Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako hana kosa lolote anahukumiwa kimakosa

Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako hana kosa lolote anahukumiwa kimakosa

Nimefuatilia kwa ukaribu mjadala unaoendelea kwa sasa kuhusiana na kauli iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa dodoma mheshimiwa Mtaka kuhusu kuanzisha makambi ya kitaaluma kwa wanafunzi.

Katika mjadala huo nimesikitishwa sana na maoni ya wadau mbali mbali wanaomnyooshea kidole Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako.

Huyu mama ni mchapakazi mzuri mwenye misimamo isiyoyumbishwa hasa tunapokuja kwenye suala la elimu tangu alipokuwa katibu wa baraza la taifa la mitihani(NECTA).

Lakini tangu apewe dhamana ya uwaziri wa elimu mama wa watu amekuwa akizodolewa hapa na pale kwamba hafai muda mwingine kwa makosa ambayo siyo yake.

Mfano kwenye suala la usimamizi wa elimu, mama ndalichako anasimamia elimu kwa ngazi ya vyuo vya kati na vyuo vikuu huku usimamizi wa elimu ngazi ya msingi na sekondari ukiwa chini ya TAMISEMI ambayo inaongozwa na Ummy Mwalimu.

Cha kushangaza kwenye hili saga la Mkuu wa Mkoa anayelalamikiwa ni Ndalichako lakini watu wanasahau kwamba hilo jukumu la usimamizi wa elimu kwa sasa lipo chini ya tamisemi ambayo inaongozwa na waziri ummy kwahiyo kama ni lawama wanaopaswa kulaumiwa ni TAMISEMI, mama ndalichako anaonewa tu.
wewe unasema ndalichako ana misimamo na hayumbishwi SIO HUYU HUYU NDALICHAKO ALIYEKUBALI KUFUNDISHWA HISTORIA KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI NAWAKACHAPISHA VITABU VIANZE KUTUMIKA MWAKA JANA.?
Vipi alipoingia mama samia vile vitabu na hayo mambo ya historia yameyayukaje gafla kama kweli ana msimamo.
Viongozi wa hii nchi wapo kiulaji tu wanabadilika kama vinyonga.
 
Kaharibu sana katika utunzi na uchapishaji vitabu vya kiada na ziada kwa mashule - vina makosa mengi sana kwa sababu watunzi ni graduates, tangu lini graduate akatunga vitabu vya watoto wa darasa la 1 hadi 4 kwa mfano. Zamani vitabu hivi vilikuwa vinatungwa na walimu waliostaafu.
 
Back
Top Bottom