Waziri wa nishati aitangaze orodha ya Watanzania ambao Hadi Sasa wameshalipia Tsh 27,000 za kufungiwa umeme Mjini. Tanesco kuna mgomo baridi

Mh waziri pale Tanesco mkuranga Meneja anawalea watendaji wanao kura rusha kwa kuchukua pesa za watu wakiwaahidi watawaunganishia umeme tume peleka tuhuma hizo lakini yule meneja wa tanesco mkuranga hazifanyii kazi mh waziri kwa dahamana uliyopewa na mamlaka uliyopewa ondoa yule meneja na watendaji wake wabovu vinginevyo tuta tumia software za kiafrica
 
Ah Tanesco Kibaha NI JIPU Sugu pale
 
Changamoto ni kubwa sana. Nimepata control number ya kulipia 27,000 baada ya miezi mitatu ya kufuatilia. Nimelipia hiyo pesa na bado sijafungiwa LUKU separate ya eneo la biashara. Ni mwezi wa nne Sasa umeingia.... Siku zinazidi kukatika.

Kumbuka sihitaji nguzo ni wire tuuu toka nguzo ya jirani. Mpaka Leo sijapata huduma hii. Nimefuatilia mpaka niseme inachosha kwa kweli.... TANESCO Mnafanya kazi kwa utaratibu upi?? Sisi si ndio wateja wenu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…