Leo ndio nimeuona huu uzi,nikalinganisha na baadhi na maneno kuhusu elimu yetu na taifa kwa ujumla.
Naomba niandike machache kuhusu yanayoendelea katika vyuo vyetu,ila leo nitaanza na hiki chuo cha serikali kilichopo morogoro yaani SUA,nikipata muda tena nitakuja na mambo ya hovyo yaliyoko UDOM na UDSM.
Hapa nitaandika kuhusu mambo aliyosema mtoa mada na mengine ninayoyafahamu.
1. Kuhusu wanafunzi kupewa marks bila kufanya UE ni kawaida sana kwa SUA ya kipindi hiki,binafsi ninawafahamu wanafunzi watatu hawajafanya UE semester iliyopita ila kwenye matokeo wana A zao,wawili wapo mazimbu mmoja main campus,na utawala akiwamo DVC academic na VC wana taarifa hizi kwa ukamilifu wake kwa maandishi,email,simu na text pia,ila hawajawahi kufatilia.
2. Kwa kuongezea,SUA kwa sasa hakuna external examiners,yaani mtu wa mitihani kutoka nje,hivyo lecturers wengi wanafanya watakavyo wakijua hakuna wa kukagua habari zao. Hii imetoa hata mwanya wa baadhi kuwekea matokeo wanafunzi bila kufanya UE,mfano yule jamaa kule forest.,nasema hivi kwa kuwa wanamjua ila hawafatilii habari hizi.
3. SUA ya sasa wanafunzi wakifeli utasumbuliwa sana kuwabadilishia marks wafaulu.
Ninyi viongozi wa SUA mnakumbuka yule mzee wa agriculture ile kozi mlivyokuwa mnamsumbua kwa barua na kulazimisha aongeze marks wanafunzi wafaulu wakati wameshindwa?,KWA SASA AMEAMUA KUSARENDA WAKIFELI ANAWAGAWIA C,angekuwepo EXTERNAL EXAMINER MNGEFANYA HIVI?,au ndio maana hamtaki kupeleka external examiner?
Mnakumbuka issue ya yule kijana mnalazimisha afaulishe wakati wale mabinti ile kozi wamefeli mkaanza kumuundia zengwe ya rushwa?.
Mnakumbuka yule jamaa mmemtesa kuchezea matokeo hadi ameondoka ?
Je.mitihani yenu ya semester hii ina viwango vya kusema ni ya Chuo Kikuu?,mfano mtihani wa jana (26.7.2022) mchana kule mazimbu wanafunzi ndani ya saa 1 wamemaliza wakati mtihani ni masaa matatu.
Quality assurance ya Chuo iko wapi?,mmeipa meno kuuma?
4. SUA unaweza kwenda kusoma masters ila ukawa unafundishwa na T.A.,hapo college ya Agribussiness ni mchezo wao na uongozi upo hapo gorofani na taarifa hizi wanazo ila kila siku kujigamba SUA chuo bora kumbe kuna uozo namna hii.
5. SUA kuna rushwa ya ngono kubwa mno kuanzia kwenye mitihani hadi darasani.,kumbukeni yule mhadhiri mliyemkamata ipoipo na TAKUKURU ikasimamia usahihishaji wa SP ya yule binti.
6. SUA mazingira ya ufundishaji si salama kwa mustakabali wa taifa kwa ujumla.hapa naongelea miundombinu kama madarasa na maabara na vifaa vyake.
(Hapa nimewahi kaundika uzi kuwa SUA ina kozi hazina waalimu yaani lecturer hata mmoja ila wanadahili wanafunzi wakifika wanapigwa crash program kwa part time,mojawapo ya hiyo kozi ni kozi zote za ualimu zenye Physics,hawa maaabara hawana,kuna semester practical kozi hazifanyiki wanaenda kufanya crashing practical pale Muslim University),Jiulize Physics ya dunia ya leo hauna maabara unafundisha nini?
Yaani utakuta wanafunzi wa masomo ya sayansi maabara haipo na vifaa havipo ila mmedanganya hadi TCU na wizara ya elimu kuwa ipo na ina kila kitu kuweza kutoa degree, ila kazi kumezesha madesa wanafunzi,mitihani line by line aliyekariri notes ndio atafaulu halafu mnakuja kudanganya watanzania mna ubora,ubora ukiwepo ni wale watu wa VET sio ninyi kama chuo kizima,mkisema mna ubora mseme wazi ni VET au COA na si wote.
Hivi ulimwengu wa leo mtu analeta kifaa cha mwaka 80 eti ndio anatolea practical za animal sciences kweli?.....
7. SUA unaweza ukaona jambo haliko sawa na ukapeleka mapendekezo yako au kusema ila yatakayokupata utajua mwenyewe,ninyi viongozi wa SUA mnakumbuka mlichomfanya kwa jamaa aliyewaambia madarasa mabovu wanafunzi wanakaa nje mwaka jana?.
ifikie wakati tuwe wakweli,SUA ya leo si ile ya miaka ya Sembuche,sasa hivi mnajipendekeza kwa wanasiasa kwa kila njia.
8. SUA IS CORRUPTED, CASE CLOSED,TUKUTANE AIRPORT BAR leo saa 1 jioni.