Waziri wa Michezo Mchengerwa unavyosema Simba na Yanga sasa 'zitaitii' Serikali unajielewa Wewe?

Waziri wa Michezo Mchengerwa unavyosema Simba na Yanga sasa 'zitaitii' Serikali unajielewa Wewe?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Hivi hapo Wizarani Kwako hakuna Watendaji waliokuzidi Akili ambazo huna ili wawe Wanakusaidia Kiushauri na usiwe Unakurupuka Kimaongezi?

Waziri Mchengerwa nani alikudanganya kuwa Vilabu vya Simba na Yanga vinamilikiwa na vinasimamiwa na Serikali yako mpaka leo katika Hafla ya Kuwopongeza Tembo Warriors ukasema kuwa vitakuwa Vinatii Muongozo wa Serikali yako katika Kufanikiwa Kwao Kimataifa Klabu Bingwa na Shirikisho?

Yaani Waziri mzima wa Michezo nchini Tanzania hujui kuwa Timu pekee iliyo mikononi mwako na Serikali yako ni ya Taifa Stars na nyinginezo ila huku Simba SC na Yanga SC hamna Ubavu huo wa Kuviamrisha na Kuvishurutisha kama usemavyo na utakavyo?

Tena kwa faida yako sasa ni kwamba hivi Vilabu vikubwa Viwili vya Tanzania ndiyo vina Nguvu ya Kiushawishi Kisiasa, Kijamii na Kiuchumi na vikiamua Mgombea Binafsi GENTAMYCINE niwe Rais wa Tanzania na Mkweo aangushwe mwaka 2025 vinaweza na ndiyo maana Serikali zote zilizopita ziliziheshimu zaidi Simba SC na Yanga SC na bila Nguvu yao Kubwa huenda mwaka 2005 mwana Yanga SC Rais Mstaafu Kikwete asingeshinda na huenda pia hata mwaka 2015 mwana Simba SC Hayati Rais Dkt. Magufuli asingeshinda.

Wewe ni Waziri wa hovyo kupita Maelezo katika hiyo Wizara ya Michezo na sijui ni Sifa zipi zilikuweka hapo na kila Siku nakuona Unaharibu tu badala ya kupatia.
 
Yule lejendari wa kutafunwa na kauli zake.

Aliwahi kusema mtu ukiwa shabiki wa uto hata uwe na phd unakuwa hamnazo hivi
 
Huyu chengerwa atakuwa na element za uto uto
Aundo wale walitajwa kwenye list ya ashura pale utoni
 
Hiyo nguvu angeitumia kwenye timu ya Taifa labda ingesaidia maana huko ndo kuna changamoto nyingi. Ya Simba na Yanga hawamuhusu ye atazame kwa macho tu!
 
Yanga wapambane kama vipi waombe viongozi wawafungie magoli.
Kimataifa hakuna kubebwa wala kuzihonga timu pinzani ili Yanga ishinde.

Wakati Simba anaanza kuingia anga za kimataifa Yanga walifanya hujuma za wazi kabisa na viongozi walikuwa Kimya kama hawaoni vile.

Nendeni mkachezee kichapo Sudani hakuna nmna nyingine.
Ili mkomae.
 
Thread Imeanzishwa Na Gwini Halafu Imenyooka Haina Makandokando Imegonga Mshono Ikaufumua Wote, Sasa Chukueni Ushauri, Maoni, Mkayafanyizie Kazi
 
Back
Top Bottom