KERO Waziri wa Elimu Prof. Mkenda, tueleze mitihani ya kila wiki kwa kuwalipisha wazazi mchango wa Tsh. 1,500 kila Ijumaa , ndiyo sera uliyoiruhusu?

KERO Waziri wa Elimu Prof. Mkenda, tueleze mitihani ya kila wiki kwa kuwalipisha wazazi mchango wa Tsh. 1,500 kila Ijumaa , ndiyo sera uliyoiruhusu?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Watoto wa wanasiasa wanasoma kwenye Shule nzuri tena zenye gharama kubwa za mamilioni na mitaala ni tofauti na shule za kayumba wanazosoma watoto wenu.

Walimu wa watu wanajitahidi angalau wawasaidie watoto wenu hata mtoe mchango wa copy ya mitihani ya majaribio kwa watoto wenu mnaona nongwa,endeleeni kuwaamini wanasiasa uchwara wakiwaambia michango haitakiwi huku mnawashingilia ilihali watoto wao wanasoma feza etc
 
Hiyo ni mikakati ya watu husika ili kuongeza ufaulu , wazazi wa miaka hii mmekuwaje ?Mbona zamani watoto walisome hata kulipia shule jirani ila kufanya mitihani ya kujipima .

Waziri hausiki kikubwa hulipi ada , mitihani ya serikali inajulikana mara 4 kwa mwaka na hamjalipishwa .

Wenzenu wanafnya joint examination na wanalipia , watu walilipia mtihani mmoja hata 100/= mpak 200/= kila siku
 
Sio mradi wa walimu bali ni makubaliano ya wazazi katika vikao, kuomba watoto waongezewe ufaulu..... Hivyo walimu ni watekelezaji.

Kama unachukua hatua chukua tu, hakuna serikali itakuja kukupa tamko kwenye hilo.
Kwahiyo mitaala ambayo serikali inawekeza fedha za kutosha kuandaa maana yake serikali inajifurahisha pasipo kuwa na impact chanya?

Serikali haijaweka mitihani ya kila wiki kwasababu wataalamu walikaa wakaona mtaala ukifundishwa ipasavyo uta meet matarajio ya kielimu sasa wewe unapokuja na habari ya mitihani kila wiki unaona serikali haina maarifa ilipopanga mtaala?

Wewe hujui njaa za walimu ama utakuwa mwalimu maana kila kukicha wanabuni mbinu mpya za kumuumiza mzazi basala wapambane na serikali iwawekee mazingira mazuri ya stahiki zao waache usumbufu kwa mzazi.
 
Laiti kama mngekua mnajua uhalisia mngeshughulikia mambo yenu binafsi binafsi na si kusema serikali serikali.......

Labda tu mkuu nikuulize hivi mwl mmoja anaefundisha watoto 700+ huyu mwalimu ana muujiza gani wa kuwafikia hawa watoto tena kwa ufanisi?? Na hayo matokeo chanya yapatikane, Huyu ni mwalimu au ni mwamposa????

Tuendelee kuisubiri serikali, mkuu karibu beer ni furahiday
 
Waacheni Walimu na wenyewe wajipatie chochote kitu
Kila siku wanalia hali ni Ngumu hivyo wemepata Mbinu….

Yoote kwa yoote Mikakati hiyo inawasaidia sana Wanafunzi kwenye kuongeza Hari ya Kusoma

Ila waweke tuu utaratibu mzuri wa kukusanya hizo hela bila kuforce au kumchapa mwanafunzi
 
Sio mradi wa walimu bali ni makubaliano ya wazazi katika vikao, kuomba watoto waongezewe ufaulu..... Hivyo walimu ni watekelezaji.

Kama unachukua hatua chukua tu, hakuna serikali itakuja kukupa tamko kwenye hilo.
Binafsi naona walimu kama Wana ka mradi wao. Hivi unadaiwa remedial 5000 ni masomo matatu. Ila walichosoma mwezi mzima ni page 3 kila daftari
 
Kila Ijumaa wazazi tunadaiwa shs 1,500 kama ada ya mtihani. Je walimu wanafanya haya kwa ruhusa ya Wizara kama examination policy?

Mtoto asipoleta hela anapigwa. Tupelekane mahakamani na walimu wako kwa kuwapiga watoto bila sababu? Kama mtoto hakupewa hela, unampiga ili hela aitoe wapi?

Au Ni miradi ya waalimu kujiongezea kipato?
Wazazi watashindwa

Nitakupa ushahidi kama ukihitaji uthibitisho

Soma :
Bro 1,500 nayo inataka ikutoe roho?
 
Binafsi naona walimu kama Wana ka mradi wao. Hivi unadaiwa remedial 5000 ni masomo matatu. Ila walichosoma mwezi mzima ni page 3 kila daftari
Shida yenu na nyie mnadhani mwalimu ana miujiza yani ukishampa mtoto wako wewe umemaliza unakaa pembeni, fatiliaaa kagua daftari za mwanao hajafundishwa fika shule upate sababu, umelipa buku ya mtihani hakikisha mtoto kafanya mtihani, umesahishwa amerudishiwa na correction kafanyiwa.

Sio kutoa buku na kukaa kando na kuja kulalamika online haisaidii
 
Kwa uzoefu wangu wa kipelelezi,huwa hakuna vikao huru vya wazazi na walimu.Zaidi ni walimu kwa kushirikiana na kamati majambazi kupitisha agenda zao tamutamu(za kuwafaidisha wao)kwa kutumia mihutasari yenye mahudhurio ya wazazi/walezi.Wazazi huwa wanaburuzwa,kupewa lugha za vitisho na agenda kupita kihunihuni tu.
Sasa hapo shida si ni yenu maana hamjielewi!! Mtaburuzwaje!!!
 
Back
Top Bottom