Waziri wa sasa wa fedha wa Tanzania ana exposure gani kwenye uchumi?

Waziri wa sasa wa fedha wa Tanzania ana exposure gani kwenye uchumi?

Ameamua kuwa mbunifu na siyo kuiga eti nchi Fulani wanafanya hivi nami nifanye Kama wao.

Unataka muige mpaka lini?
Mimi bwana nilpata A ya Basic Math O level na B ya Advanced Maths A level enzi hizo Mkapa anamalizia awamu ya pili. Il leo ukinuliza somo gani muhimu duniani mtu kujifunza nitakwambia History. History ni somo lenye umuhimu sana. Ukitaka kufanya jambo na ufanikiwe, unapaswa kufuanya walivyofanya wengine waliokua katika hali yako na wakafanikiwa. Karibuni nchi zote duniani zimewahi kuwa na hali kama yetu na wengine walifanikiwa wakatoka, njia walizotumia kufanikiwa zipo, kwanini hatuzitumii?
 
Bachelor of Economy - UDSM, 2004
Masters of Economy - UDSM, 2006
PhD in Economics - UDSM, 2017
===
Amewahi kufanya kazi kwenye daraja la - Economist I Bank of Tanzania, 2006 - 2010.

Bachelor of economy
Masters of economy
Ndiyo nini??
 
Wenye akili hawana Mamlaka ,wenye Mamlaka hawana akili.
Wajinga wanajiamini,wenye akili sana full wasiwasi,hili ni zaidi ya Tatizo kwa Nchi za Afrika.
 
Kwanini asipewe Charles Kimei maana tunajua mchango wake katika sekta fedha?
 
Kwanini asipewe Charles Kimei maana tunajua mchango wake katika sekta fedha?
Huyo Kimei wenu akili zake kama za Magufuli atahamisha hadi Wizara iende Kilimanjaro.

Acheni kuriri kama Kikwete alivyo kariri kuwa Magufuli ni jeuri basi naye pasipo hata kushirikisha ubongo wake akaamua atukomoe Watanzania kumbe ana haribu misingi yote ya Nchi.
 
Mleta uzi you have a point, jamaa alikua anajib maswali ya msingi aliyokuwa akiulizwa pale Clouds kwa majibu ya darasani kabisa ( too theoretical) mpk nikashindwa kabisa kumuelewa km huyu ndio Waziri wa fedha
 
..mama amrudishe nyumbani dr.stergomena tax ambaye ni katibu mtendaji wa sadc.

 
Kwa ujumla tuna waziri. Alisoma uchumi lakini hajawahi kuwa mchumi. Hana chapisho lolote la taaluma yake. Miaka yote alifundishwa akakariri na kujibu hadi akapewa Ph.D. Kwa ufupi hajawahi kufikiri kiuchumi, lakini alipendwa na Kikwete kwa mipasho yake.
Wakuu punguza ni shombo kwa kila kitu, fuatilia kwa makini utamuelewa Mwigulu siyo unavyomdhania. Kwa kujihusisha na masuala ya fedha na uchumi Benki kuu na wizara ya fedha kwa zaidi ya miaka 20, inatosha kwa mwanasiasa.
 
Wakuu punguza ni shombo kwa kila kitu, fuatilia kwa makini utamuelewa Mwigulu siyo unavyomdhania. Kwa kujihusisha na masuala ya fedha na uchumi Benki kuu na wizara ya fedha kwa zaidi ya miaka 20, inatosha kwa mwanasiasa.

..he is a downgrade from Dr.Phillip Mpango.

..wizara inahitaji mchumi aliyebobea kwa ku-practice taaluma yake ndani na nje ya Tz.

..Na yule mama ambaye ni Naibu pia anapaswa kubadilishwa.
 
Bachelor of Economy - UDSM, 2004
Masters of Economy - UDSM, 2006
PhD in Economics - UDSM, 2017
===
Amewahi kufanya kazi kwenye daraja la - Economist I Bank of Tanzania, 2006 - 2010.
Sio dharau lakini elimu ya UD mpaka PhD ni utata kidogo, nondo za UD sio deep , useless and outdated theories kibao na kukariri tuu, no creativity or thinking outside the box na research ni zero, angalia budget ya UD ni ya kulipa mishahara tuu na umeme and what do you expect?
 
Halafu hajawai kufanya biashara popote tufike sehemu tuwatumie watu ambao angalau wameshafanya biashara wakaonja machungu ya ulipaji kodi
Achilia mbali kufanya biashara, hapo alipo mshahara wake hakatwi kodi.
 
Huyu hayajui maisha halisi ya watz,ni bora hizi bajeti za uchumi wangekuwa wanapewa wanafunzi wa vyuo waziandae angalau wapo karibu na wananchi.
 
Acha kuwa kima wewe,kwani tozo ulizotaja hazikuwepo? Zimekuwepo miaka mingi isipokuwa alichofanya Waziri wa Fedha ni kuongeza tozo kidogo na kuzielekeza kwenye specific activities na sio kwenye mfuko mkuu wa serikali.

Matokeo yake yamekuwa na tija kuliko kuacha kwa mtu binafsi,ukiniuliza mimi nimefurahi maana sasa kuna uhakika wa barabara,afya na maji.

Hapa nampongeza Waziri maana hii nchi ukimwambia mtu adai risiti na kutoa risiti kila anaponunua hafanyi sasa kwa njia hii ni kupata kile ambacho kilistahili.

Na hizi kelele zimeanza kupungua na maisha yanaendelea kama kawaida.Ukiwasikiliza nyie pimbi wa jf unaweza dhani Hali ni mbaya sana mtaani wakati si kweli na magari watu wananunua na yako barabarani kama kawaida.
 
Bachelor of Economy - UDSM, 2004
Masters of Economy - UDSM, 2006
PhD in Economics - UDSM, 2017
===
Amewahi kufanya kazi kwenye daraja la - Economist I Bank of Tanzania, 2006 - 2010.
kwa hiyo ulitakaje mana upo nje ya uzi
 
Back
Top Bottom