Waziri wa Maji, Jumaa Aweso anashiriki Kongamano la Kumi na Tano la Uwekezaji katika Ujenzi wa Miundombinu

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso anashiriki Kongamano la Kumi na Tano la Uwekezaji katika Ujenzi wa Miundombinu

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso anashiriki Kongamano la Kumi na Tano la Uwekezaji katika Ujenzi wa Miundombinu (15th International Infrastructure Investment and Construction Forum and Expo) linalofanyika tarehe 19-21 Juni, 2024, Macao SAR, China.

Waziri Aweso ni moja wa waalikwa kati ya Mawaziri mbalimbali duniani wanaohusika na sekta zinazoendana na utekelezaji wa Miradi mbalimbali ikiwa kwa Tanzania Sekta ya Maji imetambuliwa kuwa ya mfano katika mafanikio kwenye muktadha huu.

Aidha lengo pia ni uzoefu wa namna gani Serikali kupitia Wizara ya Maji imefanikiwa katika utekelezaji wa Miradi ya Maji inayotoa huduma kwa wananchi na mageuzi yaliofanyika katika Sekta hii.
 
Hapo anashiriki huku akili inawaza posho nono na hakuna kitu atajifunza. Hopeless kabisa
sasa Ben,
hapo hopeless atakua nani, wewe au waziri 🤣

unadai anawaza posho tu. Yes, hiyo inaweza kua sasa, sasa mtu kama huyo mwenye uhakika wa posho anaweza kua hopeless kweli?🐒

wewe hopeful unawaza nini sasa kwa mfano 🤣
 
Back
Top Bottom