robinson crusoe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2020
- 762
- 1,236
Vyuo vyetu bado viko hoi sana hata kwa miundombinu tukilinganisha na waliotuacha kama South Africa.
Bila ushabiki, kupitia mitandaoni SUA imekuwa ikisikika kama mfano wa chuo bora kwa uwezo wa wahitimu wake. Ni mfano wa wahitimu wavumilivu na wabunifu ktk taaluma zao. Hata hivyo, adui mkubwa ktk vyuo vyote nchini pamoja na UD ilikuwa udhaifu wa baadhi ya waalimu, hasa wa kiume kuwapa wanafunzi wa kike alama kwa uhusiano binafsi. Ni jambo ambalo lilipigwa vita sana hata wanafunzi wenyewe kuziita ni ‘ ushindi wa chupi’ [sic!].
Nimeletewa tukio hovyo na kijana wangu kwamba kuna mwanafunzi mwenzao hakufanya mitihani amewekewa alama za ufaulu kwa urafiki na mwalimu hapo SUA lakini wao waliofanya mitihani wakawekewa alama hovyohovyo bila kujali waluichopata kwenye test zao!
Hawa vijana kwa uanafunzi wao wamelifikisha kwa barua kulalamikia ubora wa mwalimu huyo lakini ni miezi miwili hawana majawabu ya tukio hilo. Yaonekana ni mtindo ulioota mizizi kwa baadhi ya wanataaluma. Hii ni ishara ya uongozi dhaifu. Unaweza ukasema ni tukio la mtu mmoja lakini ushujaa huo kautoa wapi kama mfumo uko imara?