KERO Waziri wa Elimu Prof. Mkenda, tueleze mitihani ya kila wiki kwa kuwalipisha wazazi mchango wa Tsh. 1,500 kila Ijumaa , ndiyo sera uliyoiruhusu?

KERO Waziri wa Elimu Prof. Mkenda, tueleze mitihani ya kila wiki kwa kuwalipisha wazazi mchango wa Tsh. 1,500 kila Ijumaa , ndiyo sera uliyoiruhusu?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
U
Mzazi nenda shule kamuone mkuu wa shule mwambie "sitaki mwanangu afanye hiyo mitihani, sitaki kuombwa hiyo hela wala sitaki mwanangu aguswe"

Pia usisahau kwenye vikao vya wazazi chukua mic sema hautaki hiyo mitihani haukubaliani na hilo swala hivyo hautatoa pesa
By that response, it is most likely wewe ni mwalimu wa primary 😀 😀 😀 😀
 
Mtoto akirudi nyumbani muulize shuleni hali ikoje nini kinaendelea, kama kafanyiwa kisa muulize huyo mwalimu.....kisha kaonane na mwalimu uso kwa jicho, mwanao afanyiwe ndivyo sivyo unaogopa?
Tunawaepusha ninyi walimu wa "Nyamhongolo" msifikishwe jela kwa kuua watoto wa wenyewe kwa madai ya buku bee.Shauri yenu.
 
Kila Ijumaa wazazi tunadaiwa shs 1,500 kama ada ya mtihani. Je walimu wanafanya haya kwa ruhusa ya Wizara kama examination policy?

Mtoto asipoleta hela anapigwa. Tupelekane mahakamani na walimu wako kwa kuwapiga watoto bila sababu? Kama mtoto hakupewa hela, unampiga ili hela aitoe wapi?

Au Ni miradi ya waalimu kujiongezea kipato?
Wazazi watashindwa

Nitakupa ushahidi kama ukihitaji uthibitisho
Akihitaji zaidi uthibitisho tuwasiliane nami nitakuongezea.
Nimepita shule nyingi watoto nao hali ni ngumu sana kwao.
Watoto wasipotoa hiyo hela 1500 wanafungiwa darasani hakuna kutoka kipindi cha mapumziko.
 
Mtoto wa darasa la pili anachangia 2000 kwa mitihani miwili(copies) yenye gharama halisi ya urudufishaji ni Tsh 200 unaona ni sawa?
Usiwe serious sana na maisha yaani unaona shida hata mwalimu Alibaba hiyo 700.
Lakini bar, michepuko, Kwa manabii, pesa mnatoa
Kumpa mwalimu tip unafungua Uzi ili abanwe umharibie kazi.
Sasa kama mtoto mitihani kafanya tatizo nini
 
Mzazi nenda shule kamuone mkuu wa shule mwambie "sitaki mwanangu afanye hiyo mitihani, sitaki kuombwa hiyo hela wala sitaki mwanangu aguswe"

Pia usisahau kwenye vikao vya wazazi chukua mic sema hautaki hiyo mitihani haukubaliani na hilo swala hivyo hautatoa pesa
Simple kabisa. Tuna watu wanapenda sana kudekezwa. No wonder some guys huko nje wanatuona kituko. Au akae na huyo mtoto amtungie mitihani home
 
Usiwe serious sana na maisha yaani unaona shida hata mwalimu Alibaba hiyo 700.
Lakini bar, michepuko, Kwa manabii, pesa mnatoa
Kumpa mwalimu tip unafungua Uzi ili abanwe umharibie kazi.
Sasa kama mtoto mitihani kafanya tatizo nini
Si aje awe mchepuko wangu kama anazipenda ndururu zangu.Mengine aniachie ntaongea na paroko wangu.
 
Simple kabisa. Tuna watu wanapenda sana kudekezwa. No wonder some guys huko nje wanatuona kituko. Au akae na huyo mtoto amtungie mitihani home
Msipende kuchukulia kila kitu kiwepesi ndiyo maana tunatukanwa kila siku kwa kutokuwa wafuatiliaji kama nchi.Kila kitu kuibiwa tu.
 
Si aje awe mchepuko wangu kama anazipenda ndururu zangu.Mengine aniachie ntaongea na paroko wangu.
Nenda kawambie Sasa walimuuza mtoto wako hutak afanye mitihani kwamba 1500 yako ni nyingi,
Sisi wazazi wengine pesa tutatoa, wewe msiburi waziri wa elimu akujibu apige marufuku majaribio na mitihani shuleni ikiwa watoto wake wako international school 🎒
 
Huo utaratibu wa kupiga watoto hata mie siupendi kwakweli unanikwaza sanaaa ndio wazazi msimame sasa.....sio kuandika tu huku watoto wakati wenu wanaoga fimbo
Mpenzi wangu Evelyn Salt acha kazi ya ualimu nikupe mchongo mwingine. Wewe ni mwalimu safi unaponzwa na wenzako.
 
Tunawaepusha ninyi walimu wa "Nyamhongolo" msifikishwe jela kwa kuua watoto wa wenyewe kwa madai ya buku bee.Shauri yenu.
🤣🤣🤣🤣
Unaepusha nini bana we ijumaa leo buku jero ishakutoka......

Hiyo hela masikini mtihani uje uchapwe utolewe kopi, wasimamie wasahishe wagawane sijui elf kumi naa, umasikini ni mbaya sana itoshe kusema hivi
 
Nenda kawambie Sasa walimuuza mtoto wako hutak afanye mitihani kwamba 1500 yako ni nyingi,
Sisi wazazi wengine pesa tutatoa, wewe msiburi waziri wa elimu akujibu apige marufuku majaribio na mitihani shuleni ikiwa watoto wake wako international school 🎒
Kuwa muelewa wewe.Tunapoandika hivi,hatuandiki kwa ajili ya watoto wetu tu.Hii inashuka hadi kwa watoto wa familia zenye uchumi mwembamba zaidi ya tishu.Hao ndiyo hasa wanazungumziwa.Uwe unachukulia mambo kwa upana.Usichukulie kama tunanunuliana kimbo za rubisi kwa fujo kilabuni.
 
Back
Top Bottom