Nimememwelewa mwigulu, Raisi alitakiwa kutoa taarifa Kwa Baraza , ni Baraza lipi? Kwa mazingira yake hlo Baraza lilikuwepo , na hivyo busara aliyotumia Raisi ya kusitiri mwili Kwanza zen maswala ya kuvunja Baraza yaendelee ipo poa tuuu...anyway naweza kosolewa mana sio mtaalam wa Sheria Na katiba ....
TLS walitoa mwanga kuhusu hili.
Mwigulu naye amesema vyema tu.
Huu ni mjadala mzuri tu.
Lakini mimi nadhani tatizo liko kwenye katiba kwa sababu imenyamaza kimya kuhusu mazingira ya namna hii yanapojitokeza.
Labda watunga katiba hawakuwahi kufikiri kuwa Rais aliye madarakani anaweza kufa.
Problem iko hapa. Nadhani hekima iendelee kutumika.
Na kwa haraka haraka tu, walichosema TLS ndicho kina - make sense zaidi.
Kwamba, waziri yeyote huapa kwa Rais. Hawa waliopo waliapa kwa Rais ambaye si Rais tena, hayupo, amekufa na hana mamlaka ya Urais tena...
Na ktk kiapo kama sitakosea huapa wakisema, " nitakuwa mtiifu kwa JMT na kwa Rais..."
Sasa waliyemwapia kuwa watamtii, hayupo, hana madaraka hayo tena. Yupo mwingine. Obviously, ni sharti wale kiapo kingine tena, kwake.
Si lazima ateue wapya. Akipenda anaweza kuendelea na hawahawa ila kwa viapo vipya.
Kwa wakuu wa mikoa RCs, DCs na wote wasioapa direct kwa Rais, wao hawahusiki na viapo hivi moja kwa moja unless otherwise.
Japokuwa kila mtu angependa na anategemea kuona mabadiliko makubwa kuanzia chini hadi juu.