Mo graphics 2019
JF-Expert Member
- Oct 14, 2019
- 1,002
- 1,483
Yuko sahihi shida ni uchawa unawasumbua ndo mnakua akina ndio ndio.Tumeshuhudia Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki akipinga hadharani maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyeagiza vitalu vya NARCO vifutwe na kupewa vijana wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo SUA ili kutengeza fursa za ajira kupitia ufugaji
Mambo ambayo Waziri alipaswa kuyafanya ni mawili ama kutekeleza maagizo aliyopewa na Mh. Rais kama yalivyo ama kuandika barua ya kujiuzulu na sio kupingana na Mh Rais hadharani na kusema kabisa kwamba anaunda timu ya wataalamu ili kuishauri Sekali.
Hii ni sehemu ya nukuu ya Waziri Mashimba " jambo hili tumelipima na tukaliona linahitaji umakini mkubwa na kwa hiyo ili kutekeleza jambo hili wizara tumeunda timu ya wataalamu kutoka wizara na taasisi mbalimbali zinazohusika na mambo mbalimbali sasa timu hii tunataka ifanye tathmini ya kina ya utendaji na changamoto zilizoko ndani ya Narco ili tuweze kuishauri sawasawa Serikali"
Huu ni utovu wa nidhamu uliopitiliza lakini tukisema humu mnaanza kuhusisha mambo yenu ya udini na ukabila, sijawahi kuona Waziri anapingana na Rais wake kwa sababu madaraka ya waziri amekasimiwa na Mh Rais sasa unaposema anaundia timu ya wataalamu maagizo ya Mh Rais maana yake nini.
Haya twende, Huyo mhitimu wa SUA anapewa kitalu Ng'ombe anazitoa wapi? Au anapanda nyasi kwenye hicho kitalu?
Wazo la mheshimiwa huenda ni zuri ila sio rahisi kama mnavyo liona.
NARCO huwa wanawakodishia Wafugaji vitalu, wao wanakuja kulisha mifugo yao inapata malisho inanenepa na wanapata fedha ya kulipa na kodi ya kukodishiwa kitalu.
Sasa huyu mwanafunzi anapewa kwa muktadha upi? Amekodi au kapewa msaada? Na atapewa kwa muda gani? Ni lazma wizara ikae na wadau waujadili huo mpango kwa pamoja lasivyo sio kitu rahisi.
Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app