Waziri wa Maliasili na Utalii, Pindi chana awasili ofisini, awataka watumishi kutekeleza 4R za rais samia kwa vitendo

Waziri wa Maliasili na Utalii, Pindi chana awasili ofisini, awataka watumishi kutekeleza 4R za rais samia kwa vitendo

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Hazara Chana (Mb) amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua kusimamia kwa mara nyingine Wizara ya Maliasili na Utalii.

Ameyasema hayo leo Agosti 19,2024 aliporipoti katika ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, Mtumba jijini Dodoma.

Akizungumza na watumishi, Mhe. Balozi Chana amewataka watumishi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia 4R za Rais Samia Suluhu Hassan ambazo ni maridhiano (Reconciliation), mabadiliko (Reforms), ustahimilivu (Resilience) na kujenga upya (Rebuilding).

Pia, ameitaka Menejimenti ya Wizara hiyo, kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu hususan tembo.

“Muweke mikakati ya kukabiliana na changamoto hii, Mtanzania ni lazima tumlinde, muwe macho muda wote kutoa taarifa kwa wananchi na kukutana na Serikali za vijiji kuwaelimishe wasifike katika maeneo ya korido za wanyamapori ”amesema Mhe. Chana na kuwataka kuweka alama madhubuti za kuonyesha kwamba ni korido.”

Waziri Chana ameongeza kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa majukumu na kuitaka menejimenti hiyo na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kukamilisha ahadi zote zilizoahidiwa kutekelezwa kipindi cha hotuba.
1724069219559.jpeg
1724069245644.jpeg

1724069205257.jpeg

1724069141603.jpeg
1724069156668.jpeg
1724069171794.jpeg
1724069188086.jpeg
 
Hadithi hadithi, uongo njoo, utamu kolea..
4R imekaa kinoko noko, hawana haya, hawana aibu, hawa masela aaahh….
 
Back
Top Bottom