Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Balozi Augustine Mahiga akana Tanzania kujitoa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Balozi Augustine Mahiga akana Tanzania kujitoa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga amekanusha taarifa za Serikali kujitoa katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (AfCHPR)

Akifafanua zaidi kuhusu dai hilo, Dkt. Mahiga anasema serikali haijajitoa katika Mahakama hiyo isipokuwa imeiandikia barua Mahakama hiyo kuondoa itifaki ambayo inapingana na sheria ya Tanzania.

Anaongeza kuwa, endapo marekebisho hayo ya itifaki yasipofanyiwa kazi na Mahakama hiyo ndipo Serikali itajiondoa lakini kwa sasa Serikali haijajitoa kama inavyosemekana.

Miongoni mwa shughuli za Mahakama ya Haki za Binadamu na Watu ni kusikiliza kesi zinazofunguliwa na Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Watu dhidi ya Serikali.

Aidha, Miongoni mwa kesi za Tanzania zilizowahi kuamuliwa katika Mahakama hiyo ni pamoja na kesi ya Mwanamuziki maarufu aitwaye Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na Mwanaye Johnson Nguza maarufu kama Papi Kocha.

Hata hivyo, Dkt. Mahiga hakuweka bayana kipengele chenye utata katika itifaki hiyo na kuwataka waandishi wamuulize Mwanasheria Mkuu wa Serikali.


======
Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga amesema Serikali haijajitoa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AFCHPR) bali imeiomba kubadilisha itifaki.

Alisema uamuzi wa kujitoa utakuja baada ya ombi la kubadilisha itifaki hiyo yenye utata katika shughuli za kimahakama kushindikana.

Alisema Serikali imeiandikia barua mahakama hiyo yenye makao makuu yake jijini Arusha kuondoa itifaki hiyo ambayo inapingana na sheria ya Tanzania na kusisitiza kuwa kwa sasa haijajitoa bali inasubiri marekebisho hayo.

“Tunachosubiri kwa sasa ni marekebisho hayo ila ikishindikana basi tutajitoa. Kwa sasa bado hatujajitoa kama inavyosemekana,” alisema.

Miongoni mwa shughuli za mahakama hiyo ni kusikiliza kesi zinazofunguliwa na mashirika yasiyo ya kiserikali au wananchi dhidi ya Serikali.

Mpaka sasa nchi tisa kati ya 30 zilizoridhia itifaki hiyo zimesaini kuwapa uhuru huo wananchi wake kudai haki zao mahakamani pindi Serikali inapowatendea kinyume. Zilizosaini Benin, Burkina Faso, Ivory Coast, Gambia, Ghana, Mali, Malawi, Tanzania na Tunisia.

Zilizoridhia ni Algeria, Burundi, Cameroon, Chad, Comoros, Kongo, Gabon, Kenya, Libya, Lesotho, Msumbiji, Mauritania, Mauritius, Nigeria, Niger, Rwanda, Jamuhuri ya Kidemokrasia Sahrawi, Afrika Kusini, Senegal, Togo na Uganda.

Miongoni mwa kesi za Tanzania ambazo zimewahi kuamriwa kwenye mahakama hiyo ni ya mwanamuzi maarufu Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Johnson Nguza au Papii Kocha.

Babu Seya na wanaye walihukumiwa kufungwa maisha na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2004. Walikata rufaa Mahakama Kuu wakashindwa, Mahakama ya Rufani ikawaachia huru watoto wawili lakini Babu Seya mwenyewe na Papii Kocha wakaendelea kutumikia adhabu hiyo.

Mwaka 2015 walikimbilia katika mahakama hiyo na Machi 23, 2018 ikakubali kukiukwa kwa baadhi ya haki zao hivyo kuamuru waachiwe ingawa walishapata msamaha wa Rais.

Kwenye maelezo yake Dk Mahiga hakueleza kipengele chenye utata katika itifaki hiyo bali alitaka aulizwe Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Chanzo: Mwananchi

Pia Soma:

Hapo muhishimiwa anamaanisha ile hadithi ya nyama ya nguruwe sili lakini mchuzi nakunywa. Huwezi kubadili itifaki ya mahakama ya kimataifa kwa ajili ya nchi moja tu!!
 
Kwa nini hataki kutaja kipengele kinachokinzana na Sheria zetu? Kwa vyo vyote vile kitakuwa kinaibana Serikali!
Wamepewa maagizo kuhakikisha pandikizi lao linashinda uchaguzi Chadema, ili ikitokea likashindwa kihalali chama kifutwe,
Kwa amri ya msajili.
Chama kikifutwa chadema watakosa pa kufungulia kesi, kwani mahakama za Ibrahimu Mussa ziko kwapani kwa jiwe,
Kimbilio liliokuwa limebaki in Mahakama ya afrika
 
Jiwe kila anachofanya hapa nchini nionavyo ni sahihi na hataki aingiliwe na kwa sababu mahakama za Tz anaziamlisha atakavyo alifikili na huko ataziamlisha, ila mahiga ni spika tu anayeteseka ni jiwe mwenyewe.
 
Wapinzani wanapenda sana kuzusha uwongo
No evidence no right to speak [emoji116]
IMG_20191202_195905.jpeg
IMG_20191202_195849.jpeg
 
Na kwanini wakatae wananchi kuwashitaki. ? . nia uvu ndani yake
Kipengele muhimu cha mtu binafsi kuishitaki nchi kwenye mahakama ya Afrika kikiondolewa hiyo mahakama itabaki jengo tu la kujikinga na mvua.
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga amesisitiza kuwa Tanzania haijajiondoa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) bali imeiomba iondoe itifaki inayokinzana na sheria ya Tanzania, na endapo ombi hilo lisipotekelezwa, ndipo itajiondoa.

Wakati huo huo Shirika la Amnesty International limesema uamuzi wa Tanzania kuondoa itifaki inayoruhusu watu na NGOs kuishtaki katika Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) kunaoneshwa serikali inakwepa kuwajibishwa. Tanzania itakuwa ya pili kuondoa itifaki hiyo baada ya Rwanda.

Source. Swahili times

20191203_105437.jpg


20191203_105603.jpg


20191203_105413.jpg
 
Panapofuka Moshi..............this serves as an official notice of withdrawal. Sasa Mahiga anatueleza nini, na Kabudi anatueleza nini-au mimi kingereza kimenipiga chenga? Mbona moto umesha onekana!!!
 
Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga amesema Serikali haijajitoa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AFCHPR) bali imeiomba kubadilisha itifaki.

Alisema uamuzi wa kujitoa utakuja baada ya ombi la kubadilisha itifaki hiyo yenye utata katika shughuli za kimahakama kushindikana. Alisema Serikali imeiandikia barua mahakama hiyo yenye makao makuu yake jijini Arusha kuondoa itifaki hiyo ambayo inapingana na sheria ya Tanzania na kusisitiza kuwa kwa sasa haijajitoa bali inasubiri marekebisho hayo.

“Tunachosubiri kwa sasa ni marekebisho hayo ila ikishindikana basi tutajitoa. Kwa sasa bado hatujajitoa kama inavyosemekana,” alisema.

Miongoni mwa shughuli za mahakama hiyo ni kusikiliza kesi zinazofunguliwa na mashirika yasiyo ya kiserikali au wananchi dhidi ya Serikali. Mpaka sasa nchi tisa kati ya 30 zilizoridhia itifaki hiyo zimesaini kuwapa uhuru huo wananchi wake kudai haki zao mahakamani pindi Serikali inapowatendea kinyume. Zilizosaini Benin, Burkina Faso, Ivory Coast, Gambia, Ghana, Mali, Malawi, Tanzania na Tunisia.

Zilizoridhia ni Algeria, Burundi, Cameroon, Chad, Comoros, Kongo, Gabon, Kenya, Libya, Lesotho, Msumbiji, Mauritania, Mauritius, Nigeria, Niger, Rwanda, Jamuhuri ya Kidemokrasia Sahrawi, Afrika Kusini, Senegal, Togo na Uganda. Miongoni mwa kesi za Tanzania ambazo zimewahi kuamriwa kwenye mahakama hiyo ni ya mwanamuzi maarufu Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Johnson Nguza au Papii Kocha. Babu Seya na wanaye walihukumiwa kufungwa maisha na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2004. Walikata rufaa Mahakama Kuu wakashindwa, Mahakama ya Rufani ikawaachia huru watoto wawili lakini Babu Seya mwenyewe na Papii Kocha wakaendelea kutumikia adhabu hiyo. Mwaka 2015 walikimbilia katika mahakama hiyo na Machi 23, 2018 ikakubali kukiukwa kwa baadhi ya haki zao hivyo kuamuru waachiwe ingawa walishapata msamaha wa Rais. Kwenye maelezo yake Dk Mahiga hakueleza kipengele chenye utata katika itifaki hiyo bali alitaka aulizwe Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Hii ndiyo anayokana? Mwenzake ameshasaini
 

Attachments

  • Kujitoa Mahakama ya Africa.jpg
    Kujitoa Mahakama ya Africa.jpg
    40.8 KB · Views: 1
Sioni hiyo mahakama ibadili taratibu zake kwa ajili ya nchi moja tu inayolalamika. So yeah this is going south.

Yaani sisi ni waoga kupita hata Burundi na Rwanda, kuna udharimu gani sijui tunafanya mpaka tuogope kiasi hiki hizi mahakama
 
Back
Top Bottom