Waziri wa sasa wa fedha wa Tanzania ana exposure gani kwenye uchumi?

Waziri wa sasa wa fedha wa Tanzania ana exposure gani kwenye uchumi?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Mawazo na mpangilio wa hoja wa Mhe. Mwigulu Nchemba unakosa ladha ya utaalamu wa uchumi. Anajadili issues too theoretical au kama mtu aliyehitimu darasani akahama na skills za darasani kwenda kuongoza.

Kwa nchi hii na rasilimali tulizonazo zinazonufaisha wageni inasikitisha kuona Waziri anaagenda yakutoza Kodi ya vocha, vifurushi na mafuta.

Katika maisha ya kawaida huitaji kuwa mchumi uweze kung'amua kwamba ukiweka Kodi kwenye vocha, mafuta na vifurushi hautopata fedha utapata. Swali alilopaswa kujiuliza nikwanini mataifa mengine hayana tozo kwenye huduma hizi? Alipaswa kujiuliza kwanini mafuta Zambia yapo chini wakati yanapita dar es salaam?

Alipaswa kujiuliza kupandisha mafuta kwa kuongeza shs mia je Kuna athari kubwa kiasi gani kwenye sekta nyingine? Kwa mpangilio wake wa hoja naamini ajawahi kufanya kazi nje ya Tanzania, hajawahi kusimamia taasisi ikasogea, amepata Uwaziri kwa sababu yeye ndiyo msomi kwenye sekta hii katika wabunge waliopo bungeni.

Leo kwake yeye anavyoona biashara ya magendo inaanza kurudi kwamba watu wananunua mafuta nje anaamini Watanzania wanakosa uzalendo? Seriously Waziri wa fedha anaongelea price ziwe juu then watu wawe Wazalendo? Hizi ndizo economic principles alizofunzwa?

Nadhani kwa kuwa ndo tumefika point kila mtu anaweza kuwa Waziri Basi tuendelee kusubiri miaka 60 mingine
 
Kwa ujumla tuna waziri. Alisoma uchumi lakini hajawahi kuwa mchumi. Hana chapisho lolote la taaluma yake. Miaka yote alifundishwa akakariri na kujibu hadi akapewa Ph.D. Kwa ufupi hajawahi kufikiri kiuchumi, lakini alipendwa na Kikwete kwa mipasho yake.
 
Hapo ndio utajua tofauti ya kuhudhuria shule na kuelimika.
Kwa ujumla tuna waziri. Alisoma uchumi lakini hajawahi kuwa mchumi. Hana chapisho lolote la taaluma yake. Miaka yote alifundishwa akakariri na kujibu hadi akapewa Ph.D. Kwa ufupi hajawahi kufikiri kiuchumi, lakini alipendwa na Kikwete kwa mipasho yake.
Well said, mkuu mwingulu ni mchumi wa theoretical zaidi kuliko Realistic
 
Kwa nchi zetu za kiafrika kusoma siyo kuelimika.Wanafanya ufisadi siyo darasa la saba ndio hawa hawa wanaojimwambafy ni maDr na maProf.Afrika,soma ule basi ndio maana wanapenda kweli kuanza na title Dr.....,Prof.......Kwa wenzetu ujinga huo haupo
 
Mchumi alituaminisha kuwa upinzani wanavikundi vya ugaidi.
Mchumi akaahidi kuutoa ushahidi mbinguni na duniani.
Mchumi amesema wananchi tujifunge viuno.
Kazi iendelee
 
"Mtu anayetuma 1000 hadi 2000 anakatwa Tsh.10, anayetuma 20,000 hadi 30,000 anakatwa 960, Mil. 1 hadi Mil. 3 ni 9000 na Mil 3 na kuendelea ni 10,000, kwa anaetuma 100,000 hadi 200,000 anakatwa 2500, kama unaweza kutuma 10,000 kwanini usichangie shughuli za maendeleo?”

"Kwenye chungu, ni lazima bajeti, fedha zitatoka wapi ni lazima tutoe kodi, mwaka huu tumeleta kodi ya miamala, ni vizuri sana mjue hili la kwenye miamala sio tu kodi, hili tunatunisha mfuko, ni solidarity fund, huu ni mfuko wa mshikamano wa Watanzania"

"Sisi wenzenu tunaotafsiri dira ya Rais Samia, tumesema itakuwa aibu mno kwa kizazi hiki cha leo ziwepo shughuli zinakwama sababu tu tunataka tusitoe kodi, kwamba tusubiri tuletewa wengine wanaoweza kutozana kodi kutoka Nchi nyingine, hii haileti heshima kwa Nchi yetu na wala hailindi Uhuru wa Nchi yetu, Nchi inapokuwa huru ni lazima ijitegemee"———-Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba kwenye Clouds 360
 
Back
Top Bottom