Don Moen
JF-Expert Member
- Nov 12, 2020
- 1,636
- 3,142
WAZIRI ENG. MASAUNI
Naomba nikurudishe nyuma kidogo, miaka miwili nyuma ukiwa naibu waziri wa mambo ya ndani, ukiwa kama mwenyeketi wa usalama barabarani uliagiza kila mkoa ukusanye fedha za WIKI YA NENDA KWA USALAMA ambazo hutozwa kuanzia tsh 3,000 hadi 5,000
kwa kulingana na ukubwa wa gari husika.
Baada ya makusanyo hayo ulielekeza kila Mkoa ununue magari kwa ajili ya kusaidia utendaji wa kazi katika ofisi za ma RTO wa mikoa.
Katika maagizo yako hayo karibu mikoa yote ilijitahidi kukusanya kwa uaminifu na kutekeleza agizo lako kuwa walinunua magari kulingana na makusanyo ambapo mikoa iliyokusanya kidogo ilijitahidi kunua hata Noah.
Pamoja na mikoa mingine kutii agizo lako hilo. lakini Mikoa ya kipolisi ya Kinondoni, Ilala na Temeke haikutekeleza agizo lako hilo matokeo yake kuna tetesi kuwa Ofisi ya Kanda ilikusanya pesa zote na zikaishia mikononi mwa wajanja wachache.
Hivyo lengo la agizo lako halikutimizwa. Ili kuupata ukweli wa hili ni kazi rahisi tu ni kuwaita hao ma RTO watakueleza walipoelekeza hizo pesa.
Katika hili unayo nafasi nzuri ya kulifuatilia hili kwani sasa wewe ni Waziri kamili na hili lilikuwa agizo lako mwemyewe.
Mikoa hiyo ya kipolisi kwa ujumla haikosi kuwa na magari yasiyopungua 500,000 na ukizidisha kwa bei ya wastani ya 3,000x500,000=1,500,000,000. Hii ni pesa nyingi zingeweza kulisaidia jeshi la polisi. Naomba nisiwataje wahusika bali jaribu kufuatilia mwenyewe ndani ya muda mfupi utakua na majibu.
Mungu abariki utendaji wako.