Serekali inataka kutumia nguvu kuwaondoa wakimbizi wa Kirundi walioishi Tanzaania kwa zaidi ya miaka 40! Yote hayo ya nini kama Mwafrika mwenzetu hajafanya uovu hapa nchini? Miaka ya 60 na 70 Tanzania tulikuwa na wakimbizi wengi sana kutoka Rwanda na Burundi. Baada ya ghasia kutulia kiasi huko makwao, Nyerere alitoa blanket offer kwa wakimbizi wote ama warudi makwao, au wachukue uraia wa Tanzania. Wachache walirudi makwao. Wengi wakachukua uraia wa Tanzania. Tatizo kwisha. Si busara kutumia nguvu dhidi ya mtu aliyekuwa akiishi nchini kwetu kwa miaka yote hiyo kama hajafanya uhalifu mwingine. Tuna mataizo mengi ya kutosha ya kushughulikia zaidi ya hilo la wakimbizi wa kutoka Burundi ambao wamekuwa wakiishi Tanzania kwa miongo na miongo.