Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda ameelekeza mafunzo ya Dini Shuleni yatolewe kwa kufuata miongozo na mitaala iliyopitishwa na pia kuridhiwa na Viongozi wa Dini.
Prof. Mkenda awaasa Wazazi kuwa makini na mafunzo yanayotolewa kwa watoto kuhusu masuala ya imani.
Amesema hayo jijini Mwanza akifungua Mafunzo kwa Maafisa Elimi Kata kuhusu miongozo ya uendeshaji na usimamizi wa Vituo vya Walimu (TRC's) pamoja na matumizi ya TEHAMA.