Waziri wa Mifugo kubishana hadharani na Rais ni utovu wa nidhamu

Si kweli,jambo la Kisheria linaenda kwa Mamlaka ya sheria.
 
Hujaona wapi ? waziri yuko sahihi tunataka vitu vifanywe kitalaamu na si kukurupuka tu.hizo ni siasa kiuhalisia huwezi tu kuikabidhi Narco kwani hao wanauwezo wa kuendesha Narco?
 
Boss wako anapokupa maagizo hata kama si sahihi huna budi kuyafuata.

Rais sio Mama yako anayeweza kukutuma bombani ukachote maji na usitii amri kwa kisingizio cha kuchoka.
Hata jambo la hovyo unakubaliana naye sababu tu ni Boss.sisi watz huu ujinga ndo unatufikisha pabaya.mbona Ruto walitofautiana na Uhuru ?
 
Sasa kwa akili yako ulitaka lijibiwe, "ndiyo mama sasa tunaenda kuwakusanya vijana tuwagawie vitalu"
Mali ya serikali haigawanywi hivyo!
 
Huu ni uchonganishi wenye nia OVU dhidi ya huyo waziri wa kilimo, inawezekana mnaitaka hiyo nafasi......
 
Hata jambo la hovyo unakubaliana naye sababu tu ni Boss.sisi watz huu ujinga ndo unatufikisha pabaya.mbona Ruto walitofautiana na Uhuru ?
Yaani kuna watu wanaandika vitu mpaka unashangaa kama waliwahi kuingia darasani
 
Kwanini asibishiwe kama hayupo sahihi. Kwani Raisi ni Mungu akili zako funza kabisa wewe
Hutakiwi kumbishia hadharani
Kwanini asibishiwe kama hayupo sahihi. Kwani Raisi ni Mungu akili zako funza kabisa wewe
Hutakiwi kumpinga hadharani,pale unakubali Kisha pembeni ndiyo unatoa hayo maoni/ushauri wako,tatizo vijana hatujui utaratibu
 
Mashimba Ndaki ana mfumo dume wa kisukuma shida ipo hapo.....plus aliemteua aahhhh
 
Yule wa nishati aliewaita KAMATI YA BUNGE wapuuzi hajadharau mhimili wa Bunge?

Narudia, Waziri wa mifugo anapewa JINA BAYA Ili atumbuliwe!!!!!

Fanyeni, ni muda wenu, ingawa na mchache!!!!
 
Taahi.ra wewe, wapi na lini Rais alisema wapewe vijana wa SUA? hivi unajua vyuo vya mifugo vya serikali (LITA) vinazalisha vijana wangapi kwa mwaka? wenyewe waende wapi?
 
Pale kuna mikataba ya watu na Serikali, kwaiyo Waziri huwezi kuamua tu Kama Mwenyekiti wa VICOBA lazima taratibu zifuatwe,mnataka Mashimba akurupuke alafu baadaye kibubu Cha wanyonge kichotwe fedha za fidia baada ya serikali kushitakiwa kwa kukiuka mikataba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…