"Mtu anayetuma 1000 hadi 2000 anakatwa Tsh.10, anayetuma 20,000 hadi 30,000 anakatwa 960, Mil. 1 hadi Mil. 3 ni 9000 na Mil 3 na kuendelea ni 10,000, kwa anaetuma 100,000 hadi 200,000 anakatwa 2500, kama unaweza kutuma 10,000 kwanini usichangie shughuli za maendeleo?”
"Kwenye chungu, ni lazima bajeti, fedha zitatoka wapi ni lazima tutoe kodi, mwaka huu tumeleta kodi ya miamala, ni vizuri sana mjue hili la kwenye miamala sio tu kodi, hili tunatunisha mfuko, ni solidarity fund, huu ni mfuko wa mshikamano wa Watanzania"
"Sisi wenzenu tunaotafsiri dira ya Rais Samia, tumesema itakuwa aibu mno kwa kizazi hiki cha leo ziwepo shughuli zinakwama sababu tu tunataka tusitoe kodi, kwamba tusubiri tuletewa wengine wanaoweza kutozana kodi kutoka Nchi nyingine, hii haileti heshima kwa Nchi yetu na wala hailindi Uhuru wa Nchi yetu, Nchi inapokuwa huru ni lazima ijitegemee"———-Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba kwenye Clouds 360