Kuna tatizo la ufundishaji ktk vyuo vyetu.
Najisikia vibaya kwamba tunalaumiwa kwa kutopenda kusoma vitabu lakini kuna uzembe kwa wafundishaji wetu ktk vyuo na hata sekondari kwa sasa.
Kuna mtindo wa kutumia simu za mkononi kuandika notisi badala ya kuwashawishi wanafunzi kusoma vitabu, Mtindo huu siyo mzuri na sijui ni kwa kiasi gani wizara imnaweza kuingilia kati.
Tumekuwa malimbukeni wa teknolojia kwa kiasi kikubwa sana.
Katika Mawaziri Rais Magufuli aliowarudisha kwenye awamu yake ya pili, ambao wame-perform vibaya Ndalichako ni among them.To me Wizara ya Elimu is the worst performing.Mimi kama mdau wa elimu, nilitegemea major reforms kwenye elimu, lakini hakuna reforms zozote,Waziri amelala tu.Kwa uchache nilitegemea reforms zifuatazo:
1.Uniformity kwenye elimu in terms of facilities,quality and school fees.Sioni sababu kwa mfano kwa nini kuwe na shule zinazolipa 20m na nyingine 250,000/=! Kiukweli nilitegemea kuona masterplan ya kufanya elimu yetu iwe uniform,lakini sijaona.
2.Quality of teachers enhancement:Waalimu wengi tulionao sasa hawakidhi haja kabisa.Kulipaswa kuwe na programme ya kuwa-phase out wasio na weledi appropriate na slowly tuingize qualified and better paid teachers.Sijaona mkakati wowote kuelekea huko.
3.Salary scales:Kama tunataka waalimu kuwa na morale ya kufundisha,ni vema Waalimu wakawa na na salary scales zao.Hapa napo sijaona mkakati!
4.Qualifications:Iwe mandatory kwamba kwa mtu kuwa mwalimu,ni lazima Form IV awe amepata Division I or II or else asiwe-entertained Wizara ya Elimu kabisa.Pamoja na unyeti wa swala hili,so far no initiative.
5.Mitaala na vitabu vya kufundishia ni vibovu mno.Kunatakiwa kuwe na programme ya makusudi, ili kuboresha eneo hili.So far sijaona chochote.No wonder wahitimu wetu ni vihiyo sana .
6.Elimu yetu haiwaandai vijana kujiajiri,inawaandaa kuajiariwa,this should be changed. Hata hivyo sioni mkakati wowote wa kupeleka elimu yetu huko.
Frankly sioni kwa nini huyu mama yupo,we need a better person in terms of ubunifu.