Waziri wa Elimu simamia ubora wa elimu na mbinu za ufundishaji

nakuunga mkono 100 kwa 100. Angekuwepo waziri kama Jafo au prof Mbarawa tungeshaona mambo kwa utofauti.
Huyu mama ni prof na amekuwa sekta ya Elimu muda mrefu lkn hana mchango wowote chanya katika sekta ya Elimu.
 
Vyuo vya binafsi ni sawa kwa sababu hao ni watu wazima. Lakini Primary education ni sehemu ya social service, duniani kote hutolewa na serikali. Ukijifanya kuitegemea sekta binafsi unaelekea kuzimu. Hadi leo nchi ya Uingereza elimu ya heshima iko kwa shule za serikali, siyo binafsi. Finland iliyo mbali kielimu kuliko nchi yoyote kwa sasa, elimu inashikiliwa na serikali. Sisi limbukeni, kwa mawazo yako tuendelee na uzembe huo.
 
Mimi Kama mdau wa elimu naomba nitoe mchango wangu katika hili
1.kwa Sasa Kuna uhaba mkubwa wa vitabu mashule. Hata vitabu vya msingi vya literature ni adimu.
2 .walimu wengi hawajawa active,kwa maana kuwa Mwalimu anatumia notes za 2011 mwaka huu 2021.hili ni Tatizo
3. Hakuna semina za kuwafundisha walimu kwa kuwakumbusha mambo muhimu ya kielimu.
Nini kufanyike?
1 kuwe na application of technology shuleni,mfano kutumia power point technology badala ya machaki na maubao meusi.
2.shule zigawiwe laptop au vifaa vitakavyosaidia kudisplay hizo notes na michoro,ikibidi hata video.
NB:Ili kuireform elimu Yetu iwe ni more technological kuliko sasa.kwa sasa 79%ha walimu hawaandiki notes ubaoni,wanafundisha tu wanawaambia wanafunzi Ndio waandike notes,au wakati mwingine hawatoi kabisa.

Tukumbuke mtaala wa elimu unataka Mwalimu awe na 25% katika kumwezesha Mwanafunzi,75%ni za Mwanafunzi mwenyewe kujiwezesha
 
Suala la vitabu ni kama suala la mitaala. Kuna wakati tunalazimisha kuhitaji kitabu kipya bila sababu. Sayansi ya sekondari ni ile ile bila kuhitaji kitabu kipya cha mwaka 2020. Hesabu, historia, jiografia zote ni yale yale! Labda civics ndo tunaweza kusema Chama kikuu cha upinzani siyo CUF ni CHADEMA au n.k. Hilo hatuna shida sana. Kuna baadhi anajidai, oooh mitaala imepitwa na wakati ukimuuliza anataka wafundishe mobile phone! Nonsense!

Kuna watu wanajifanya ni watalaamu wa elimu na wanaendana na wakati lakini kuna misingi ya kujifunza. Primary mwanafunzi anategemea 100% ya elimu yake itoke kwa mwalimu. Ukimnyima notes umemtoa ktk learning. Sekondari sikumbuki kwa uhakika lakini naelewa huwa ni zaidi ya 80% na kidogo kinachobaki, anaanza kuzoezwa kujitafutia. Ajitafutie vitabuni, simu bado wanaziona siyo za masomo na hatuna simu kwa ajili hiyo. Sehemu kubwa wanaishia kuwa na exchange ya mambo ya kijinga, nje ya masomo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…