Waziri wa Elimu, ubora wa Vyuo Vikuu hauko sawa; natoa mfano wa SUA

Waziri wa Elimu, ubora wa Vyuo Vikuu hauko sawa; natoa mfano wa SUA

Vyuo vyetu bado viko hoi sana hata kwa miundombinu tukilinganisha na waliotuacha kama South Africa.

Bila ushabiki, kupitia mitandaoni SUA imekuwa ikisikika kama mfano wa chuo bora kwa uwezo wa wahitimu wake. Ni mfano wa wahitimu wavumilivu na wabunifu ktk taaluma zao. Hata hivyo, adui mkubwa ktk vyuo vyote nchini pamoja na UD ilikuwa udhaifu wa baadhi ya waalimu, hasa wa kiume kuwapa wanafunzi wa kike alama kwa uhusiano binafsi. Ni jambo ambalo lilipigwa vita sana hata wanafunzi wenyewe kuziita ni ‘ ushindi wa chupi’ [sic!].

Nimeletewa tukio hovyo na kijana wangu kwamba kuna mwanafunzi mwenzao hakufanya mitihani amewekewa alama za ufaulu kwa urafiki na mwalimu hapo SUA lakini wao waliofanya mitihani wakawekewa alama hovyohovyo bila kujali waluichopata kwenye test zao!

Hawa vijana kwa uanafunzi wao wamelifikisha kwa barua kulalamikia ubora wa mwalimu huyo lakini ni miezi miwili hawana majawabu ya tukio hilo. Yaonekana ni mtindo ulioota mizizi kwa baadhi ya wanataaluma. Hii ni ishara ya uongozi dhaifu. Unaweza ukasema ni tukio la mtu mmoja lakini ushujaa huo kautoa wapi kama mfumo uko imara?
Ningeshauri tu ujue kwamba,kupata degree si akili tu,pia bahati na kibali cha Mwenyezi Mungu.

Wapo wengi hawakubahatika kupata degree na wana akili.
 
Mwambie kijana wako asome sana aache kuumia na mbinu za wengne sabu ata uku dunian anakokuja watu wanapewa kaz bila interview Wala CV ni mwendo wa chipi tu sasa ataumia sana
Mkuu mbona siwaskii mabint wakilalama kuwa vijana wanabinua viti kwa zile idara zinazosimamiwa na jinsia pendwa na kupata nafasi haramu au vijana hawajilengeshi kisawa sawa?
 
Nimemkumbuka Prof Mkude UDSM (Linguistics) Alisemaga Darasani "Maisha Haya Hayana Usawa, Pambana Ufaulu Kwa Njia Yoyote Ili Ada Yako Isiende Na Maji"

Mwenye Uchi Atatoa
Mwenye Pesa Atatoa
Mwenye Mzaz Kigogo Atamuweka

Nakumbuka Ya JESCA WA MAGUFULI UDOM Nabakia Kukaa Kimya Tu
Kilitokea nini kuhusu Jesca wa Magu huko UDOM?
 
Kijana wako yeye imemiathiri nini mtu kuwekewa alama ?
Najaribu kuliweka wazo lako hili mtaani. Tunamchoma moto kibaka, kwa sababu tu kaiba pasi ya mkaa nyumba ya jilani. Kaibiwa jilani, wewe inakuhusu nini? Kama tumefikia hatua ya kufikiri kama wewe, hii ni hatua ya kuanza kuwaza mkia sawa na nyani tu!

Mimi ni binadamu, natakiwa evolution inisogeze mbele siyo kunirudisha nyuma ya ustaarabu wa wanyama. Kwa ujumla ni hisia ya maisha ya kishenzi ndo inakaribisha mawazo kama haya ya kwako.
 
Vyuo vyetu bado viko hoi sana hata kwa miundombinu tukilinganisha na waliotuacha kama South Africa.

Bila ushabiki, kupitia mitandaoni SUA imekuwa ikisikika kama mfano wa chuo bora kwa uwezo wa wahitimu wake. Ni mfano wa wahitimu wavumilivu na wabunifu ktk taaluma zao. Hata hivyo, adui mkubwa ktk vyuo vyote nchini pamoja na UD ilikuwa udhaifu wa baadhi ya waalimu, hasa wa kiume kuwapa wanafunzi wa kike alama kwa uhusiano binafsi. Ni jambo ambalo lilipigwa vita sana hata wanafunzi wenyewe kuziita ni ‘ ushindi wa chupi’ [sic!].

Nimeletewa tukio hovyo na kijana wangu kwamba kuna mwanafunzi mwenzao hakufanya mitihani amewekewa alama za ufaulu kwa urafiki na mwalimu hapo SUA lakini wao waliofanya mitihani wakawekewa alama hovyohovyo bila kujali waluichopata kwenye test zao!

Hawa vijana kwa uanafunzi wao wamelifikisha kwa barua kulalamikia ubora wa mwalimu huyo lakini ni miezi miwili hawana majawabu ya tukio hilo. Yaonekana ni mtindo ulioota mizizi kwa baadhi ya wanataaluma. Hii ni ishara ya uongozi dhaifu. Unaweza ukasema ni tukio la mtu mmoja lakini ushujaa huo kautoa wapi kama mfumo uko imara?
SUA hiii.ambayo.inasifa lukuki duniani ikiwemo kumfundisha panya mahawa kazi ya kutegua mabomu
 
Kichwa cha habari hakina uhusiano na main content, hapo ndipo mtoa mada amefeli. Kitendo cha mwanafunzi mmoja kupewa maksi za chupi haiifanyi elimu yote ya Tanzania kuwa mbovu.
UD Ina nafuu kweli?
 
Nashauri baadhi ya mambo uyaweke vizuri kuhusu mtihani wa tarehe 26.07, na Kuhusu wanafunzi kufeli imekuwa nongwa na ni case kubwa na inamkumba mwalimu wa somo, inaonekana unaifahamu taasisi ni vema ukaweka bayana kwa kuchana vizuri Kwa hoja na vielelezo. Inaudhi Kwa mfumo wa tetesi tu.

Elimu ilishakufa enzi zetu za akina Professor Mathew Luhanga na Professor Biseko Lwoga
Umenikumbusha utawala wa (Injinia) Luhanga. Aliondoka akaja Mkandara mpenda sifa kwa rais. Matokeo yake UD ikageuka kuwa sekondari hadi leo. Yaani eti mwanafunzi anafukuzwa chuo kwa sababu ya kubishana na Mkandara. Tuliona ni kawaida matokeo yake wanafunzi wamekuwa wanyonge, hawana arguments, wengine ni waalimu hapo hapo na kwingineko, nadhani ndo hawa wanaogawa marks.
 
Kama hii ndio michango ya watanzania kwenye mada iliyoko mezani,basi tukubali tuna taifa la hovyo kabisa.

Yaani mtu ameleta suala kama hili,halafu mwingine anajibu kama vile kilichofanyika ni halali?,

Kuhusu SUA naomba muda wa kazi ukiisha nije kuandika uozo ulioko pale.

SUA iko overrated sana.
Nimerudi baada ya kuwa nimejisahau,asante jf kwa notification zenu.

Kuna watu wamehisi labda wengine hawaitaki SUA,isiwaziwe hivi kabisa,ijulikane tu leo watu wengi tuliosoma pale huwa hatukubali kuambiwa au kujulikana matatizo yetu na hii imesababisha kwa sasa kuna rundo la watu wanafiki sana wakiwa na degree mkononi.

Baadhi yetu tunaishi kwa sababu ya uwepo wa SUA,hivyo huwezi kuona mapungufu,chukulia huyo muuza miti hapo hata akiona kitu hakiko sawa atasema nini.

Naomba ieleweke,kwa uongozi ulioko SUA kwa sasa tusahau mabadiliko au chochote kwenye elimu kile chuo kabisa,utakuta jambo linatoka uongozini ila ni mawazo binafsi ya DVC academic au kiongozi fulani tu kwa kulazimisha yakapita kama muongozo.
Utakuta chuo kinajiendesha kwa mitaala ya zamani ila walikaa wakasema wanakuja na mtaala mpya kumbe kupiga pesa tu.

Kuhusu rushwa kwenye mitihani hii ipo wazi kibaya zaidi inajulikana ila wako busy kulindana,ukiripoti jambo uongozini unaanza kupewa vitisho kibao uwe mwanafunzi uwe mwalimu,ndio maana hata hao wanafunzi wameripoti hilo jambo ila ufatiliaji hakuna.
Bado rushwa kwenye usajili wa kupata hostel ni hatari tupu

Mwaka jana mwalimu wa kozi moja anawaambia wanafunzi wa record managements watoe chochote alete tutorials ambazo hizohizo ndio zitakua UE unafikiria nini hapo kitatokea.

Naona wameanza na UDOM ,tena kwa tangazo la wizara.
 
SUA hiii.ambayo.inasifa lukuki duniani ikiwemo kumfundisha panya mahawa kazi ya kutegua mabomu
Ukifanikiwa kufanya hata utafiti ukiwa sua yaani angalau uwe mwanajumuia pale,kuna mambo utajua tunadanganywa sana na watanzania wenzetu tuliowaamini kushika madaraka.
 
Wanajua Kwa vielelezo au Kwa hisia?! Na wewe ni nani katika taasisi hiyo ya SUA? Credibilit, reliability na validity ya uliyoyasema itapimwaje? Wewe ni sehemu ya SUA au snitch tu au mpiga mbiu ya wanyonge?
Samahani,unataka umjue aliyechangia ikusaidie nini?
Si ufatilie ili uturudishie hapa kuwa amesema ukweli au uongo?

Sema kwa mchango wa huyo jamaa anaijua SUA vizuri sana ukute yuko hapohapo anawaangalia mambo yenu tu.
 
Vyuo vyetu bado viko hoi sana hata kwa miundombinu tukilinganisha na waliotuacha kama South Africa.

Bila ushabiki, kupitia mitandaoni SUA imekuwa ikisikika kama mfano wa chuo bora kwa uwezo wa wahitimu wake. Ni mfano wa wahitimu wavumilivu na wabunifu ktk taaluma zao. Hata hivyo, adui mkubwa ktk vyuo vyote nchini pamoja na UD ilikuwa udhaifu wa baadhi ya waalimu, hasa wa kiume kuwapa wanafunzi wa kike alama kwa uhusiano binafsi. Ni jambo ambalo lilipigwa vita sana hata wanafunzi wenyewe kuziita ni ‘ ushindi wa chupi’ [sic!].

Nimeletewa tukio hovyo na kijana wangu kwamba kuna mwanafunzi mwenzao hakufanya mitihani amewekewa alama za ufaulu kwa urafiki na mwalimu hapo SUA lakini wao waliofanya mitihani wakawekewa alama hovyohovyo bila kujali waluichopata kwenye test zao!

Hawa vijana kwa uanafunzi wao wamelifikisha kwa barua kulalamikia ubora wa mwalimu huyo lakini ni miezi miwili hawana majawabu ya tukio hilo. Yaonekana ni mtindo ulioota mizizi kwa baadhi ya wanataaluma. Hii ni ishara ya uongozi dhaifu. Unaweza ukasema ni tukio la mtu mmoja lakini ushujaa huo kautoa wapi kama mfumo uko imara?
Niliwahi kuja na Uzi hapa Mwezi Mmoja tu uliopita nikisema jinsi Wanafunzi wa SUA wanavyopenda kula Bata Morogoro hasa katika Baa, huku Mabinti wakiliwa hovyo Uroda tena na Wauza Chips na Waendesha BodaBoda na nikasema kuwa Wahadhiri Wao waongeze Msuli na Waache kuwa Cheap kama kawaida GENTAMYCINE sikueleweka na Wapumbavu ( Mapopoma ) wengi hapa, ila nashukuru Leo nawe umekuja na the same Concern kuhusu SUA.
 
Inatisha sana mtihani ukiwa mgumu matokeo shida mtihani ukiwa rahisi shida, rahisi inapimwaje? na ngumu inapimwaje? Una haki na uhuru wa maoni japo kuna sehemu inaonesha Nia mbaya au mhemko au kuegemea hisia zako zaidi.
Hivi mbona kama unampinga jamaa kwa maneno rahisi hivi?,
Kwani mtihani mwepesi wa masaa matatu unapaswa kumalizwa ndani ya saa 1?
Huu ndio wepesi wa mtihani? Jamaa amesemea ubora sio wepesi au ugumu wa mtihani.

Naona umeanza kushambulia badala ya kumjibu au kuhakiki mambo yake,kama uko sua chekicheki uturudishie mambo tulinganishe taarifa zenu sio kuanza kushambulia mtu.

Amesema anajua watu watatu hawajafanya UE na matokeo wanayo,na taarifa zinajulikana uongozini,je ni kweli wana taarifa hawafanyii kazi?
Kuhusu hizo kozi za physics hazina mwalimu na maabara,je ni kweli?
Tusaidie haya itakua poa.
 
Katika dunia Kuna misingi mitatu tu ya kufanikiwa
1. Ukiwa unauwezo mkubwa wa kutunza Siri
2. Kutoa- hili ni suala la nature ningumu iwe Kwa mazuri au mabaya mtu anaetoa chochote ni ngumu Kwa mpokeaji kuendelea na msimamo na hasa akiwa na kitu specific hao malecture mnawalaumu bure alishindwa SAMSON! Tusisahau hata hela ya kaisali ilipokelewa pale hekaluni, tena hao malecture wanawafundisha uhalisia wa maisha kuwa hata ukimaliza hapo hayo utakutana nayo sana huko duniani. Ni ngumu kukwepa rushwa ya value against valueless eg A inathamani Kwa mwanafunzi ila Kwa lecture ni herufi kama herufi nyingine hivyo exchange ya human body to alphabet A unaweza ukaona urahisi ulivyo pia. Hili neno kutoa ndio msingi wa pili uliobeba mafanikio ya dunia ndio maana hata mungu hana shida lakini tunatoa Dhaka,sadaka,fungu la kumi nk hata kwa shetani Ili ufanikiwe unatoa kafara hivyo katika hili vijana mtaumia sana mioyo yenu chamsingi pambana kivyako Kwa angle nyingine maana aliepokea ukisema upambane nae ujue huto weza kwani Kila mtu duniani anapenda kupokea hivyo hata huko mlikoenda kushitaki nao ni wapokeaji ni sawa na kuombwa rushwa na police then unaenda shitaki Kwa police mwingine kisa anacheo kikubwa[emoji16]
3. Kuamini Kila kitu kinakinyume chake hapa duniani- hivyo kama Kuna haki basi kunabatili ila target ni moja ni wewe kuamua unapitia wapi kufikia target nje ya hapo neno furaha hautakuwa nalo milele juu ya huu USO wadunia
Hivyo huu ni ukweli usiopingika yaliobaki yote ni makelele ndio maana hata wanasiasa wakati wa uchaguzi hutoa Kila kitu tena bure Ili wapate wanachokitaka, yaani mjumbe ameshapokea then aanze kujiuliza sijui nani anahaki loh!
Na wew nae unategemewa kwenye familia kbs
 
Wanawake wapigwe vita Sana na wadhibitiwe maana wamechangia kwa sehemu kuiharibu hii Dunia. Wanapenda vitu vizuri vyote wavipate kwa kutumia silaha Yao kuu.
 
Kuhusu mtihani niliosema wa tarehe 26.7,huu umefanyika upande wa mazimbu,kusema vizuri ningeweza kufanya hivyo,nimestahi kazi za watu zisiwe rehani lakini wasimamizi waliokuwa pale wanajua kilichokuwa kinaitwa mtihani ni mtihani au maneno kwenye karatasi na nembo ya chuo,hata waliofanya hiyo pepa wanajua.

Hiyo kusema ni tetesi nimekubali kwa kuwa umesema wewe,bali mimi najua waliofanya hivyo wanajua sio tetesi.

Nimesema mimi binafsi ninafahamu wanafunzi watatu kuwa na matokeo bila kufanya UE,chukulia huyo wa mtoa mada ni wa nne,hao ni wale waliojulikana,vipi kuhusu hao tusiowajua?.
BOSS! Hii JF ni nzuri sana maana tunazungumza gizani bila kujulikana. Hebu tupia picha ya huo mtihani tuujadili kwa elimu zetu za vyuo vikuu. Tusiishie SUA tu, tuwafuate na UDOM (mbaharia), UD (wazee/wakongwe), MUHAS (wana super doctor), woote tuone mitihani na udhaifu wao. Elimu ya nchi inateketea mbele ya wanaojiita walisoma zamani.
 
Leo ndio nimeuona huu uzi,nikalinganisha na baadhi na maneno kuhusu elimu yetu na taifa kwa ujumla.

Naomba niandike machache kuhusu yanayoendelea katika vyuo vyetu,ila leo nitaanza na hiki chuo cha serikali kilichopo morogoro yaani SUA,nikipata muda tena nitakuja na mambo ya hovyo yaliyoko UDOM na UDSM.

Hapa nitaandika kuhusu mambo aliyosema mtoa mada na mengine ninayoyafahamu.

1. Kuhusu wanafunzi kupewa marks bila kufanya UE ni kawaida sana kwa SUA ya kipindi hiki,binafsi ninawafahamu wanafunzi watatu hawajafanya UE semester iliyopita ila kwenye matokeo wana A zao,wawili wapo mazimbu mmoja main campus,na utawala akiwamo DVC academic na VC wana taarifa hizi kwa ukamilifu wake kwa maandishi,email,simu na text pia,ila hawajawahi kufatilia.

2. Kwa kuongezea,SUA kwa sasa hakuna external examiners,yaani mtu wa mitihani kutoka nje,hivyo lecturers wengi wanafanya watakavyo wakijua hakuna wa kukagua habari zao. Hii imetoa hata mwanya wa baadhi kuwekea matokeo wanafunzi bila kufanya UE,mfano yule jamaa kule forest.,nasema hivi kwa kuwa wanamjua ila hawafatilii habari hizi.

3. SUA ya sasa wanafunzi wakifeli utasumbuliwa sana kuwabadilishia marks wafaulu.
Ninyi viongozi wa SUA mnakumbuka yule mzee wa agriculture ile kozi mlivyokuwa mnamsumbua kwa barua na kulazimisha aongeze marks wanafunzi wafaulu wakati wameshindwa?,KWA SASA AMEAMUA KUSARENDA WAKIFELI ANAWAGAWIA C,angekuwepo EXTERNAL EXAMINER MNGEFANYA HIVI?,au ndio maana hamtaki kupeleka external examiner?

Mnakumbuka issue ya yule kijana mnalazimisha afaulishe wakati wale mabinti ile kozi wamefeli mkaanza kumuundia zengwe ya rushwa?.

Mnakumbuka yule jamaa mmemtesa kuchezea matokeo hadi ameondoka ?

Je.mitihani yenu ya semester hii ina viwango vya kusema ni ya Chuo Kikuu?,mfano mtihani wa jana (26.7.2022) mchana kule mazimbu wanafunzi ndani ya saa 1 wamemaliza wakati mtihani ni masaa matatu.
Quality assurance ya Chuo iko wapi?,mmeipa meno kuuma?

4. SUA unaweza kwenda kusoma masters ila ukawa unafundishwa na T.A.,hapo college ya Agribussiness ni mchezo wao na uongozi upo hapo gorofani na taarifa hizi wanazo ila kila siku kujigamba SUA chuo bora kumbe kuna uozo namna hii.

5. SUA kuna rushwa ya ngono kubwa mno kuanzia kwenye mitihani hadi darasani.,kumbukeni yule mhadhiri mliyemkamata ipoipo na TAKUKURU ikasimamia usahihishaji wa SP ya yule binti.

6. SUA mazingira ya ufundishaji si salama kwa mustakabali wa taifa kwa ujumla.hapa naongelea miundombinu kama madarasa na maabara na vifaa vyake.
(Hapa nimewahi kaundika uzi kuwa SUA ina kozi hazina waalimu yaani lecturer hata mmoja ila wanadahili wanafunzi wakifika wanapigwa crash program kwa part time,mojawapo ya hiyo kozi ni kozi zote za ualimu zenye Physics,hawa maaabara hawana,kuna semester practical kozi hazifanyiki wanaenda kufanya crashing practical pale Muslim University),Jiulize Physics ya dunia ya leo hauna maabara unafundisha nini?

Yaani utakuta wanafunzi wa masomo ya sayansi maabara haipo na vifaa havipo ila mmedanganya hadi TCU na wizara ya elimu kuwa ipo na ina kila kitu kuweza kutoa degree, ila kazi kumezesha madesa wanafunzi,mitihani line by line aliyekariri notes ndio atafaulu halafu mnakuja kudanganya watanzania mna ubora,ubora ukiwepo ni wale watu wa VET sio ninyi kama chuo kizima,mkisema mna ubora mseme wazi ni VET au COA na si wote.

Hivi ulimwengu wa leo mtu analeta kifaa cha mwaka 80 eti ndio anatolea practical za animal sciences kweli?.....

7. SUA unaweza ukaona jambo haliko sawa na ukapeleka mapendekezo yako au kusema ila yatakayokupata utajua mwenyewe,ninyi viongozi wa SUA mnakumbuka mlichomfanya kwa jamaa aliyewaambia madarasa mabovu wanafunzi wanakaa nje mwaka jana?.
ifikie wakati tuwe wakweli,SUA ya leo si ile ya miaka ya Sembuche,sasa hivi mnajipendekeza kwa wanasiasa kwa kila njia.

8. SUA IS CORRUPTED, CASE CLOSED,TUKUTANE AIRPORT BAR leo saa 1 jioni.
Daah Mungu akusamehe sana kwa uongo ulioandika hapo namba 6.Hivi ni lini tulienda kufanya practical Muslim university[emoji848][emoji119][emoji119][emoji119].

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wewe inaonekana ni mwanafunzi wa sua hadi muda huu,basi tuambie elimu yenu hapo unaionaje?

Je,kwa sasa mna waalimu wa physics baada ya wale jamaa wawili TAs kuhama?
 
Wewe inaonekana ni mwanafunzi wa sua hadi muda huu,basi tuambie elimu yenu hapo unaionaje?

Je,kwa sasa mna waalimu wa physics baada ya wale jamaa wawili TAs kuhama?
Wale jamaa wamehama?
Wamehama sababu gani?
Na vyuo hani wamehamia?

Kuna yule mmoja mweupe hivi alikua na ndevu an manywele mengi,nimemsahau jina,jamaa akikufundisha electronics usipoelewa basi una shida kubwa,hakuna theory jamaa haijui,hakuna idea utasema asikupe solution,sijawahi kuona mtu kama yule aliyebobea.

Kuna siku aliwaalika jamaa fulani kwake wanakuambia sebule yote imejaa sensors,hatumii tv mpuuzi yule,anakuambia kwake kupumzika ni kulala tu akiamka mezani na electronics zake.

Jamaa nasikia toka mdogo anafanya hayo maelectronics tu,hata shuleni alikosoma ni hayohayo anafanya,ndio mtu wa kwanza kukuta anafanya kwa mikono yale anayofundisha.
Sua kama mmempoteza huyo basi kuna shida.

Yule mjinga atakua mtu mkubwa sana hapo mbele kwenye academia,halafu sikujua kama alikua Tutorial Assistant.
Yuko deep sana aisee,nawaza akiwa profesa itakuaje.

Nimemaliza hapo 2021,Niko kitaa.
 
Back
Top Bottom