Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo avikumbusha vyombo vya habari kuwa kutumia uvumi kama habari rasmi ni kukiuka sheria

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo avikumbusha vyombo vya habari kuwa kutumia uvumi kama habari rasmi ni kukiuka sheria

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Innocent Bashungwa ametoa wito kwa vyombo vya habari kuendelea kutoa taarifa zinazotolewa kwenye vyanzo rasmi na kuepuka kutumia uvumi/rumours, kwani kitendo hicho ni kukiuka sheria na kitapelekea vyombo hivyo kuwajibika. Waziri Innocent amesema hayo kupitia ukurusa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.

"Natoa wito kwa wanahabari na wananchi wetu kuendelea na utaratibu wa kupata taarifa kupitia vyanzo rasmi vya habari. Kutumia rumours/uvumi kama habari rasmi ni kukiuka sheria zinazosimamia sekta ya habari. Epukeni kusambaza habari ambazo mtawajibika nazo."

Bashungwa.jpg
 
Hapana atakuwa anaongelea uvumi wa Bernard Morrison kukosana kocha wa simba, Maulid Kitenge aliripoti huo uvumi halafu Haji Manara akachafua hali ya hewa🙂
Ha ha ha ha haaaaaaaaa!!! Kwakweli!
 
Angetumia nafasi hiyo kukanusha huo uvumi nakueleza ukweli bila hivyo uvumi utaendelea , ile kitu ni kama njaa haina baunza jobaaa!!!!
 
I cement that kabisaaaa maana watu wamekalia umbea tuuu , oo flani anaumwa ooh flani kafa , turudi kwenye misingi yetu ya zamani ya utu ifike mahali usifurahie mwenzio akipata matatizo hata kama ni kweli. Enzi za mwalimu haikuwa hivi tubadilike
 
Back
Top Bottom