Mhandisi Mzalendo
JF-Expert Member
- Aug 23, 2010
- 8,069
- 15,029
Aonye wanaowaua watu sio wanaoandamana kwa amani.
Serekali inataka kutumia nguvu kuwaondoa wakimbizi wa Kirundi walioishi Tanzaania kwa zaidi ya miaka 40! Yote hayo ya nini kama Mwafrika mwenzetu hajafanya uovu hapa nchini? Miaka ya 60 na 70 Tanzania tulikuwa na wakimbizi wengi sana kutoka Rwanda na Burundi. Baada ya ghasia kutulia kiasi huko makwao, Nyerere alitoa blanket offer kwa wakimbizi wote ama warudi makwao, au wachukue uraia wa Tanzania. Wachache walirudi makwao. Wengi wakachukua uraia wa Tanzania. Tatizo kwisha. Si busara kutumia nguvu dhidi ya mtu aliyekuwa akiishi nchini kwetu kwa miaka yote hiyo kama hajafanya uhalifu mwingine. Tuna mataizo mengi ya kutosha ya kushughulikia zaidi ya hilo la wakimbizi wa kutoka Burundi ambao wamekuwa wakiishi Tanzania kwa miongo na miongo.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, ametoa wito kwa vijana na wananchi wa Tanzania kulinda amani na kuepuka kushiriki maandamano, akisisitiza kuwa taifa bado linakabiliwa na athari nzito zilizosababishwa na maandamano ya Oktoba 29, 2025.
Amesema hayo usiku wa Novemba 28, 2025 katika burudani ya amani iliyofanyika Soko la Nyama Choma Kumbilamoto katika kata ya Vingunguti wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam akibainisha kuwa maandamano hayo yalisababisha vifo, uharibifu wa mali za serikali na binafsi pamoja na kusimama kwa shughuli za kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Simbachawene ameonya kuwa kuna taarifa za mipango ya maandamano mapya yanayotarajiwa kufanyika Desemba 9, 2025, akisisitiza kuwa Serikali haitaruhusu kutokea kwa vurugu nyingine na kuwaomba wananchi ‘kutotumika na kuchochewa kurudia makosa yaliyopita’.
Akirejea athari za maandamano ya Oktoba 29, Waziri Simbachawene amewataka vijana kufahamu gharama kubwa za uharibifu wa miundombinu, ikiwemo kuchoma vituo vya mabasi ya mwendokasi- mradi alioutaja kuwa umejengwa kwa ajili ya wananchi wasio na uwezo wa kumiliki magari. Amefafanua kuwa miradi hiyo inagharimiwa na kodi pamoja na mikopo ambayo vizazi vijavyo vitapaswa kuilipa.
Akizidi kusisitiza umuhimu wa amani, Waziri Simbachawene amesema Tanzania inaonekana kuonewa wivu kutokana na mafanikio yake, hivyo wananchi wanapaswa kuepuka kuvuruga misingi ambayo imeijengea nchi heshima na utulivu wa miaka mingi. Ameongeza kuwa baadhi ya majirani wa Tanzania wamekumbwa na migogoro kwa muda mrefu, akisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kujifunza kutokana na changamoto za mataifa hayo.
“Na leo hii nilikuwa na mkutano mkubwa sana wa utatu kati ya Tanzania, Burundi na UNHCR (Shirika la kuhudumia wakimbizi duniani), tunafikiria namna ya kuwarudisha wakimbizi wale wa Burundi kurudi kwao maana wamekaa hapa karibu miaka 40…sasa tunafikiria warudi kwao kwa sababu masharti ya ukimbizi yameisha hawataki kuondoka, tunafikiria kutumia ushawishi wa nguvu ili waweze kuondoka. Kama wakimbizi hawataki kuondoka kwetu halafu sisi hatuienzi na kuiheshimu amani ya nchi yetu tutakuwa sisi ni wajinga wa mwisho".
View attachment 3509173
Chanzo: Jambo Tv
Too late broWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, ametoa wito kwa vijana na wananchi wa Tanzania kulinda amani na kuepuka kushiriki maandamano, akisisitiza kuwa taifa bado linakabiliwa na athari nzito zilizosababishwa na maandamano ya Oktoba 29, 2025.
Amesema hayo usiku wa Novemba 28, 2025 katika burudani ya amani iliyofanyika Soko la Nyama Choma Kumbilamoto katika kata ya Vingunguti wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam akibainisha kuwa maandamano hayo yalisababisha vifo, uharibifu wa mali za serikali na binafsi pamoja na kusimama kwa shughuli za kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Simbachawene ameonya kuwa kuna taarifa za mipango ya maandamano mapya yanayotarajiwa kufanyika Desemba 9, 2025, akisisitiza kuwa Serikali haitaruhusu kutokea kwa vurugu nyingine na kuwaomba wananchi ‘kutotumika na kuchochewa kurudia makosa yaliyopita’.
Akirejea athari za maandamano ya Oktoba 29, Waziri Simbachawene amewataka vijana kufahamu gharama kubwa za uharibifu wa miundombinu, ikiwemo kuchoma vituo vya mabasi ya mwendokasi- mradi alioutaja kuwa umejengwa kwa ajili ya wananchi wasio na uwezo wa kumiliki magari. Amefafanua kuwa miradi hiyo inagharimiwa na kodi pamoja na mikopo ambayo vizazi vijavyo vitapaswa kuilipa.
Akizidi kusisitiza umuhimu wa amani, Waziri Simbachawene amesema Tanzania inaonekana kuonewa wivu kutokana na mafanikio yake, hivyo wananchi wanapaswa kuepuka kuvuruga misingi ambayo imeijengea nchi heshima na utulivu wa miaka mingi. Ameongeza kuwa baadhi ya majirani wa Tanzania wamekumbwa na migogoro kwa muda mrefu, akisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kujifunza kutokana na changamoto za mataifa hayo.
“Na leo hii nilikuwa na mkutano mkubwa sana wa utatu kati ya Tanzania, Burundi na UNHCR (Shirika la kuhudumia wakimbizi duniani), tunafikiria namna ya kuwarudisha wakimbizi wale wa Burundi kurudi kwao maana wamekaa hapa karibu miaka 40…sasa tunafikiria warudi kwao kwa sababu masharti ya ukimbizi yameisha hawataki kuondoka, tunafikiria kutumia ushawishi wa nguvu ili waweze kuondoka. Kama wakimbizi hawataki kuondoka kwetu halafu sisi hatuienzi na kuiheshimu amani ya nchi yetu tutakuwa sisi ni wajinga wa mwisho".
View attachment 3509173
Chanzo: Jambo Tv
Atoke hapa huyo Waziri feki anamfokea nani?Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, ametoa wito kwa vijana na wananchi wa Tanzania kulinda amani na kuepuka kushiriki maandamano, akisisitiza kuwa taifa bado linakabiliwa na athari nzito zilizosababishwa na maandamano ya Oktoba 29, 2025.
Aende zake huko tena akae kimya sio waziri halali huyo ni waziri feki anamwambia nani matamko yake hayo? Wananchi hatumtambuiWataanza lini kufanya tena mazoezi wale jamaa zake?
Sio kwa pesa za mama tena?inagharimiwa na kodi pamoja na mikopo ambayo vizazi vijavyo vitapaswa kuilipa.
JItokeze uone safari hii risasi ilivyo ya baridi ikiingiahuyo jamaa ni pathetic
njoo uwanjani tarehe hiyo usikie kitu cha baridi kikiiingia mwiliniAende zake huko tena akae kimya sio waziri halali huyo ni waziri feki anamwambia nani matamko yake hayo? Wananchi hatumtambui
ndo utajua matako yako hayaweszi kuzuia risasi siku hiyoLabda kama sisi ni matako yake
Tarehe 9 D ni maandamano ya amani nchi nzima
Tutaelewana tu si mnajifanya viziwi hamsikii tunataka nini basi mtasikia..njoo uwanjani tarehe hiyo usikie kitu cha baridi kikiiingia mwilini
Ni mwendo wa kutunishiana vifua.Hivi hakuna kiongozi mwenye Iq kubwa Serikalini anayeweza kusimama akalihutubia taifa mambo yanaoweza kushusha hasira za wananchi, mambo hayo machache mbona yanafahamika na kila mtu?
Kiongozi asimame akemee hadharani mambo ya utekaji, mauaji, kusingizia watu kesi, ku upgrade kesi kutoka za uzurulaji na kuwa kesi za uhaini ili kukandamiza raia.
Kueleza wazi hatua madhubuti zitakazochukuliwa kwa wale wote walioshiriki mauaji ya raia wasio na silaha D29 pamoja na kuwalipa fidia wote waliopoteza maisha.
Naendelea kujiuliza, hivi kweli Serikali nzima imeshindwa kubaini point ndogo hizi ili kuweza kuleta afueni kwenye mtanziko huu?
Haya mambo ya kuonya watu walio na hasira mioyoni mwao, tena walio na mamlaka juu ya nchi yao ni dharau na uvunjifu wa katiba.
Sasa wote tutaonyana, Serikali inatuonya wananchi na wananchi nao tunaionya Serikali, mwisho utakuwaje hapo?
Waziri feki.. mwambieni azime maikiAmeanza kutetea tumbo lake