wa hizo semina?
Mimi niseme kwamba tunao wajibu wa kuhakikisha kwamba tunakomesha tabia hizi kwa kushirikiana kinaga ubaga kati yetu sisi Watanzania na serikali yetu kwa namna yoyote ile.
Kwa bahati mbaya sana Watanzania tulio wengi na hasa wa kipato cha chini kazi ya malezi tumewaachia walimu ijapo hatuna mahusiano mazuri na hao walimu kutokana na CHUKI ILIYO PANDIKIZWA NA WANASIASA ILI WAJIPATIE UMAARUFU WA KISIASA.
Somo la mathematics halina mkazo tena kule NECTA pamoja na kwamba walimu wa hilo somo hawapo kwa shule za Msingi na sekondari ila UFAHULU WA 100% ni lazima mpaka kwa hili somo lisilokuwa na mvuto kwa wanafunzi na NECTA nao kwa kuliona hilo wakaondoa penalty ya kutofahulu somo hili.
Sasa ni mwanafunzi gani wa shule ya kata ataacha kulitenga hili ili afanye vizuri zaidi kwenye masomo mengine (kwa mjibu wa mawazo yao) km siyo wachache?
Vp,shule wanazosoma watoto wao (Seminary na WAJA) nako wana lipuuzia somo hili?
Jibu ni hapana kwakuwa ahadi ya mzazi wake kwake ni kuwa akimaliza chuo atakuwa Boss pale BOT,TRA,TPA,TANAPA na kwingineko na ndiyo maana mtoto huyu aliyeko WAJA akifanya mabadiliko chanya kwenye somo flani basi mzazi atamtafuta mwl kwa kificho lkn (uongozi wa shule haruhusu) na kumtuza mwl.
Haya siyo ya kuvujisha mtihani km huku kwenye UFAHULU wa 100%.
Sasa kipindi cha likizo hawa watoto hasa wa st KAYUMBA,walimu hasa wa masono yenye upungufu mkubwa wa walimu ndiyo hutumia kufundisha.
Hii ni tuition japo kwa makubaliano na wazazi na uongozi wa shule.
Ukiachana na mdudu USHOGA,hata mdogo wangu huyu toka akiwa form one mpaka form four,shule haikuwa na mwl wa physics and mathematics.
Walikuwa wakifundishwa na form 6 leavers na ufundishaji ulikuwa ukifanyika kabla ya kwenda vyuoni hivyo sisi km wazazi na walezi tulikuwa tukitoa fedha ya taaluma lkn pia kipindi cha likizo tulikuwa tukitoa kadri mwl atakavyo ridhia (haikuwa chini ya 15K) na wale form 6 leavers walikuwa wakifundishia hapo hapo shuleni.
Sasa zuio hili kwa sasa halina maana ya kwamba wanafunzi wapumzishe akili na kupata mafunzo mbalimbali ya kimaadili nyumbani,bali ni kutengeneza wajinga wengi ili tuwatawle sisi tu.
Nasema hivyo kwa sababu gani?
Kwani hawa watoto wataenda tuition ambako mzazi mwenyewe hapajui.
Mzazi huyu huyu ata hajui mtoto wake yuko ngazi gani ya kielimu (yuko bize na vikoba,michepuko na kuisaka fedha) wakati huo adui ni house girl/house boy ambaye ndiye aliye karibu na mtoto.
Mtoto muda wote yuko mafundisho,madrassa ambako huko ndiko kuliko chafuka kuzidi shuleni.
Jamani,tutengeneze urafiki na watoto wetu,tuwaepushe na balaa hili.
NAKARIBISHA KUKOSOLEWA.
Naziweka shukurani zangu hapa chini.