Waziri wa Elimu, ubora wa Vyuo Vikuu hauko sawa; natoa mfano wa SUA

Ningeshauri tu ujue kwamba,kupata degree si akili tu,pia bahati na kibali cha Mwenyezi Mungu.

Wapo wengi hawakubahatika kupata degree na wana akili.
 
Mwambie kijana wako asome sana aache kuumia na mbinu za wengne sabu ata uku dunian anakokuja watu wanapewa kaz bila interview Wala CV ni mwendo wa chipi tu sasa ataumia sana
Mkuu mbona siwaskii mabint wakilalama kuwa vijana wanabinua viti kwa zile idara zinazosimamiwa na jinsia pendwa na kupata nafasi haramu au vijana hawajilengeshi kisawa sawa?
 
Kilitokea nini kuhusu Jesca wa Magu huko UDOM?
 
Kijana wako yeye imemiathiri nini mtu kuwekewa alama ?
Najaribu kuliweka wazo lako hili mtaani. Tunamchoma moto kibaka, kwa sababu tu kaiba pasi ya mkaa nyumba ya jilani. Kaibiwa jilani, wewe inakuhusu nini? Kama tumefikia hatua ya kufikiri kama wewe, hii ni hatua ya kuanza kuwaza mkia sawa na nyani tu!

Mimi ni binadamu, natakiwa evolution inisogeze mbele siyo kunirudisha nyuma ya ustaarabu wa wanyama. Kwa ujumla ni hisia ya maisha ya kishenzi ndo inakaribisha mawazo kama haya ya kwako.
 
SUA hiii.ambayo.inasifa lukuki duniani ikiwemo kumfundisha panya mahawa kazi ya kutegua mabomu
 
Kichwa cha habari hakina uhusiano na main content, hapo ndipo mtoa mada amefeli. Kitendo cha mwanafunzi mmoja kupewa maksi za chupi haiifanyi elimu yote ya Tanzania kuwa mbovu.
UD Ina nafuu kweli?
 
Umenikumbusha utawala wa (Injinia) Luhanga. Aliondoka akaja Mkandara mpenda sifa kwa rais. Matokeo yake UD ikageuka kuwa sekondari hadi leo. Yaani eti mwanafunzi anafukuzwa chuo kwa sababu ya kubishana na Mkandara. Tuliona ni kawaida matokeo yake wanafunzi wamekuwa wanyonge, hawana arguments, wengine ni waalimu hapo hapo na kwingineko, nadhani ndo hawa wanaogawa marks.
 
Nimerudi baada ya kuwa nimejisahau,asante jf kwa notification zenu.

Kuna watu wamehisi labda wengine hawaitaki SUA,isiwaziwe hivi kabisa,ijulikane tu leo watu wengi tuliosoma pale huwa hatukubali kuambiwa au kujulikana matatizo yetu na hii imesababisha kwa sasa kuna rundo la watu wanafiki sana wakiwa na degree mkononi.

Baadhi yetu tunaishi kwa sababu ya uwepo wa SUA,hivyo huwezi kuona mapungufu,chukulia huyo muuza miti hapo hata akiona kitu hakiko sawa atasema nini.

Naomba ieleweke,kwa uongozi ulioko SUA kwa sasa tusahau mabadiliko au chochote kwenye elimu kile chuo kabisa,utakuta jambo linatoka uongozini ila ni mawazo binafsi ya DVC academic au kiongozi fulani tu kwa kulazimisha yakapita kama muongozo.
Utakuta chuo kinajiendesha kwa mitaala ya zamani ila walikaa wakasema wanakuja na mtaala mpya kumbe kupiga pesa tu.

Kuhusu rushwa kwenye mitihani hii ipo wazi kibaya zaidi inajulikana ila wako busy kulindana,ukiripoti jambo uongozini unaanza kupewa vitisho kibao uwe mwanafunzi uwe mwalimu,ndio maana hata hao wanafunzi wameripoti hilo jambo ila ufatiliaji hakuna.
Bado rushwa kwenye usajili wa kupata hostel ni hatari tupu

Mwaka jana mwalimu wa kozi moja anawaambia wanafunzi wa record managements watoe chochote alete tutorials ambazo hizohizo ndio zitakua UE unafikiria nini hapo kitatokea.

Naona wameanza na UDOM ,tena kwa tangazo la wizara.
 
SUA hiii.ambayo.inasifa lukuki duniani ikiwemo kumfundisha panya mahawa kazi ya kutegua mabomu
Ukifanikiwa kufanya hata utafiti ukiwa sua yaani angalau uwe mwanajumuia pale,kuna mambo utajua tunadanganywa sana na watanzania wenzetu tuliowaamini kushika madaraka.
 
Wanajua Kwa vielelezo au Kwa hisia?! Na wewe ni nani katika taasisi hiyo ya SUA? Credibilit, reliability na validity ya uliyoyasema itapimwaje? Wewe ni sehemu ya SUA au snitch tu au mpiga mbiu ya wanyonge?
Samahani,unataka umjue aliyechangia ikusaidie nini?
Si ufatilie ili uturudishie hapa kuwa amesema ukweli au uongo?

Sema kwa mchango wa huyo jamaa anaijua SUA vizuri sana ukute yuko hapohapo anawaangalia mambo yenu tu.
 
Niliwahi kuja na Uzi hapa Mwezi Mmoja tu uliopita nikisema jinsi Wanafunzi wa SUA wanavyopenda kula Bata Morogoro hasa katika Baa, huku Mabinti wakiliwa hovyo Uroda tena na Wauza Chips na Waendesha BodaBoda na nikasema kuwa Wahadhiri Wao waongeze Msuli na Waache kuwa Cheap kama kawaida GENTAMYCINE sikueleweka na Wapumbavu ( Mapopoma ) wengi hapa, ila nashukuru Leo nawe umekuja na the same Concern kuhusu SUA.
 
Inatisha sana mtihani ukiwa mgumu matokeo shida mtihani ukiwa rahisi shida, rahisi inapimwaje? na ngumu inapimwaje? Una haki na uhuru wa maoni japo kuna sehemu inaonesha Nia mbaya au mhemko au kuegemea hisia zako zaidi.
Hivi mbona kama unampinga jamaa kwa maneno rahisi hivi?,
Kwani mtihani mwepesi wa masaa matatu unapaswa kumalizwa ndani ya saa 1?
Huu ndio wepesi wa mtihani? Jamaa amesemea ubora sio wepesi au ugumu wa mtihani.

Naona umeanza kushambulia badala ya kumjibu au kuhakiki mambo yake,kama uko sua chekicheki uturudishie mambo tulinganishe taarifa zenu sio kuanza kushambulia mtu.

Amesema anajua watu watatu hawajafanya UE na matokeo wanayo,na taarifa zinajulikana uongozini,je ni kweli wana taarifa hawafanyii kazi?
Kuhusu hizo kozi za physics hazina mwalimu na maabara,je ni kweli?
Tusaidie haya itakua poa.
 
Na wew nae unategemewa kwenye familia kbs
 
Wanawake wapigwe vita Sana na wadhibitiwe maana wamechangia kwa sehemu kuiharibu hii Dunia. Wanapenda vitu vizuri vyote wavipate kwa kutumia silaha Yao kuu.
 
BOSS! Hii JF ni nzuri sana maana tunazungumza gizani bila kujulikana. Hebu tupia picha ya huo mtihani tuujadili kwa elimu zetu za vyuo vikuu. Tusiishie SUA tu, tuwafuate na UDOM (mbaharia), UD (wazee/wakongwe), MUHAS (wana super doctor), woote tuone mitihani na udhaifu wao. Elimu ya nchi inateketea mbele ya wanaojiita walisoma zamani.
 
Daah Mungu akusamehe sana kwa uongo ulioandika hapo namba 6.Hivi ni lini tulienda kufanya practical Muslim university[emoji848][emoji119][emoji119][emoji119].

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Daah Mungu akusamehe sana kwa uongo ulioandika hapo namba 6.Hivi ni lini tulienda kufanya practical Muslim university[emoji848][emoji119][emoji119][emoji119].

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Wewe inaonekana ni mwanafunzi wa sua hadi muda huu,basi tuambie elimu yenu hapo unaionaje?

Je,kwa sasa mna waalimu wa physics baada ya wale jamaa wawili TAs kuhama?
 
Wewe inaonekana ni mwanafunzi wa sua hadi muda huu,basi tuambie elimu yenu hapo unaionaje?

Je,kwa sasa mna waalimu wa physics baada ya wale jamaa wawili TAs kuhama?
Wale jamaa wamehama?
Wamehama sababu gani?
Na vyuo hani wamehamia?

Kuna yule mmoja mweupe hivi alikua na ndevu an manywele mengi,nimemsahau jina,jamaa akikufundisha electronics usipoelewa basi una shida kubwa,hakuna theory jamaa haijui,hakuna idea utasema asikupe solution,sijawahi kuona mtu kama yule aliyebobea.

Kuna siku aliwaalika jamaa fulani kwake wanakuambia sebule yote imejaa sensors,hatumii tv mpuuzi yule,anakuambia kwake kupumzika ni kulala tu akiamka mezani na electronics zake.

Jamaa nasikia toka mdogo anafanya hayo maelectronics tu,hata shuleni alikosoma ni hayohayo anafanya,ndio mtu wa kwanza kukuta anafanya kwa mikono yale anayofundisha.
Sua kama mmempoteza huyo basi kuna shida.

Yule mjinga atakua mtu mkubwa sana hapo mbele kwenye academia,halafu sikujua kama alikua Tutorial Assistant.
Yuko deep sana aisee,nawaza akiwa profesa itakuaje.

Nimemaliza hapo 2021,Niko kitaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…