Waziri wa sasa wa fedha wa Tanzania ana exposure gani kwenye uchumi?

Waziri wa sasa wa fedha wa Tanzania ana exposure gani kwenye uchumi?

"Mtu anayetuma 1000 hadi 2000 anakatwa Tsh.10, anayetuma 20,000 hadi 30,000 anakatwa 960, Mil. 1 hadi Mil. 3 ni 9000 na Mil 3 na kuendelea ni 10,000, kwa anaetuma 100,000 hadi 200,000 anakatwa 2500, kama unaweza kutuma 10,000 kwanini usichangie shughuli za maendeleo?”

"Kwenye chungu, ni lazima bajeti, fedha zitatoka wapi ni lazima tutoe kodi, mwaka huu tumeleta kodi ya miamala, ni vizuri sana mjue hili la kwenye miamala sio tu kodi, hili tunatunisha mfuko, ni solidarity fund, huu ni mfuko wa mshikamano wa Watanzania"

"Sisi wenzenu tunaotafsiri dira ya Rais Samia, tumesema itakuwa aibu mno kwa kizazi hiki cha leo ziwepo shughuli zinakwama sababu tu tunataka tusitoe kodi, kwamba tusubiri tuletewa wengine wanaoweza kutozana kodi kutoka Nchi nyingine, hii haileti heshima kwa Nchi yetu na wala hailindi Uhuru wa Nchi yetu, Nchi inapokuwa huru ni lazima ijitegemee"———-Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba kwenye Clouds 360

Mhhhhhh "hao wanaotafsiri dira ya Rais" hawajasikia wanavyopigiwa kelele kuwa wakatwe kodi? mbona wameweka pamba masikioni.
 
N/waziri wa fedha ni Eng,
Kuna siku niliona anatoa semina elekezi kwa maofisa wa hazina.
Halafu ndio mshauri wa waziri wa fedha.

Kuna wizara tunafanyia maigizo ndio maana malalamiki hayaishi
 
Mawazo na mpangilio wa hoja wa Mhe. Mwigulu Nchemba unakosa ladha ya utaalamu wa uchumi. Anajadili issues too theoretical au kama mtu aliyehitimu darasani akahama na skills za darasani kwenda kuongoza.

Kwa nchi hii na rasilimali tulizonazo zinazonufaisha wageni inasikitisha kuona Waziri anaagenda yakutoza Kodi ya vocha, vifurushi na mafuta.

Katika maisha ya kawaida huitaji kuwa mchumi uweze kung'amua kwamba ukiweka Kodi kwenye vocha, mafuta na vifurushi hautopata fedha utapata. Swali alilopaswa kujiuliza nikwanini mataifa mengine hayana tozo kwenye huduma hizi? Alipaswa kujiuliza kwanini mafuta Zambia yapo chini wakati yanapita dar es salaam?

Alipaswa kujiuliza kupandisha mafuta kwa kuongeza shs mia je Kuna athari kubwa kiasi gani kwenye sekta nyingine? Kwa mpangilio wake wa hoja naamini ajawahi kufanya kazi nje ya Tanzania, hajawahi kusimamia taasisi ikasogea, amepata Uwaziri kwa sababu yeye ndiyo msomi kwenye sekta hii katika wabunge waliopo bungeni.

Leo kwake yeye anavyoona biashara ya magendo inaanza kurudi kwamba watu wananunua mafuta nje anaamini Watanzania wanakosa uzalendo? Seriously Waziri wa fedha anaongelea price ziwe juu then watu wawe Wazalendo? Hizi ndizo economic principles alizofunzwa?

Nadhani kwa kuwa ndo tumefika point kila mtu anaweza kuwa Waziri Basi tuendelee kusubiri miaka 60 mingine
Phd from UDSM, akili ya kuku na bado akaondoka na Phd
 
Mwigulu anao uwezo wa kutumia laki kwa siku kununua vocha,hivyo hawezi kuona makali ya maisha.

Vocha anapewa fungu na ofisi kwa mawasiliano, kodi halipi kutoka kwenye mshahara wake. Saa ngapi mtaongea nae lugha moja mkaelewana?

Ni kama mnaishi dunia mbili tofauti.
 
Ameamua kuwa mbunifu na siyo kuiga eti nchi Fulani wanafanya hivi nami nifanye Kama wao.

Unataka muige mpaka lini?
Umemsoma vizuri mleta UZI!? Hajalaumu ku copy kutoka nchi zingine, kauliza "unadhani ni kwanini nchi zingine hazitozi kodi kwenye hayo maeneo!?" Mbona vitu vingine ni virahisi tu kuvielewa, havihitaji shule kubwa hadi upotoshe alicho sema mleta UZI!?
 
Maadui zetu bado ni wale wale tu:

Ujinga
Umasikini
Maradhi

The circle in that order.
 
Mawazo na mpangilio wa hoja wa Mhe. Mwigulu Nchemba unakosa ladha ya utaalamu wa uchumi. Anajadili issues too theoretical au kama mtu aliyehitimu darasani akahama na skills za darasani kwenda kuongoza.

Kwa nchi hii na rasilimali tulizonazo zinazonufaisha wageni inasikitisha kuona Waziri anaagenda yakutoza Kodi ya vocha, vifurushi na mafuta.

Katika maisha ya kawaida huitaji kuwa mchumi uweze kung'amua kwamba ukiweka Kodi kwenye vocha, mafuta na vifurushi hautopata fedha utapata. Swali alilopaswa kujiuliza nikwanini mataifa mengine hayana tozo kwenye huduma hizi? Alipaswa kujiuliza kwanini mafuta Zambia yapo chini wakati yanapita dar es salaam?

Alipaswa kujiuliza kupandisha mafuta kwa kuongeza shs mia je Kuna athari kubwa kiasi gani kwenye sekta nyingine? Kwa mpangilio wake wa hoja naamini ajawahi kufanya kazi nje ya Tanzania, hajawahi kusimamia taasisi ikasogea, amepata Uwaziri kwa sababu yeye ndiyo msomi kwenye sekta hii katika wabunge waliopo bungeni.

Leo kwake yeye anavyoona biashara ya magendo inaanza kurudi kwamba watu wananunua mafuta nje anaamini Watanzania wanakosa uzalendo? Seriously Waziri wa fedha anaongelea price ziwe juu then watu wawe Wazalendo? Hizi ndizo economic principles alizofunzwa?

Nadhani kwa kuwa ndo tumefika point kila mtu anaweza kuwa Waziri Basi tuendelee kusubiri miaka 60 mingine
Darasani alifanya vizuri sana,na amefanya kazi benki kuu kwa muda mrefu tu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Vocha anapewa fungu na ofisi kwa mawasiliano, kodi halipi kutoka kwenye mshahara wake. Saa ngapi mtaongea nae lugha moja mkaelewana?

Ni kama mnaishi dunia mbili tofauti.
Mswahili akiwa na njaa ndio huwa na akili.We angalia maraisi wote na 80% ya viongozi wote washawahi kuwa walimu shida na tabu za wenzao wanazijua lakini walipopata tu madaraka hata wa kuwaza tu kuwainua waalimu hayupo washaasau wote.
 
Kwa nchi zetu za kiafrika kusoma siyo kuelimika.Wanafanya ufisadi siyo darasa la saba ndio hawa hawa wanaojimwambafy ni maDr na maProf.Afrika,soma ule basi ndio maana wanapenda kweli kuanza na title Dr.....,Prof.......Kwa wenzetu ujinga huo haupo
Hahahahaaaa.. mambo hayo kama ya Brigedia Dkt.........Tz watu Kwa title hawajambo, lakini hebu njoo kwenye tija kulingana na hizo qualifications kizungumkuti.........matokeo yake ndio mbunge Msukuma huwa akihoji wanamtolea povu.....kazi kwelikweli.
 
Aweke hapa publication zake kwenye international peer reviewed journals kama walivyo watu kama prof. Lipumba. Kuna theory zozote au hypothesis za kiuchumi alizofanyia kazi zikaja na matokeo? au kaishia tu kujificha kwenye phd ya kutunukiwa hapo mlimani...
 
Back
Top Bottom