Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Muda uliotolewa wa kuboresha Mashine za EFD wa mwezi mmoja (kuanzia desemba 7 hadi Januari 7) hautoshi, kwa sababu mawakala wanaofanya kazi hiyo wamezidiwa na kazi hiyo kutokana na wingi wa mashine hizo na tayari wameomba kuongezewa muda wa kufanya marekebisho hayo ya ghafla yaliyosababishwa na TRA wenyewe kutokana na sababu zisizofahamika.
Tayari Kamishna wa TRA amekataa kuongeza muda na ameahidi kuwaadhibu wafanyabiashara walioshindwa kuboresha machine zao za EFD kwa muda uliopangwa , hapa analenga kuwakamua pesa wafanyabiashara ambao tayari wana hali mbaya kutokana na kuzorota kwa biashara nchini.
Sasa kwa hali hii kamishna haondoi Tatizo bali anaharibu zaidi, ikumbukwe kwamba wafanyabiashara wenye EFD hawajakataa kuboresha mashine zao bali mawakala wenye dhamana hiyo wameshindwa kumaliza kazi kwa wakati, wako ambao mashine zao ziko kwa mawakala mpaka sasa zikisubiri foleni ya kuboreshwa, sasa kamishna anapokataa kuongeza muda halisaidii Taifa bali ataleta mkanganyiko zaidi.
Namuomba Waziri wa fedha aingilie kati jambo hili ili kuokoa biashara za watu kwa Manufaa ya Taifa.