KERO Waziri wa Elimu Prof. Mkenda, tueleze mitihani ya kila wiki kwa kuwalipisha wazazi mchango wa Tsh. 1,500 kila Ijumaa , ndiyo sera uliyoiruhusu?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Watu mnachukulia poa maisha ya Tizii. Kuna familia huku uraiani hiyo 1500 ni pesa ya kula siku nzima. Humu JF kila mtu ni tajiri ndio maana hatujui mtaani hali ipoje.
 
Swiming lessons katika private schools ni 45,000 per month study tour 70,000 mhula wa mwisho come tógather party, nk huyu ni mtoto wa kitanzania pia mtagombania ajira zile zile. 1500 tu mtu analalamika kweli.
Mara moja moja toka kwenye hiyo "cycle" uliyopo mkongwe, ingia mtaani uone Watanzania wenzako wana maisha ya namna gani. 1500 ni pesa kubwa sana, kuna watu wana hali mbaya aisee, kuna wazazi huku mtaani anatamani kuona mtoto wake anafeli ili aepukane na aibu ya kushindwa kusomesha.
 
I

lla wewe ni kubwa jinga au mtoto wako ni kilaza hivi 1500 Kwa ajili ya mitihani ya mwanao ni ya kutolea Uzi kweli?Mimi nachokihisi mwanao hajiwezi ndio maana unahisi hiyo 1500 ni kutapeliwa.Upo sahihi
Wapo watoto ambao hawana watu/wazazi wa kuwapa hizo 1500 za mtihani.
 
Jf ilikuwa na vichwa vya logic na reasoning ila ninyi ndio mnafanya humu kuonekane kituko na member wote waonekane hovyo.
Wewe ni mmoja kati ya watu mnaofanya JF ionekane kituko!
1500 sio pesa ndogo, kuna Watanzania hawawezi kuwapa watoto wao hiyo pesa kila wiki. Kama familia yako inamudu kufanya hivyo shukuru sana.
 
Ndiooooooooooo tena ndiooooooooooo










KAZI ni kipimo cha UTU
 
Elimu
Elimu
Elimu






KAZI ni kipimo cha UTU
 
Kutoa Pesa ya mitihan kwa ajili ya ustawi wa mwanao inakutoa povu kiasi hiki
Hebu jiulize kwa wiki unahonga wanawake wangapi au kuzungusha round mezan
alafu shirikisha ubongo wako uone kipi bora
 
Ni 1500 sio 15000 watu mnachanganya fingure.....1500 ni kilo moja ya sembe.
 
Kjn tulia watoto waongezew ELIMU, ruzuku c toshelez
 
We jamaa unalalamika Sana

Mimi nimesoma miaka ya nyuma nilikuwa natoa buku kila mtihani

Niseme haujui faida za mitihani kwa mtoto wako
 
Poleni sana ndio mkaikatae sasa huko mashuleni msiishie kulalamika mitandaoni haisaidii, hata waziri unaemlalamikia hatokusaidia chochote mtoto wake yuko huko school of naniliu shida zako na mwanao wala hazijui
 
Ubarikiwe sana mkuu na mizimu ya kiafrika kwa wema unaomtendea huyo mtoto kwa kumpeleka shule ingali huna nasaba naye.
 
Ni 1500 sio 15000 watu mnachanganya fingure.....1500 ni kilo moja ya sembe.
Hiyo kilo moja ya sembe kuna watu mtaani inawashinda kuipata!
Mkongwe, kuna familia hapa Tanzania zinakula mlo mmoja tu kwa siku na huo mlo mmoja sio mlo kamili, halafu unataka hiyo familia itoe 1500 kila wiki kwaajili ya mtihani wa kujipima wa mwanafunzi!?
 
Sio mradi wa walimu bali ni makubaliano ya wazazi katika vikao, kuomba watoto waongezewe ufaulu..... Hivyo walimu ni watekelezaji.

Kama unachukua hatua chukua tu, hakuna serikali itakuja kukupa tamko kwenye hilo.
Kweli kabisa Madam Eva...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…