Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba anawasilisha Bajeti Kuu ya Serikali 2025/2026

Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba anawasilisha Bajeti Kuu ya Serikali 2025/2026

Deni la taifa trillion 107, mama yenu kashakopa trillion 30 na ushee, tangia aokote dodo chn ya mnazi.

mama mitano tena, mpaka atoke madarakani 2030 kama atatoboa deni litakuwa over 150 trillion wallah.
 
Hivi hawawezi achana na uchawa hata kwenye mambo serious.

Anasoma budget au kusifia viongozi, waziri wa fedha kageuka msemaji wa CCM kama vile yeye ndio Makalla.
Kwanza mna moyo sana wenye uthubutu wa kufuatilia hilo bunge.
 
Kwanza mna moyo sana wenye uthubutu wa kufuatilia hilo bunge.
Nimeona copy ya speech na-download huko nishaokoa bando langu.

Waziri wa ulinzi yeye
Waziri wa afya yeye
Msemaji wa serikali yeye.
Msemaji wa CCM yeye

Inaonekana bila ya kupachika mambo mengine muda wa kusoma budget ungekuwa mfupi.

Sasa hivi yupo kwenye kuelezea mafanikio walau hili ni linamaelezo ya budget.

Sasa hivi kawa waziri wa kilimo.
 
Nimeona copy ya speech na-download huko nishaokoa bando langu.

Waziri wa ulinzi yeye
Waziri wa afya yeye
Msemaji wa serikali yeye.
Msemaji wa CCM yeye

Inaonekana bila ya kupachika mambo mengine muda wa kusoma budget ungekuwa mfupi.

Sasa hivi yupo kwenye kuelezea mafanikio walau hili ni linamaelezo ya budget.

Sasa hivi kawa waziri wa kilimo.
Aisome mwigulu Nchemba
 
Leo Juni 12, 2025 Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwasilisha mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Machi 11,2025, Dkt. Mwigulu aliwasilisha Mwelekeo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2025/26 ilionyesha ongezeko la asilimia 13, ikikuwa kutoka TSh 50.29 Trilioni katika mwaka wa 2024|25 hadi TSh 57.04 trilioni.

Nini vitakuwa vipaombele vya serikari? Matarajio ya Wanachi, Taasisi na Asasi za Kiraia yatafikiwa?


"Mhe. Spika, katika Bajeti ya mwaka 2024/25, Serikali ilipanga kukusanya jumla ya Sh. Trilioni 50.29 kutoka katika vyanzo vya ndani na nje. Hadi Mei 2025, kiasi cha Sh. Trilioni 45.07 kimekusanywa, ikiwa ni sawa na asilimia 89.6 ya lengo la mwaka."

"Mapato yaliyokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yalikuwa Sh Trilioni 26.86 sawa na aslimia 91.3 ya lengo"

"Mapato yanayokusanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa yalifikia shilingi trilioni 1.26, sawa na asilimia 93.2 ya lengo"

"Misaada na mikopo nafuu kutoka nje ya nchi iliyopokelewa ilikuwa shilingi trilioni 5.32, sawa na asilimia 87.5 ya lengo"

"Mikopo ya ndani ikijumuisha mikopo ya kulipia dhamana za Serikali zilizoiva ilifikia shilingi trilioni 6.23, sawa na asilimia 94.1 ya lengo; na

"Mikopo ya masharti ya kibiashara ya nje ya nchi ilifikia shilingi trilioni 2.43, sawa na asilimia 81.3 ya lengo."

"Mhe. Spika, mapato ya ndani yameongezeka kutoka shilingi trilioni 20.59 mwaka 2020/21 hadi trilioni 29.83 mwaka 2023/24, huku wastani ukipanda kutoka trilioni 1.72 hadi 2.49 kwa mwezi. Kuanzia Julai 2024 hadi Mei 2025, wastani umefikia trilioni 2.83 kwa mwezi. Uwiano wa mapato kwa Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 13.7 hadi 15.0, ikidhihirisha mageuzi makubwa ya ukusanyaji mapato."

"Viashiria vinaonesha kuwa kwa mwaka 2024/25, tathmini ya sasa ya deni la Serikali kwa Pato la Taifa ni asilimia 40.3 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55, hivyo hatupaswi kuwa na hofu kuhusu jambo hili. Kwa upande wa thamani ya sasa ya deni la nje kwa Pato la Taifa, ni asilimia 23.6 dhidi ya ukomo wa asilimia 40 ambao ni kiwango cha kimataifa. Aidha, thamani ya sasa ya deni la nje kwa mauzo ya nje ni asilimia 123.8 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 180, hivyo hakuna sababu ya kuwa na hofu."

"Mhe. Spika, makadirio ya matumizi yaliyoidhinishwa na Bunge lako Tukufu kwa mwaka2024/25 ni shilingi trilioni 50.29 ambapo shilingi Trilioni 33.75 ni matumizi ya kawaida na shilingi Trilioni 16.54 ni matumizi ya maendeleo. Katika kipindi cha Julai 2024 hadi Mei 2025, ridhaa yamatumizi iliyotolewa ilikuwa shilingi trilioni 42.90,sawa na asilimia 85.3 ya lengo la mwaka."

"Mhe. Spika, kati ya kiasi hicho, shilingi Trilioni 30.63 (asilimia 90.8) zilitolewa kwa matumizi ya kawaida, na shilingi Trilioni 15.74 (asilimia 95.1) kwa miradi ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na Trilioni 3.47 kutoka kwa Washirika wa Maendeleo kupitia D-Fund."

"Mhe. Spika, kati ya Julai 2024 hadi Mei 2025, fedha zilitumika kugharamia deni la Serikali shilingi Trilioni 11.16, mishahara ya watumishi Trilioni 10.27, na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu Bilioni 741.5. Pia, Serikali imelipa madeni yaliyohakikiwa shilingi Trilioni 1.01, hatua iliyosaidia kulinda mitaji na kuchochea uchumi."

"Serikali imeendelea kugharamia miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja na viwanja vya ndege (Trilioni 1.58), reli ikiwemo SGR (Trilioni 1.68), pamoja na miradi ya umeme JNHPP na REA (Bilioni 574.8) pamoja na ujenzi wa viwanja vya mpira kwa maandalizi ya AFCON 2027 (Bilioni 179.8)."

"Serikali pia imeendelea kuboresha huduma za jamii kwa kugharamia mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya juu na vyuo vya kati (Bilioni 636.0), Elimumsingi na Sekondari bila Ada (Bilioni 444.7), miradi ya maji (Bilioni 378.7), ununuzi wa dawa na vifaa tiba (Bilioni 414.7), ujenzi wa hospitali (Bilioni 47.2), na vituo vya afya na Zahanati (Bilioni 7.3)."

"Hadi Aprili 2025, deni la Serikali lilifikia shilingi Trilioni 107.70, likijumuisha deni la nje trilioni 72.94 na deni la ndani trilioni 34.76. Tathmini ya Oktoba 2024 imeonesha kuwa deni ni himilivu kwa muda mfupi, wa kati na mrefu, ambapo viashiria vinaonesha thamani ya sasa ya deni kwa Pato la Taifa ni asilimia 40.3 (ukomo 55%), deni la nje kwa Pato la Taifa asilimia 23.6 (ukomo 40%), na deni la nje kwa mauzo ya nje asilimia 123.8 (ukomo 180%)."

"Kwa takwimu za 2024, shule za msingi zimeongezeka hadi 20,533 kutoka 3,270, walimu 229,840 kutoka 9,885 na wanafunzi 11.39m kutoka 486,470. Sekondari zimefika 6,269 kutoka 41, walimu 128,686 kutoka 764 na wanafunzi 3.31m kutoka 11,832. Vyuo vya ualimu 65 kutoka 8, vyuo vikuu 79 kutoka 1, wahadhiri 8,625 kutoka 6 na wanafunzi 334,854 kutoka 14."

"Baadhi ya hatua zilizochukuliwa ni pamoja na ruzuku kwa kaya maskini (Sh. bilioni 9,615), elimu bila ada (Trilioni 1.3), mikopo ya elimu ya juu (Trilioni 2.7), na ruzuku ya nusu bei ya mbolea (Bilioni 708.6) kati ya 2021/22–2023/24."

Utekelezaji wa Miradi ya Kimkakati
"Serikali ya Awamu ya Sita ilikuta Mradi wa JNHPP ukiwa unaendelea na sasa umefikia asilimia 99.93 na umeanza kuzalisha umeme. Pia, ujenzi wa Daraja la Kigongo–Busisi na barabara unganishi umekamilika kwa asilimia 100 na unatarajiwa kuzinduliwa Juni 19, 2025."



Utekelezaji wa 30%%% wa budget hii ni kama maonyesho tu
 
Akiwasilisha inakuaje,?CCM akili zao wanazijua wenyewe maana bunge la bajeti lilikuwa lina jadili derby ya Simba na Yanga,Kumfukuza Gwajima,kuwajibu Gen Z na kumtukunuku Samia tuzo gani sijui,kwahio msitegemee la maana hapo.
nimesoma mara kadhaa nimekutana na hili neno deni la taifa ni himilivu sijui hili neno ni kwa faida ya nani
 
Deni la taifa trillion 107, mama yenu kashakopa trillion 30 na ushee, tangia aokote dodo chn ya mnazi.

mama mitano tena, mpaka atoke madarakani 2030 kama atatoboa deni litakuwa over 150 trillion wallah.
Mbna 200 kabisaa, hii awamu sio atakopa? Ni kuzoa mahela WB. LOL
 
Back
Top Bottom