Leo Juni 12, 2025 Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwasilisha mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Machi 11,2025, Dkt. Mwigulu aliwasilisha Mwelekeo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2025/26 ilionyesha ongezeko la asilimia 13, ikikuwa kutoka TSh 50.29 Trilioni katika mwaka wa 2024|25 hadi TSh 57.04 trilioni.
Nini vitakuwa vipaombele vya serikari? Matarajio ya Wanachi, Taasisi na Asasi za Kiraia yatafikiwa?
"Mhe. Spika, katika Bajeti ya mwaka 2024/25, Serikali ilipanga kukusanya jumla ya Sh. Trilioni 50.29 kutoka katika vyanzo vya ndani na nje. Hadi Mei 2025, kiasi cha Sh. Trilioni 45.07 kimekusanywa, ikiwa ni sawa na asilimia 89.6 ya lengo la mwaka."
"Mapato yaliyokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yalikuwa Sh Trilioni 26.86 sawa na aslimia 91.3 ya lengo"
Kupunguza ada ya leseni ya uendeshaji wapikipiki, bajaji na guta kutoka shilingi 70,000hadi shilingi 30,000.
"Mapato yanayokusanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa yalifikia shilingi trilioni 1.26, sawa na asilimia 93.2 ya lengo"
"Misaada na mikopo nafuu kutoka nje ya nchi iliyopokelewa ilikuwa shilingi trilioni 5.32, sawa na asilimia 87.5 ya lengo"
"Mikopo ya ndani ikijumuisha mikopo ya kulipia dhamana za Serikali zilizoiva ilifikia shilingi trilioni 6.23, sawa na asilimia 94.1 ya lengo; na
"Mikopo ya masharti ya kibiashara ya nje ya nchi ilifikia shilingi trilioni 2.43, sawa na asilimia 81.3 ya lengo."
"Mhe. Spika, mapato ya ndani yameongezeka kutoka shilingi trilioni 20.59 mwaka 2020/21 hadi trilioni 29.83 mwaka 2023/24, huku wastani ukipanda kutoka trilioni 1.72 hadi 2.49 kwa mwezi. Kuanzia Julai 2024 hadi Mei 2025, wastani umefikia trilioni 2.83 kwa mwezi. Uwiano wa mapato kwa Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 13.7 hadi 15.0, ikidhihirisha mageuzi makubwa ya ukusanyaji mapato."
"Viashiria vinaonesha kuwa kwa mwaka 2024/25, tathmini ya sasa ya deni la Serikali kwa Pato la Taifa ni asilimia 40.3 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55, hivyo hatupaswi kuwa na hofu kuhusu jambo hili. Kwa upande wa thamani ya sasa ya deni la nje kwa Pato la Taifa, ni asilimia 23.6 dhidi ya ukomo wa asilimia 40 ambao ni kiwango cha kimataifa. Aidha, thamani ya sasa ya deni la nje kwa mauzo ya nje ni asilimia 123.8 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 180, hivyo hakuna sababu ya kuwa na hofu."
"Mhe. Spika, makadirio ya matumizi yaliyoidhinishwa na Bunge lako Tukufu kwa mwaka2024/25 ni shilingi trilioni 50.29 ambapo shilingi Trilioni 33.75 ni matumizi ya kawaida na shilingi Trilioni 16.54 ni matumizi ya maendeleo. Katika kipindi cha Julai 2024 hadi Mei 2025, ridhaa yamatumizi iliyotolewa ilikuwa shilingi trilioni 42.90,sawa na asilimia 85.3 ya lengo la mwaka."
"Mhe. Spika, kati ya kiasi hicho, shilingi Trilioni 30.63 (asilimia 90.8) zilitolewa kwa matumizi ya kawaida, na shilingi Trilioni 15.74 (asilimia 95.1) kwa miradi ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na Trilioni 3.47 kutoka kwa Washirika wa Maendeleo kupitia D-Fund."
"Mhe. Spika, kati ya Julai 2024 hadi Mei 2025, fedha zilitumika kugharamia deni la Serikali shilingi Trilioni 11.16, mishahara ya watumishi Trilioni 10.27, na maandalizi ya
Uchaguzi Mkuu ni Sh. Bilioni 741.5. Pia, Serikali imelipa madeni yaliyohakikiwa shilingi Trilioni 1.01, hatua iliyosaidia kulinda mitaji na kuchochea uchumi."
"Serikali imeendelea kugharamia miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja na viwanja vya ndege (Trilioni 1.58), reli ikiwemo SGR (Trilioni 1.68), pamoja na miradi ya umeme JNHPP na REA (Bilioni 574.8) pamoja na ujenzi wa viwanja vya mpira kwa maandalizi ya AFCON 2027 (Bilioni 179.8)."
"Serikali pia imeendelea kuboresha huduma za jamii kwa kugharamia mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya juu na vyuo vya kati (Bilioni 636.0), Elimumsingi na Sekondari bila Ada (Bilioni 444.7), miradi ya maji (Bilioni 378.7), ununuzi wa dawa na vifaa tiba (Bilioni 414.7), ujenzi wa hospitali (Bilioni 47.2), na vituo vya afya na Zahanati (Bilioni 7.3)."
"Hadi Aprili 2025,
deni la Serikali lilifikia shilingi Trilioni 107.70, likijumuisha
deni la nje trilioni 72.94 na
deni la ndani trilioni 34.76. Tathmini ya Oktoba 2024 imeonesha kuwa deni ni himilivu kwa muda mfupi, wa kati na mrefu, ambapo viashiria vinaonesha thamani ya sasa ya deni kwa Pato la Taifa ni asilimia 40.3 (ukomo 55%), deni la nje kwa Pato la Taifa asilimia 23.6 (ukomo 40%), na deni la nje kwa mauzo ya nje asilimia 123.8 (ukomo 180%)."
"Kwa takwimu za 2024, shule za msingi zimeongezeka hadi 20,533 kutoka 3,270, walimu 229,840 kutoka 9,885 na wanafunzi 11.39m kutoka 486,470. Sekondari zimefika 6,269 kutoka 41, walimu 128,686 kutoka 764 na wanafunzi 3.31m kutoka 11,832. Vyuo vya ualimu 65 kutoka 8, vyuo vikuu 79 kutoka 1, wahadhiri 8,625 kutoka 6 na wanafunzi 334,854 kutoka 14."
"Baadhi ya hatua zilizochukuliwa ni pamoja na ruzuku kwa kaya maskini (Sh. bilioni 9,615), elimu bila ada (Trilioni 1.3), mikopo ya elimu ya juu (Trilioni 2.7), na ruzuku ya nusu bei ya mbolea (Bilioni 708.6) kati ya 2021/22–2023/24."
Utekelezaji wa Miradi ya Kimkakati
"Serikali ya Awamu ya Sita ilikuta Mradi wa JNHPP ukiwa unaendelea na sasa umefikia asilimia 99.93 na umeanza kuzalisha umeme. Pia, ujenzi wa Daraja la Kigongo–Busisi na barabara unganishi umekamilika kwa asilimia 100 na unatarajiwa kuzinduliwa Juni 19, 2025."
"Dkt. Samia alipokea mradi wa SGR ukiwa asilimia 83.55 (Dar–Morogoro) na asilimia 57.57 (Morogoro–Makutupora), ambapo vipande hivyo sasa vimekamilika, treni zimeanza kazi na hadi Machi 2025 abiria 2,054,828 wamesafirishwa na mapato ya TSh. bilioni 60.25 kukusanywa."
"Mhe. Spika, sisi sote tumeshuhudia usafiri kwa kutumia reli ya SGR umepunguza muda wa safari kutoka saa tisa (9) hadi saa tatu (3) kwa safari kati ya Dar es Salaam na Dodoma. Vilevile, utekelezaji wa kipande cha tano cha kutoka Mwanza– Isaka (km 341) umefikia asilimia 63.16. Kwa upande mwingine, Serikali imefanya majaribio ya Treni ya mizigo ya SGR tarehe 01 Juni 2025."
"Itakumbukwa Mheshimiwa Dkt. Samia alianza ujenzi wa reli ya SGR ambapo utekelezaji umefikia asilimia 14.53 kwa Lot 3 (Makutupora–Tabora), asilimia 6.65 kwa Lot 4 (Tabora–Isaka), pamoja na kuanzisha Lot 6 (Tabora–Kigoma) na Lot 7 (Uvinza–Musongati). Serikali inaendelea kutafuta fedha na wabia kukamilisha miradi hiyo."
"Upatikanaji wa fedha utawezesha ujenzi wa reli ya SGR maeneo yaliyobaki kama Kaliua–Mpanda–Karema, Mtwara–Mbamba Bay na matawi ya Liganga na Mchuchuma, Tanga–Arusha–Musoma, pamoja na reli za mijini Dar es Salaam na Dodoma. Serikali za Tanzania, Zambia na China zilisaini MoU ya kuboresha uendeshaji wa reli ya TAZARA."
"Mhe. Spika, mwaka 2024/25 Serikali imewekeza katika bandari zetu ili kuongeza tija na kuchochea maendeleo, hasa katika kilimo, madini, na usambazaji wa bidhaa. Kupitia ushirikiano na sekta binafsi, Bandari ya Dar es Salaam imepata mafanikio kama ongezeko la mapato ya kodi ya forodha kutoka shilingi trilioni 7.08 hadi 8.26 kutoka Julai 2024 hadi Februari 2025, na kupungua kwa gharama za uendeshaji kutoka bilioni 975.0 hadi 685.2. Hii imetoa fedha za ziada kwa miradi kama ujenzi wa Kituo cha Matenki (Tank Farm) Bandari ya Dar es Salaam."
"Kupunguzwa kwa ushuru wa
vinywaji vya kuongeza nguvu (energy drinks) vinavyozalishwa ndani kutoka
Shilingi 561 hadi
134.2 kwa lita, lengo likiwa kuweka unafuu kwa wazalishaji wa ndani, kuongeza ushindani na kuchochea uwekezaji, hatua inayotarajia kupunguza mapato ya Serikali kwa shilingi milioni 170.2."
"Kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango chaasilimia 10 kwenye sabuni zinazoingizwakutoka nje ya nchi zinazotambulika kwa HSCodes 3401.11.00, 3401.19.00, 3402.50.00 na 3402.90.00. Lengo la hatua hii ni kulindawazalishaji wa ndani na kuongeza ajira. Hatuahii inatarajia kuongeza mapato ya Serikali kwakiasi cha shilingi milioni 143,395.8."
"Kuongeza kiwango cha ushuru wa bidhaakwenye malipo ya kutazama vipindi maalumvya televisheni
(pay per view) kutoka asilimia 5hadi asilimia 10. Lengo la hatua hii ni102kuongeza mapato ya Serikali. Hatua hiiinatarajia kuongeza mapato kwa kiasi chashilingi milioni 113,376.8."
"Kupunguza
ada ya usajili wa pikipiki zabiashara kutoka
shilingi 340,000 hadi
shilingi 170,000 kwa miaka mitatu. Ada husika italipwa wakati wa usajili wa awali pekee."
"Kupunguza ada ya leseni ya uendeshaji wa pikipiki, bajaji na guta kutoka shilingi 70,000 hadi shilingi 30,000."
"Kutoza ushuru wa forodha kwa kiwango chaasilimia 25 badala ya asilimia 10 kwenyekaratasi za kutolea risiti za kielektronikizinazotambulika kwa HS Code 4811.90.00 kwamwaka mmoja. Lengo la hatua hii ni kulindaviwanda vya ndani vinavyozalisha bidhaa hii."
"Kuongeza kifungu cha 8(7) ambacho kinampa mamlaka Waziri mwenye dhamana na masuala ya biashara kuainisha shughuli za
kibiashara ambazo hazipaswi kufanywa na wageni. Utaratibu wa utekelezaji wa kifungu hiki utafanywa kupitia Amri (Order) itakayotolewa na Waziri ambayo itakua na orodha ya shughuli za kibiashara ambazo hazipaswi kufanywa na wageni."
"
Kutoza shilingi 500 kwa
kila tiketi inayotolewana mtoa huduma za
usafirishaji kwa njia ya treni."
"
Kutoza shilingi 1000 kwa
kila tiketi inayotolewa na mtoa huduma za
usafirishaji kwa njia ya anga. Hatua hizi kwa pamoja zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa shilingi
milioni 586,404.9.